Kikwete


Mlolongo wa Habari zinazomhusu Rais Kikwete

Saed Kubenea's picture

Ikulu yapuuzia afya ya Kikwete


Na Saed Kubenea - Imechapwa 23 December 2009

Mwenyewe akata anga na mbuga
Atenda kinyume cha daktari wake

AFYA ya Rais Jakaja Kikwete imo hatarini kufuatia kupuuza masharti ya daktari wake ya kupunguziwa kazi na kupumzika, MwanaHALISI limeelezwa.

Jonathan Liech's picture

Kikwete bado anayo nafasi


Na Jonathan Liech - Imechapwa 23 December 2009

MARAIS au wafalme, kote duniani, hukumbukwa kwa matendo yao wakiwa madarakani miaka mingi baada ya kuwa wamemaliza vipindi vyao vya uongozi au hata wakiwa wamefariki dunia.

M. M. Mwanakijiji's picture

Sababu za kukwamisha Kikwete


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 23 December 2009

Ameendekeza safari za nje, ombaomba

WIKI iliyopita tulichapisha kwenye ukurasa huu sababu 10 kati ya 51 za kuzuia Rais Jakaya Kikwete kugombea urais tena mwaka kesho. Zifuatazo ni sababu nyingine 10.

Maggid Mjengwa's picture

Mwinyi atamsaidia Kikwete kuiponya CCM?


Na Maggid Mjengwa - Imechapwa 23 December 2009

KUNA matukio mawili yenye kuashiria jinsi Rais Jakaya Kikwete anavyoishiwa uvumilivu kutokana na malumbano ya kimakundi ndani ya chama chake- Chama Cha Mapinduzi (CCM).

M. M. Mwanakijiji's picture

Kikwete amekwishafanya uamuzi mgumu


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 09 December 2009

TUNAPOELEKEA uchaguzi mkuu ujao tukiwa "ndani ya kumi na mbili" hatuna budi kuangalia uongozi kwa mwanga mpya. Tukiendelea kuangalia uongozi kwa mwanga wa zamani basi tutajikuta tunarudia makosa yale yale tuliyoyafanya huko nyuma.

Saed Kubenea's picture

Kikwete ampiga 'stop' Rostam


Na Saed Kubenea - Imechapwa 02 December 2009

Ahofia kuibua EPA nyingine
Ataka kutafutwa fedha halali

Taarifa kutoka ndani ya CCM zinasema hivi sasa unaandaliwa utaratibu mpya wa kutafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka kesho.

Jonathan Liech's picture

Rais na bembea, wananchi na ukame


Na Jonathan Liech - Imechapwa 02 December 2009

MIONGONI mwa nukuu maarufu zaidi kuhusu umuhimu wa picha ni ile inayosema picha moja nzuri ina uwezo wa habari nzuri yenye urefu wa maneno 1000.

Saed Kubenea's picture

Ahadi ya Rais Kikwete kwa vijana ina walakini


Na Saed Kubenea - Imechapwa 25 November 2009

RAIS Jakaya Kikwete amerudia ndweo. Ni marejeo ya nafasi ya vijana katika uongozi na utawala nchini. Anasema katika kipindi chake cha pili cha uongozi, ataweka vijana wengi katika serikali yake.

Mbasha Asenga's picture

Kikwete ameamua kufa na mizigo yake


Na Mbasha Asenga - Imechapwa 18 November 2009

KAMA kuna kitu kimekuwa kinamsumbua Rais Jakaya Kikwete kwa muda mrefu ni uwezo mdogo wa baadhi ya mawaziri wake. Ninaamini kwa kauli zake amekuwa akijilaumu kwa nini amewapa madaraka makubwa watu hao ambao kwa kweli wameshindwa kuleta mabadiliko yoyote katika nchi.

Saed Kubenea's picture

Nyumba ya Kikwete inaungua


Na Saed Kubenea - Imechapwa 11 November 2009

KAMATI ya rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi iliyoundwa kutafuta "kiini cha uhasama" miongoni mwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), imezidisha nyongo.

Navaya ole Ndaskoi's picture

Hoja ya Rais kushindwa kazi


Na Navaya ole Ndaskoi - Imechapwa 11 November 2009

Serikali Kilosa ilivyopora wafugaji

NINACHANGIA mjadala ulioibuliwa na Profesa Ibrahim Lipumba, aliyesema Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kazi; ukweli unaowakera wapambe wa Kikwete.

Nkwazi Mhango's picture

Nani ataokoa Kikwete?


Na Nkwazi Mhango - Imechapwa 04 November 2009

UKIANGALIA jinsi mambo yanavyokwenda, utaona kama vile Rais Jakaya Kikwete hajali kutumbikiza serikali yake katika kashfa.

Saed Kubenea's picture

Mgawanyiko ndani ya CCM: Rais Kikwete anakimbia kivuli chake


Na Saed Kubenea - Imechapwa 01 November 2009

UKWELI ni upi? Baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanakiri kuna mgawanyiko ndani ya chama chao.

Mulokozi Eligius's picture

Rais bora hapimwi kwa mambo madogo


Na Mulokozi Eligius - Imechapwa 01 November 2009

NIMEVUTIWA na mjadala ulioanzishwa na Salva Rweyemamu katika gazeti hili, kwamba ni Rais Jakaya Kikwete pekee aliyefanikiwa kuleta maendeleo, ikilinganishwa na marais waliomtangulia, ukiondoa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Nkwazi Mhango's picture

Kikwete ameshindwa, ameangusha umma


Na Nkwazi Mhango - Imechapwa 01 November 2009

NIMEVUTIWA na mjadala unaoendelea juu ya utendaji kazi wa Rais Jakaya Kikwete. Niseme kuwa Tanzania haijawahi kupata rais mwenye kutatanisha na aliyekatisha tamaa kama huyu wa sasa.

Mwandishi wetu's picture

Udhaifu wa mawaziri wa Kikwete hadharani


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 01 November 2009

KUZOROTA kwa utendaji wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete kunatokana, pamoja na mambo mengine, baadhi ya watendaji wake kuhujumiana, imefahamika.

Saed Kubenea's picture

Afya ya Kikwete yazua mjadala


Na Saed Kubenea - Imechapwa 06 October 2009

AFYA ya Rais Jakaya Kikwete sasa imekuwa mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi wa rika tofauti. Kufuatia rais kuishiwa nguvu, kushindwa kusimama na kukatisha hotuba mjini Mwanza mwishoni mwa wiki, wananchi waliohojiwa na gazeti hili wamesema, kwa njia mbalimbali, kuwa afya ya rais inastahili kuchunguzwa kwa makini.

Mwandishi wetu's picture

JK angalia boriti jichoni mwako ndipo...


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 06 October 2009

NDANI ya mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Jakaya Kikwete analia mbele ya Jumuiya ya Kimataifa akitaka iunge mkono msimamo wa Umoja wa Afrika (AU) wa kupinga utawala uliojiweka madarakani kwa kuiba kura na uliopindua serikali halali.

Dady Igogo's picture

Kikwete hajafanikiwa, anaanguka


Na Dady Igogo - Imechapwa 29 September 2009

NIMESUKUMWA na hoja aliyoitoa Salva Rweyemamu kwamba ni Rais Kikwete pekee aliyefanikiwa kuleta maendeleo, akilinganishwa na marais wote waliotangulia isipokuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Markus Honorius's picture

Ya Rais Kikwete kama ya Hugo Chavez


Na Markus Honorius - Imechapwa 29 September 2009

TAREHE 23 Mei 1999, Rais wa Venezuela, Hugo Chavez alianzisha kipindi cha kujibu maswali, kutoka kwa wananchi, kwa njia ya televisheni.

Aristariko Konga's picture

Marekani inafanya dhihaka?


Na Aristariko Konga - Imechapwa 22 September 2009

KEJELI, utani au ndio njia ya "wakubwa kuwasiliana?"

Siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kutetea safari zake nje ya nchi, ubalozi wa Marekani nchini ulitoa taarifa inayoelezea vigezo vya nchi kupata msaada. Havihusu safari za wakuu wa nchi.

John Kibasso's picture

Kikwete asaidie iwepo sera dhidi ya ufisadi


Na John Kibasso - Imechapwa 22 September 2009

RAIS Kikwete Jumatano 09 Septemba, 2009, aliamsha hisia za wananchi kwa kutoa staili mpya ya kuwaruhusu kumweka kiti moto 'live' kwenye luninga na vituo vya redio hapa nchini.

Saed Kubenea's picture

Kagoda yamwakia Kikwete


Na Saed Kubenea - Imechapwa 15 September 2009

Wahisani washinikiza ukaguzi
Misaada ya wafadhili yakatwa

SERIKALI imesalimu amri. Imerudisha nchini maodita wa Deloitte & Touche kutoka Afrika Kusini kufanya tena ukaguzi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), MwanaHALISI limegundua.

Saed Kubenea's picture

Rais ameshindwa 'kumaliza kiu'


Na Saed Kubenea - Imechapwa 15 September 2009

MUDA wa saa mbili uliotengwa kwa Rais Jakaya Kikwete kujibu maswali ya wananchi kupitia vyombo vya habari haukutosha.

Emmanuel Shilatu's picture

Rais Kikwete amefanya mengi


Na Emmanuel Shilatu - Imechapwa 08 September 2009

NAUNGANA na Salva Rweyemamu, John Kibaso na Dunia Ibrahimu, kupinga kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kazi.

Dunia Ibrahim's picture

Kikwete ni zaidi ya Mkapa na Mwinyi


Na Dunia Ibrahim - Imechapwa 01 September 2009

MAKALA sita zilizochapishwa mfululizo katika MwanaHALISI wiki tano zilizopita, ndizo zilizonisukuma kupata ujasiri wa kumtetea Rais Jakaya Kikwete, dhidi ya hoja za wapinzani wake wa kisiasa.

Julius Mruta Ngenya's picture

Utetezi wa Kikwete hauna mashiko


Na Julius Mruta Ngenya - Imechapwa 25 August 2009

MAKALA ya Salva Rweyemamu na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) John Kibaso, waliopinga kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kazi, ndiyo imenivuta katika mjadala huu.

John Kibasso's picture

Rais Kikwete apata mtetezi


Na John Kibasso - Imechapwa 18 August 2009

NIMELAZIMIKA kuandika makala hii baada ya kubaini upotoshaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya wasomaji wa MwanaHALISI wakichangia makala ya Salva Rweyemamu aliyempinga mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Professa Ibrahim Lipumba ambaye alisema "Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kazi."

Mwandishi Maalum's picture

Kikwete amtelekeza Sitta


Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 18 August 2009

Aruhusu 'mafisadi' kumsulubu
Mpasuko mkubwa CCM waja

RAIS Jakaya Kikwete ameshindwa kulinda hadhi ya Spika wa Bunge la Jamhuri, Samwel Sitta katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma.

Nicoline John's picture

Kikwete kushindwa ahadi zake


Na Nicoline John - Imechapwa 11 August 2009

MWAKA kesho ni mwaka wa uchaguzi. Tayari Rais Jakaya Kikwete amenukuliwa akijitapa kwamba yeye na chama chake watatimiza kile walichoahidi kabla na baada ya kuingia madarakani. Anasema atafanya hivyo, kabla ya uchaguzi mkuu mwingine kufanyika.