Bunge

CCM wanasikilizwa, CHADEMA wanaheshimika
- MWENENDO WABUNGE WETU
MKUTANO wa Bunge la bajeti unaendelea mjini Dodoma, pamoja na kwamba wananchi wengi wamekatishwa tamaa na mwenendo wa serikali, lakini bado wanaendelea kufuatilia mjadala wake.

Kiti cha spika kimezidi wanaokikalia?
KITI cha spika kinaweza kuwa ni kikubwa “mno” kuliko uwezo wa waliopo kukikalia iwapo wahusika hawa hawatakuwa wanapima athari za maamuzi yao kuhusu miongozo ya wabunge.

Pinda na danadana kuhusu Zanzibar
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezidi kupiga “danadana” ahadi yake ya kulipa kifuta machozi kwa familia zilizopoteza raia wakati wa maandamano yaliyoitishwa na Chama cha Wananchi (CUF) kudai uchaguzi mpya baada ya ule wa 2000 kuvurugwa kwa nia ya “kupendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).”

Udhaifu wa JK bungeni
KAMBI ya upinzani imerejesha mjadala wa “udhaifu wa rais” bungeni kwa kutaja maeneo mbalimbali ambayo Rais Jakaya Kikwete alitakiwa kuchukua hatua, lakini badala yake alikaa kimya.

Wabunge, hasira haziijengi Bajeti
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juzi jioni lilitibuka. Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walitibua hali ya hewa kwa kutoa lugha chafu.

Tulichojifunza kutoka bungeni Dodoma
MKUTANO wa sita wa Bunge la 10 uliokuwa na vikao tisa, umemalizika. Swali, wananchi wamejifunza nini kutokana na vikao hivyo vilivyomalizika?
Ni katika mkutano huo wananchi wameshuhudia kwa mara ya kwanza Ikulu, Ofisi ya Spika na Waziri mkuu zikishindwa kusema ukweli. Ongezeko la posho za wabunge ndilo lilikuwa chanzo cha mtafaruku.

Nani muasi, Kikwete au wabunge?
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimesherehekea miaka 35 tangu kizaliwe. Kilele cha sherehe hizo kimefanyika jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba, eneo ambako zilifanyika sherehe za kuadhimisha miaka 3 ya CCM mwaka 1980 na kuvutia maelfu ya watu.
Kuna mengi yanaweza kusemwa kuhusu maadhimisho haya ya miaka 35. Maelfu ya waliohudhuria sherehe hizo au kuzishuhudia kupitia televisheni, walighubikwa na mawazo mengi kuhusu mustakabali wa chama hicho kikongwe.

Rais na serikali wanalidharau Bunge?
SAKATA la David Jairo linaelekea kusahaulika. Hii si bahati mbaya bali ni mpango mahsusi. Kwa bahati mbaya, mkakati wa kupunguza makali ya ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoshughulikia suala hili unafanana sana mikakati mingine ya huko nyuma.
Tunaikumbuka Richmond; kamati teule ilitoa ripoti na kusababisha baraza la mawaziri kujiuzuru na kuundwa upya.

Posho: Unafiki au uzalendo?
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinaendelea kujitundika msalabani. Ni kutokana na hatua yake ya kupinga nyongeza ya posho zilizopangwa kulipwa kwa wabunge wa Bunge la Muungano.
Taarifa ya Sektarieti ya Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wiki iliyopita, inasema pamoja na mambo mengine, nyongeza mpya posho inayofikia Sh. 200,000 kutoka Sh.

Rais Kikwete chupuchupu
RAIS Jakaya Kikwete amenusurika kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, taarifa za ndani ya Bunge zimeeleza.

Bunge sasa laweza kumchunguza Rais Kikwete?
UNAHITAJIKA ujasiri kusema kuwa Bunge sasa litachunguza Ofisi ya Rais. Lakini unahitajika ujasiri zaidi kwa bunge lenyewe kufanya hivyo. Je, sivyo ilivyo?

Ulevi wa kisiasa uliyumbisha Bunge
SIKU za mwanzo za mkutano wa nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilijaa ulevi wa kisiasa kupita kiasi. Hakuna aliyesimama wima kutokana na ulevi; kila mmoja aliyumba kutetea sera za vyama kama vile ulikuwa wakati wa kampeni.

Wabunge wapimwe akili, tuanze meza kuu
MAKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliovikwa majoho ya uspika, naibu spika na uenyekiti wa Bunge wameamua kuligeuza bunge la Jamhuri kuwa jumba la sinema. Hao ni Job Ndugai (naibu spika), na wenyeviti wa Bunge, George Simbachawene, Sylvester Mabumba na Jenesta Mhagama.
Wote hawa kwa namna moja au nyingine wanaendesha Bunge kwa upendeleo.

Nguvu ya spika ni imani ya wabunge
UENDESHAJI wa bunge kwa sasa unaelekea kuwa janga la kitaifa na maafa ya kisiasa kwa ukanda wa Afrika Mashariki. Yamesemwa mengi kuhusu uwezo wa Spika Anna Makinda katika kukiendesha chombo hiki muhimu kwa ustawi wa demokrasia nchini.

Bajeti imelenga watawala au wananchi?
BAJETI ya kwanza ya serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar (SUK) chini ya uongozi wa rais Dk. Ali Mohamed Shein, inabezwa na wadau wakuu.

Serikali ya CCM bado inacheza na muswada
KATIKA mkutano uliopita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Spika Anne Makinda alitoa kauli inayohitaji ufafanuzi kuhusu hatima ya muswada wa serikali wa kuunda Tume ya Kukusanya Maoni ya marejeo ya katiba ya Tanzania.