Kikwete


Mlolongo wa Habari zinazomhusu Rais Kikwete

Haji AmeirAmeir's picture

Ni kweli Kikwete ameshindwa


Na Haji AmeirAmeir - Imechapwa 11 August 2009

MAKALA ya Salva Rweyemamu, aliyepinga kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kazi, ndiyo imenivuta katika mjadala huu.

David Kafulila's picture

Mafanikio ya Kikwete hayajaonekana


Na David Kafulila - Imechapwa 04 August 2009

NAJADILI makala ya Salva Rweyemamu iliyochapishwa katika MwanaHALISI toleo la 16-21 Julai mwaka huu na kupewa kichwa cha "Lipumba: Nani kashindwa kazi?"

Saed Kubenea's picture

Kikwete ang'ang'ania 'zigo' la Richmond


Na Saed Kubenea - Imechapwa 28 July 2009

RAIS Jakaya Kikwete amejitwisha upya "zigo" ambalo tayari lilishafika ufukweni. Jumamosi iliyopita, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima alitangaza uamuzi wa serikali wa "kuwabeba" viongozi wawili waandamizi waliokuwa wanatuhumiwa katika sakata la kampuni ya Richmond Development Company (LLC).

Mohamed Yusuph's picture

Nani mkweli, Salva na Lipumba?


Na Mohamed Yusuph - Imechapwa 21 July 2009

MAKALA ya Salva Rweyemamu iliyochapishwa ukurasa wa sita wa gazeti hili, toleo lililopita, imeibua hisia kwa wasomaji wengi.

Mbasha Asenga's picture

Kikwete timua wateule wabovu


Na Mbasha Asenga - Imechapwa 14 July 2009

KARIBU mwezi sasa, kumeenea habari za kutisha kuhusu uchafuzi wa mazingira katika Wilaya ya Tarime unaosababishwa na kuvuja kwa sumu kutoka mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya kuchimba dhahabu ya Barrick.

Salva Rweyemamu's picture

Profesa Lipumba: Nani kashindwa kazi?


Na Salva Rweyemamu - Imechapwa 14 July 2009

WIKI iliyopita, Mwenyekiti wa muda mrefu wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alikaririwa na gazeti la MwanaHALISI akisema kuwa Rais Jakaya Kikwete "ameshindwa kazi."

Navaya ole Ndaskoi's picture

Tamko la Kikwete bado sumu kwa wafugaji


Na Navaya ole Ndaskoi - Imechapwa 07 July 2009

WAFUGAJI wa asili nchini wamo hatarini kutoweka. Wana matatizo mengi kiasi cha kuhofia kupata yale maisha bora yaliyoahidiwa kwa kila Mtanzania.

Jonathan Liech's picture

Rais Kikwete ametuangusha


Na Jonathan Liech - Imechapwa 16 June 2009

NISEME mapema mimi ni miongoni mwa Watanzania waliokwishakata tamaa kuhusu ufanisi wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete.

editor's picture

Kikwete anashangaa nini?


Na editor - Imechapwa 09 June 2009

HATIMAYE Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete ametema nyongo. Amesema hadharani kuwa amesikitishwa na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi (WAZAZI) ya chama chake kugawanyika na kufikia hatua ya kupigana ngumi.

Saed Kubenea's picture

Kikwete ametelekeza wapambanaji


Na Saed Kubenea - Imechapwa 02 June 2009

KAMANDA Jakaya Kikwete amesalimu amri? Vita dhidi ya ufisadi imemwelemea? Mbona hatekelezi ahadi zake za kupambana na ufisadi? Turejee kauli zake.

Saed Kubenea's picture

Kikwete aanza kutema wanamtandao?


Na Saed Kubenea - Imechapwa 12 May 2009

RAIS Jakaya Kikwete ametupa wanamtandao wake waliomuingiza madarakani miaka minne iliyopita? Hilo ndilo swali ambalo bila shaka wafuatiliaji wa mkondo wa siasa nchini wanajiuliza hivi sasa.

Saed Kubenea's picture

Mabilioni yakusanywa kumwangusha Kikwete


Na Saed Kubenea - Imechapwa 14 April 2009

RAIS Jakaya Kikwete atahitaji kutumia nguvu mara tatu kukabiliana na “genge” linalotaka kumzuia kugombea urais kwa kipindi cha pili, MwanaHALISI limeelezwa. Taarifa zilizopatika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki zilisema, wanaotaka kumzuia Kikwete kugombea urais kwa kipindi cha pili, wamepanga kutumia, na tayari wamekusanya Sh. 2.5 bilioni kwa shughuli hiyo.

M. M. Mwanakijiji's picture

Wanaompigia Kikwete kampeni, wanaogopa nini?


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 14 April 2009

KUNA kundi la watu woga ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kundi la wasiojiamini na wasioamini kuwa Rais Jakaya Kikwete anaweza kuchagulika tena 2010.

M. M. Mwanakijiji's picture

Kikwete ametuacha njia panda


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 07 April 2009

HOTUBA ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa 1 Aprili 2009, haiwezi kupita bila kujadiliwa. Sababu zipo nyingi. Lakini kubwa ni kwamba hotuba ya rais ni kichocheo cha mijadala.

Saed Kubenea's picture

Malecela amesimama na Kikwete?


Na Saed Kubenea - Imechapwa 31 March 2009

MBUNGE wa Mtera, mkoani Dodoma, makamu mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu (CC), John Samwel Malecela ameibuka na kusema chama chake “hakitishiwi na kundi la viongozi wa chama hicho wanaotaka kujimega.”  

Mwandishi wetu's picture

Mafisadi wamtishia Kikwete


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 25 March 2009

WATUHUMIWA wa ufisadi, wanaolalamika kuwa Rais Jakaya Kikwete amewatelekeza, wanapanga kumhusisha katika baadhi ya tuhuma zinazowakabili ili kumshinikiza kutimiza matakwa yao, MwanaHALISI limeelezwa.

Mwandishi wetu's picture

Kikwete kupangua MaDC


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 18 February 2009

RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa katika uteuzi wa wakuu wa wilaya wakati wowote kutoka sasa, imefahamika.

Saed Kubenea's picture

Kikwete atafukuza Mnali wangapi?


Na Saed Kubenea - Imechapwa 18 February 2009

IJUMAA iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alitangaza kumfuta kazi mkuu wa wilaya ya Bukoba, Albert Mnali kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Jabir Idrissa's picture

Kikwete akiri kushindwa Zanzibar


Na Jabir Idrissa - Imechapwa 11 February 2009

KAMA si kujipunja alama za kuitwa muungwana ni nini? Rais Jakaya Kikwete kusema Wapemba wanaweza kuchagua wabunge na wawakilishi watakao, bali wakabidhi serikali kwa CCM, ni kujipunja alama.

editor's picture

Rais unakotupeleka siko


Na editor - Imechapwa 04 February 2009

WAKATI Rais Jakaya Kikwete anajua kwamba Zanzibar kuna mgogoro, hata kama anaupaka rangi na kuuita “mpasuko;” na mgogoro umeleta maafa kisiasa, kiuchumi na kijamii, kauli zake akiwa ziarani Pemba zimepanua ufa.

Saed Kubenea's picture

Kikwete atishia wenzake


Na Saed Kubenea - Imechapwa 28 January 2009

Wapanga kuhama chama
Aliyotabiri Mkapa yaja

BAADHI ya viongozi na wanachama mashuhuri ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wana mpango wa kuanzisha chama cha siasa ili kuweka upinzani mkali kwa Rais Jakaya Kikwete ifikapo 2010, MwanaHALISI limeelezwa.

Saed Kubenea's picture

Miaka 3 ya JK: Tumevuna nini?


Na Saed Kubenea - Imechapwa 14 January 2009

SIKU 24 zilizopita Rais Jakaya Kikwete alitimiza miaka mitatu ya madarakani. Aliapishwa 21 Desemba 2005.

Saed Kubenea's picture

Njama kumng'oa Kikwete zafichuka


Na Saed Kubenea - Imechapwa 07 October 2008

Mwanae Ridhiwani ashiriki njama
Watuhumiwa ufisadi wajipanga

KUNDI la watuhumiwa wa ufisadi limejipanga kumng’oa Rais Jakaya Kikwete ili asigombee urais mwaka 2010, MwanaHALISI limegundua.

Saed Kubenea's picture

Membe amwokoa Kikwete


Na Saed Kubenea - Imechapwa 16 September 2008

NEC ilikaribia kupasuka
Ni katika sakata la Nape

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe ndiye alimwezesha Rais Jakaya Kikwete kubaini njama za kupasua Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Mwandishi wetu's picture

Wizi wa mabilioni BoT: Kikwete alidanganya


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 09 September 2008

RAIS Jakaya Kikwete hakuwa na haja ya kuunda Timu ya Kuchunguza Wizi wa fedha za EPA kwa kuwa anajua kilichotendeka, MwanaHALISI limegundua.

Mafaili ya Benki Kuu yamejaa mawasiliano juu ya udanganyifu mkubwa, hasa uliofanywa na kampuni ya Kagoda Agriculture ambayo pia yatakuwa mikononi mwa Timu yake.

Mwandishi wetu's picture

Ikulu ya umma au mafisadi?


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 02 September 2008

EPA na Richmond ni mchezo mmoja wenye waigizaji walewale. Hata Rais Jakaya Kikwete anajua hivyo.

editor's picture

Pasipo uhuru pana utumwa


Na editor - Imechapwa 26 August 2008

RAIS Jakaya Kikwete ameonyesha kuwa muda si mrefu hasira yake itavishukia vyombo vya habari. Akihutubia Bunge, Alhamisi, 21 Agosti 2008, rais alionya juu ya kile alichoita kutumia vibaya uhuru wa kutoa maoni.

Mbasha Asenga's picture

Rais apakwa mafuta kwa mgongo wa chupa


Na Mbasha Asenga - Imechapwa 26 August 2008

KILE kimbunga tulichozoea kukiona zama za mfumo wa chama kimoja kinarejea kwa kasi. Kimeanza na kinaendelea kujikusanya.

Mwandishi wetu's picture

Kikwete na Ngulla: Nani anajua zaidi sheria za kazi?


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 26 August 2008

NANI anajua zaidi? Rais Jakaya Kikwete au Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Nestory Ngulla?

Jabir Idrissa's picture

Lipumba amvaa Mkapa


Na Jabir Idrissa - Imechapwa 12 August 2008

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema hakina imani na juhudi za Rais Jakaya Kikwete za kupambana na rushwa kwa kuwa uongozi wake ulipatikana kwenye misingi ya rushwa.