Amri ya hakimu ni hatari


Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 09 May 2011

Printer-friendly version

Unajua kwa nini hakimu anapiga marufuku kuandikwa habari za kesi ya Manji na Mengi? Ni kutokana na upotoshaji mnaoufanya waandishi. Ebu angalia wewe fidia uliyoiandika (ya Sh. 1/=) kuwa Manji anadai. Hivi iposahihi au unapotosha umma? Kuweni makini katika uandishi na uhariri wa habari zenu. Ila mnajitahidi kimawazo na kimtazamo. 0756308805. (Hakika Manji anadai Sh. 1 tu. Mhariri)

Habari hii inasikitisha sana, hasa kwa taifa hili linalohubiri ukweli na uwazi. Huyu mheshimiwa hakimu anafikiri bado tuko kwenye enzi zipi, kwamba ukisema “kimya!” inakuwa hivyo. 0712155790

Huu uchambuzi wako unatisha. Nashauri uweke wazi maoni yetu kwenye toleo lijalo ili taifa lijue  kwa undani namna huyu hakimu anavyotaka tusipate kinachoendelea mahakamani. Leo amezuia tusijue lolote juu ya kesi ya Mengi na Manji. Msishangae … kesho vyombo vya habari vikachimbwa mkwara kuripoti makubwa zaidi…. Samuel Vilima, Sumbawanga 0752236789

Nimefurahi nimepata uchambuzi wako juu ya amri ya hakimu Kisutu. Tunakuombea kwa Mungu. 0712146090

Naunga mkono hoja yako ya kugomea maamuzi ya hakimu kesi ya Mengi na Manji. Hapo hakimu amechemka. Hajatutendea haki kabisa wananchi kwa kuwa tuhuma za ufisadi zinaguza umma, siyo mtu binafsi. Naunga mkono hoja yenu waandishi. Lazima mjadili suala hili kwani huko mbeleni mwaweza kukabiliwa na kitisho cha aina hiyohiyo ya uamuzi. Fadhil Ngajiro, Mwenyekiti UV-CCM, Iringa 0784609477

Ndiyo, amri hii ya hakimu wa Kisutu  haifai kabisa, Martin, Babati 0784474940

Mimi naamini ni harakati dhidi ya media ila hizi ni dalili za kuelekea kushindwa (watawala) katika jamii yetu. 0713278910

Ninachojua mahakimu au majaji wanayo sheria inayowalinda kuzuia kesi kuongelewa wakati shauri bado lipo mahakamani… Wako Mwiyi. 0714 890790

Kesi ya Zombe na wenzake ni kati ya kesi ngumu zilizowahi kutokea na iliripotiwa na waandishi wa habari hadi hukumu… Hii ina nini? 0715348448

Habari za kuadimika. We missed your sparkling analysis. Maoni yangu kuhusu amri ya hakimu Kisutu ni hivi: It is irrelevant (haina maana) kujadili amri ya Mgeta; cha kujadili hapa ni hii fidia anayoidai Manji – Sh. 1 ya Tanzania. Kuna kesi nyingi sana na muhimu  hazijashughulikiwa. Watu wanasota na kuozea rumande. Leo hii mnashabikia na kulilia  kuripoti kesi ya…anayedai fidia ya shilingi moja. Uko wapi uzalendo wenu. Uko wapi weledi. Dk. M. Lupembe (Ph.D) 0788397692.

Your article deserves international award (makala yako inastahili tuzo ya kimataifa) 0717422334
 
Makala yako katika MwanaHALISI ni nzuri. Lakini kwenye zama hizi… wenye kutaka umoja wa kupigania nchi ni wachache. 0754 882861

Amri zinazokataza matendo ya usambazaji habari zinavunja nguzo ya uwazi; nguzo muhimu kwenye kujenga demokrasia. Lakini jambo moja ni dhahiri Ndimara, mara kadhaa waandishi hawaripoti ipasavyo taarifa za mahakamani na nyingine zinazohusisha sheria. Athari za maneno/maamuzi mengi ya kisheria ni tofauti sana na vile inavyoweza kueleweka kwa akili ya kawaida. Siungi mkono amri ya hakimu; lakini wanahabari pia wana wajibu wa kujua kuripoti taarifa za mahakama. Mallya John. 0719285060

 

Urithi…mbinu, namna na aina ya uandishi wako uliotukuka, utamwachia nani? Mwandae sasa. Mwankemwa, Bagamoyo. 0769500554

0
Your rating: None Average: 5 (1 vote)
Soma zaidi kuhusu: