Chenge
Mlolongo wa Habari zinazomhusu Andrew Chenge

Taifa la JK linajiendea lenyewe
Lazima tukubaliane kwamba taifa hili kwa sasa halina viongozi wa kutoa mwelekeo, lawama zote zikiendee Chama Cha Mapinduzi (CCM) Chama tawala.

Wapelelezi wa SFO waiumbua TAKUKURU
HAKUNA ubishi kuwa "ufisadi" ni neno lililochukua nafasi kubwa zaidi magazetini katika awamu hii ya uongozi wa nchi kuliko huko nyuma.
Hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, anayetetea uamuzi wa serikali wa kushindwa kufikisha watuhumiwa ufisadi mahakamani, anafahamu hili.
Katika kipindi cha miezi 28 ya uongozi kwa Rais Jakaya Kikwete, ufisadi limetamkwa na kuandikwa mara nyingi zaidi.

Ya Chenge yathibitisha CCM chama genge
NI lazima uwe na shahada ya falsafa ili ukielewe vema Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kadri siku zinavyokwenda ndivyo mambo yanavyozidi kudhihirisha kwamba chama tawala ni dude lisiloweza kueleweka.

Aliyechukua serikali ya Kikwete airudishe
KUNA kila dalili kwamba serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeelemewa. Wananchi wanauliza, "Mbona serikali yetu inakwenda kama imechukuliwa na msukule!"

Kujiuzulu hakutoshi
WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge amejiuzulu. Inajulikana kilichomsukuma hadi kuchukua hatua hiyo, ni tuhuma za kujilimbikizia utajiri kwa njia zisizofaa.

Kikwete amtosa Chenge kujinusuru
- Pinda alishinikiza 'asulubiwe!'
- Wabunge waliteta kumfukuza
SIRI ya kumtosa bilionea Andrew Chenge ni "kunusuru hadhi ya serikali inayotota" katika kipindi cha kilio cha wananchi dhidi ya ufisadi, MwanaHALISI limeelezwa.

Yaliyosemwa tayari yameanza kutokea
- Kuteuliwa na Kujiuzulu kwa Chenge
MwanaHALISI toleo la 20 – 26 Februari mwaka huu, lilichapisha makala ifuatayo juu ya wateule wa Rais Jakaya Kikwete katika baraza lake jipya la mawaziri chini ya kichwa "Wasioteulika ndio wameteuliwa." Mmoja wao alikuwa Andrew Chenge.

Kikwete unda upya Baraza la Mawaziri
KATIKA hili, Andrew Chenge, aliyejiuzulu uwaziri juzi, alisema kweli. Miezi miwili iliyopita aliwaeleza waliokuwa wanakerwa na kuteuliwa kwake tena kuwa waziri wamuulize huyo aliyemteua.

Chenge kufuru tupu, amiliki bilioni 25
- Amchotea kigogo bilioni moja
- Amwashia indiketa Ben Mkapa
WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge anaogelea katika utajiri wa zaidi ya Sh. 25 bilioni zenye utata huku Rais Jakaya Kikwete akiendelea kumkumbatia, MwanaHALISI limegundua.

Kikwete mbeba mzigo wa kiburi na chenga za Chenge
YAPO mambo mengi aliyozushiwa Andrew Chenge, Waziri wa Miundombinu ambayo mengi watu waliyaona kama mambo ya mtaani tu. Kwa mfano, niliwahi kusikia Chenge alikuwa akisafirisha suti zake kwa DHL kwenda London, Uingereza kufuliwa.