Kikwete


Mlolongo wa Habari zinazomhusu Rais Kikwete

Saed Kubenea's picture

Anne Kilango na mbio za kumpiku Rais Kikwete


Na Saed Kubenea - Imechapwa 15 February 2012

ANNA Kilango anampenda rais kuliko rais anavyojipenda. Anamtetea. Anataka kumpa kazi kila mahali.

Mwandishi wetu's picture

Kikwete chupuchupu


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 15 February 2012

MPANGO wa kuzima wabunge kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) nusura umwengue Rais Jakaya Kikwete.

Saed Kubenea's picture

Kikwete atikisa Bunge


Na Saed Kubenea - Imechapwa 08 February 2012

USHABIKI wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) sasa umewaponza.

Mwandishi wetu's picture

Mwinyi na Isambe, Kikwete na Benki ya Makaburu


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 08 February 2012

WIKI iliyopita, niliandika makala katika safu hii iliyobeba kichwa kilichosema, “Serikali haina hata busara ya kukopa?” Swali hili lilitokana na hali halisi ya mambo ilivyo nchini kwa sasa. Kubwa ni mgomo wa madaktari.

Nilifikia hitimisho hilo baada ya kutazama, kutafakari na kuzingatia kwa mapana yake mwenendo wa viongozi wakuu wa kitaifa, kuanzia kwa Rais Jakaya Kikwete, makamu wa rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kisha Waziri wa Afya, Haji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya.

Kondo Tutindaga's picture

Nani muasi, Kikwete au wabunge?


Na Kondo Tutindaga - Imechapwa 08 February 2012

CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimesherehekea miaka 35 tangu kizaliwe. Kilele cha sherehe hizo kimefanyika jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba, eneo ambako zilifanyika sherehe za kuadhimisha miaka 3 ya CCM mwaka 1980 na kuvutia maelfu ya watu.

Kuna mengi yanaweza kusemwa kuhusu maadhimisho haya ya miaka 35. Maelfu ya waliohudhuria sherehe hizo au kuzishuhudia kupitia televisheni, walighubikwa na mawazo mengi kuhusu mustakabali wa chama hicho kikongwe.

Saed Kubenea's picture

Kikwete, katiba na mafisadi


Na Saed Kubenea - Imechapwa 08 February 2012

KATIKA hotuba yake ya kuadhimisha miaka 35 ya kuzaliwa kwa chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumapili iliyopita, mjini Mwanza, Rais Jakaya Kikwete alisema mengi.

Kubwa ambalo wengi watalikumbuka, ni hatua yake ya kukana ukweli huku na kuukubali kule.

Kwa mfano, Kikwete ambaye pia ndiye mwenyekiti wa chama hicho alisema, “Sisi tunayo ajenda yetu. Tunazo ahadi zetu; na yote ambayo tunatekeleza yametokana na yale tuliyoahidi.” Aliwataka wenzake wasikubali kuhama kwenye mstari.

Saed Kubenea's picture

Kikwete asaliti wabunge CCM


Na Saed Kubenea - Imechapwa 01 February 2012

MSIMAMO wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu marekebisho ya sheria ya katiba sasa uko njiapanda, imefahamika jijini Dar es Salaam.

Kondo Tutindaga's picture

JK ukipuuza katiba, utajipuuza


Na Kondo Tutindaga - Imechapwa 01 February 2012

BAADA ya Rais Jakaya Kikwete kukutana na vyama vya upinzani ikulu jijini Dar es Salaam ili kushauriana nao juu ya mchakato wa katiba mpya, kuna mambo mawili makubwa yamejitokeza yanayoweza kumpotosha rais na kumwingiza katika mgogoro.

Kwanza, wapo washauri wake pamoja na Wanikulu kadhaa wanaoeneza fitina kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilijifanya kumsusa rais, lakini sasa kimenywea na kuanza kumbembeleza ili awasamehe na kujadiliana nao.

Jacob Daffi's picture

CHADEMA yamtega tena JK


Na Jacob Daffi - Imechapwa 25 January 2012

RAIS Jakaya Kikwete aweza kukitosa tena Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuhusu uundwaji wa katiba mpya, MwanaHALISI limeelezwa.

Jabir Idrissa's picture

‘JK anavunja Katiba’


Na Jabir Idrissa - Imechapwa 11 January 2012

DK. Willibrod Slaa amemtuhumu Rais Jakaya Kikwete kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoapa kuilinda.

Saed Kubenea's picture

Kikwete aingia tope jipya


Na Saed Kubenea - Imechapwa 04 January 2012

SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete yaweza kufikishwa mahakamani kwa mara nyingine. Mara hii kwa kushindwa kutoa malipo yanayohusiana na uzalishaji nishati ya umeme.

Alfred Lucas's picture

Ahadi za Rais Kikwete hazijatekelezwa


Na Alfred Lucas - Imechapwa 04 January 2012

NI vema wananchi wamemaliza mwaka 2011 na kuanza mwaka mpya wa 2012. Hata hivyo, ukweli utabaki palepale; wengi wao hawatasahau kauli tata na ahadi mithili ya Abunuwasi zilizotolewa na Rais wa Jamhuri, Jakaya Kikwete.

Nyaronyo Kicheere's picture

Kikwete kamlisha kasa Jaji Damian Lubuva


Na Nyaronyo Kicheere - Imechapwa 04 January 2012

HIVI karibuni, Rais Jakaya Kikwete, alimteua Jaji mstaafu Damian Lubuva kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kondo Tutindaga's picture

Rais na serikali wanalidharau Bunge?


Na Kondo Tutindaga - Imechapwa 28 December 2011

SAKATA la David Jairo linaelekea kusahaulika. Hii si bahati mbaya bali ni mpango mahsusi. Kwa bahati mbaya, mkakati wa kupunguza makali ya ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoshughulikia suala hili unafanana sana mikakati mingine ya huko nyuma.

Tunaikumbuka Richmond; kamati teule ilitoa ripoti na kusababisha baraza la mawaziri kujiuzuru na kuundwa upya.

Saed Kubenea's picture

Rais Kikwete atibua nyongo


Na Saed Kubenea - Imechapwa 21 December 2011

NISHANI ZA UHURU

RAIS Jakaya Kikwete ametunuku nishani 57 kwa alioita, “Watu waliotoa mchango mbalimbali ya kutukuka katika nchi kwenye miaka 50 ya uhuru wake. Nishati hizo ni ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwenge wa Uhuru daraja la kwanza na Mwenge wa uhuru daraja la pili.

Saed Kubenea's picture

Kikwete akaliwa kooni


Na Saed Kubenea - Imechapwa 14 December 2011

Naye atakiwa kujiuzulu
Waraka mzito wavuja
CHADEMA yaitwa ‘mchawi’

RAIS Jakaya Kikwete amekaliwa kooni. Wakati chama chake kinakabiliwa na wimbi la kukimbiwa na wanachama na viongozi, swahiba wake anashikilia kuwa wenye “tuhuma za ufisadi” wajiuzulu kama yeye.

Jacob Daffi's picture

Kikwete atavua magamba mangapi?


Na Jacob Daffi - Imechapwa 07 December 2011

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), sasa kinatafuta mlango wa kutokea baada ya kushindwa kutekeleza kwa vitendo mradi wake wa kujivua gamba.

Ukweli wa kama kimeshindwa kujivua gamba uko wazi, kinachokosekana sasa ni ujasiri wa kukiri hadharani kuwa kimeshindwa.

Tangu kushindwa kutekeleza mradi huo, kumekuwa na kauli tofauti zinazotafuta kupunguza makali ya aibu ya kushindwa kutoka kwa viongozi wakuu wa chama hicho.

Kwa mfano, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita, Wilson Mukama, katibu mkuu wa chama hicho, amenukuliwa akisema, “Sharti

Kondo Tutindaga's picture

CCM na urais wa makanisani


Na Kondo Tutindaga - Imechapwa 07 December 2011

BAADA ya vikao vya Chama cha Mapinduzi vilivyomalizika mjini Dodoma wiki mbili zilizopita, taarifa ilitolewa na wasemaji wa chama hicho kuwa mojawapo ya matatizo yanayokikabili chama hicho ni minyukano inayotokana na mbio za kuusaka urais wa mwaka 2015.

Mapema mwaka huu, baadhi ya wanaohisiwa kuwa tayari wameanza harakati za kuusaka urais, waliitwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho, Tanzania Bara, Pius Msekwa na kuonywa kuwa wasiendelee na harakati hizo.

Aidha, taarifa ya kamati ya wazee watatu walioteuliwa na chama kutafuta suluhu ya minyukano ndani ya chama – rais msta

Joster Mwangulumbi's picture

JK kweli rais wa CCM


Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 07 December 2011

NIMEWAHI kuandika katika safu hii kauli nzito ya kwanza aliyotoa Barack Obama baada ya kushinda urais nchini Marekani.

Alisema, “Mimi ni rais wa Wamarekani.

Saed Kubenea's picture

Kikwete, Lowassa hapatoshi


Na Saed Kubenea - Imechapwa 30 November 2011

HATIMAYE Edward Lowassa ametoka hadharani na kuonyesha kuwa anataka kupimana ubavu na Rais Jakaya Kikwete.

Fred Okoth's picture

CHADEMA yatikisa Ikulu


Na Fred Okoth - Imechapwa 30 November 2011

RAIS Jakaya Kikwete hakufahamu kwa undani kilichomo kwenye muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba (Constitutional Review Bill 2011), uliopitishwa na bunge hivi karibuni, MwanaHALISI limeelezwa.

Joster Mwangulumbi's picture

CCM watamtosa Kikwete


Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 30 November 2011

KABLA ya kufikia uamuzi wa jambo fulani la kitaalam, wasomi hubungua bongo taaluma iwaongoze. Hakuna kupiga kura.

Kura hutumika katika masuala ya kisiasa. Mtindo huu wa kura huwa hauzingatii uzito wa hoja ila wingi wa kura kurahisisha mambo.

Upande unaopata kura chache huhesabika umeshindwa hata kama una hoja zenye maslahi.

Kondo Tutindaga's picture

Kikwete mtuhumiwa, tufanye nini?


Na Kondo Tutindaga - Imechapwa 30 November 2011

UKURASA mpya kuhusu sakata la Richmond, umefunguliwa baada ya mambo mawili kutokea katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), vilivyomalizika mjini Dodoma Alhamisi iliyopita.

Nyaronyo Kicheere's picture

Namhurumia rais wangu Kikwete


Na Nyaronyo Kicheere - Imechapwa 30 November 2011

WIKI iliyopita ilikuwa mbaya sana kwa rais wangu, Jakaya Mrisho Kikwete, kwa namna alivyoumbuliwa mkutanoni na rafiki yake, Luteni wa Jeshi Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa, ambaye tumeambiwa mara nyingi kuwa hawakukutana barabarani.

Katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Dodoma , Lowassa alipewa dakika saba tu kusema jambo naye akazitumia vilivyo, kwa kifupi na kwa ufasaha.

Nimeambiwa na wale waliokuwapo Dodoma , ndugu zangu wa Mwananchi, kama walivyoripoti katika gazeti lao, kwamba Lowassa alisema:

“Mwenyekit

Saed Kubenea's picture

Ikulu aibu tupu


Na Saed Kubenea - Imechapwa 23 November 2011

VIGOGO kadhaa waandamizi serikalini na katika bunge wamenufaika na mamilioni ya shilingi yaliyokusanywa kinyume cha taratibu na David Jairo, katibu mkuu wizara ya nishati na madini, MwanaHALISI limeelezwa.

Mwandishi wetu's picture

Gamba lamponza Kikwete


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 23 November 2011

MRADI wa kujivua gamba umeanza kumyumbisha Rais Jakaya Kikwete. Baadhi ya marafiki zake tayari wamegawanyika; wengine wameanza kukata tamaa na wengine wanajisalimisha kwa wanaotuhumiwa ufisadi, MwanaHALISI linaweza kuripoti.

Alfred Lucas's picture

Dk. Slaa, Kikwete uso kwa uso


Na Alfred Lucas - Imechapwa 23 November 2011

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinakusudia kumshitaki Rais Jakaya Kikwete kwa umma, iwapo atagoma kukutana nao, imeleezwa.

Saed Kubenea's picture

Mzigo wa makundi wamuelemea Kikwete


Na Saed Kubenea - Imechapwa 09 November 2011

KILE kinachoitwa, “Utafutaji tiba ya makundi” yanayohasimiana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), bado hakijapatikana.

Mikutano miwili iliyofanyika jijini Dar es Salaam na ule wa jijini Arusha, badala ya kumaliza mpasuko uliokuwapo, imeishia kupambanua makundi hayo.

Kwenye mkutano wa Dar es Salaam, uliofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee,  31 Oktoba 2011, makundi mawili hasimu – lile linalodaiwa kubeba watuhumiwa  wa ufisadi na lile linalojiita “wapambanaji ufisadi” – yalitumia vikao hivyo kujiimarisha na kuonyesha wapambe wao kwamba bado wako imara

Fred Okoth's picture

Kikwete na Museveni wanaelewa ujumbe wa wasomi?


Na Fred Okoth - Imechapwa 02 November 2011

SIKU ya Kongamano la kuadhimisha miaka 50 ya Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tarehe 20 Oktoba 2011, ilikuwa siku ya msukosuko kwa watu wawili maarufu – Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Jakaya Kikwete.

Saed Kubenea's picture

Kikwete maji ya shingo


Na Saed Kubenea - Imechapwa 19 October 2011

RAIS Jakaya Kikwete amebakiwa na njia mbili tu kulinda nafasi yake katika Chama cha Mapinduzi (CCM).