Lowassa


Mlolongo wa Habari zinazomhusu Edward Lowassa

Saed Kubenea's picture

Lowassa, Rostam waumbuana


Na Saed Kubenea - Imechapwa 05 May 2009

SIRI imefichuka. Vigogo waliojaribu kuiba ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu kashfa ya Richmond kabla ya kuwasilishwa bungeni, waliiba “kanyaboya,” MwanaHALISI limegundua.

Saed Kubenea's picture

Vita vya makundi CCM vyamwandama Kikwete


Na Saed Kubenea - Imechapwa 07 April 2009

Mwakyembe amkomalia Chiligati
Mkuchika kuvaana na Makamba

VITA vya makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake, sasa siyo siri tena. Sasa vinaelekezwa moja kwa moja kwa Rais Jakaya Kikwete, MwanaHALISI limeelezwa.

Saed Kubenea's picture

Lowassa amzunguka Kikwete


Na Saed Kubenea - Imechapwa 31 March 2009

Ni katika uteuzi wa Ma-DC
Orodha yabadilishwa mwishoni

UTEUZI wa wakuu wapya wa wilaya,  uhamisho wa baadhi na kustaafishwa kwa wengine, vinadaiwa kuingiliwa na mtandao wa aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa, MwanaHALISI limeelezwa.

M. M. Mwanakijiji's picture

Mgawanyiko CCM: Kikwete njiapanda


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 25 March 2009

WABUNGE wenye msimamo kama wa mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, na wale wenye msimamo kama wa Rostam Aziz, mbunge wa Igunga, hawawezi kubakia ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wakati mmoja. Sharti wale wa msimamo mmoja watoke ili chama kinusurike.

Owawa Stephen's picture

Dowans ina harufu ya Lowassa


Na Owawa Stephen - Imechapwa 11 March 2009

TAREHE 7 Februari 2008 aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa alilazimika kuachia ngazi nafasi hiyo kutokana na kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond Development Company (LLC).

Charles Nkwabi's picture

Majanga 6 ya mwaka 200


Na Charles Nkwabi - Imechapwa 14 January 2009

KWENYE sherehe za sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kumeibuka tathimini mpya inayoonyesha waziwazi kuwa Tanzania sasa siyo tena “kisiwa cha amani.”

Saed Kubenea's picture

Membe amwokoa Kikwete


Na Saed Kubenea - Imechapwa 16 September 2008

NEC ilikaribia kupasuka
Ni katika sakata la Nape

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe ndiye alimwezesha Rais Jakaya Kikwete kubaini njama za kupasua Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Saed Kubenea's picture

Lowassa kiboko


Na Saed Kubenea - Imechapwa 02 September 2008

Asaini mkataba pekee yake
Makamba: Tutaita Kamati Kuu

MKATABA wa kitegauchumi cha ujenzi wa jengo la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM) umechukua sura mpya baada ya wajumbe wa Baraza la Wadhamini mmoja baada ya mwingine, kumkana mwenyekiti wao, Edward Lowassa.

Saed Kubenea's picture

Masikini Lowassa


Na Saed Kubenea - Imechapwa 19 August 2008

Mjumbe wa Baraza la Wadhamini amkana
Dk. Nagu naye adaiwa kutoshiriki mkataba

MGOGORO kuhusu mkataba wenye utata wa Umoja wa Vijana wa CCM umeingia katika sura mpya baada ya baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wadhamini kuukana, MwanaHALISI limeelezwa.

Saed Kubenea's picture

Kikwete amliza Lowassa


Na Saed Kubenea - Imechapwa 12 August 2008

Asema mkataba hauna maslahi
Aelekea kuunga mkono Nape

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete amesema mkataba wa mradi wa ujenzi wa kitegauchumi cha Umoja wa Vijana (UV-CCM), una dosari nyingi na haukubaliki kama ulivyo, MwanaHALISI limeelezwa.

Saed Kubenea's picture

Lowassa aumbuka


Na Saed Kubenea - Imechapwa 29 July 2008

Mkataba wake watinga kwa Kikwete
Ni ule wa mradi tata wa UV-CCM

KUNA ushahidi wa kutosha kwamba Baraza la Wadhamini la Umoja wa Vijana (UV-CCM) chini ya Edward Lowassa limeingiza umoja huo katika mkataba wa utata na bila kufuata utaratibu.

Saed Kubenea's picture

Mradi wa UV-CCM, kashifa tupu


Na Saed Kubenea - Imechapwa 22 July 2008

Makamba amdanganya Kikwete
Nchimbi, Isaack wakumbwa na aibu

YUSUPH Makamba, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni mwongo, MwanaHALISI limegundua. Wiki iliyopita Makamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkataba kati ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na mwekezaji ulikuwa haujatiwa saini.

Saed Kubenea's picture

Msumari wa mwisho katika 'jeneza' la Lowassa abakia na 'galasa'


Na Saed Kubenea - Imechapwa 22 July 2008

Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba sasa wanaelekea ukingoni kisiasa.

Saed Kubenea's picture

Rais Kikwete atapeliwa


Na Saed Kubenea - Imechapwa 15 July 2008

Ni katika mradi wa mabilioni
Edward Lowassa ahusishwa

BARAZA la Wadhamini la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), limemtapeli Rais Jakaya Kikwete katika mradi wa mabilioni ya shilingi, MwanaHALISI limeelezwa.

Saed Kubenea's picture

Bomu la Mwakyembe lalipuka


Na Saed Kubenea - Imechapwa 08 July 2008

Ni katika Sakata la Richmond
Mke wa waziri alipigia magoti Kamati

MKE wa mmoja wa mawaziri watatu waliojiuzulu kutokana na sakata la Richmond, alipigia magoti baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge akiomba wamlinde mume wake, imefahamika.

Mwandishi Maalum's picture

Mtandao safisha Lowassa: Waliotajwa waanza kuukana


Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 24 June 2008

MBUNGE wa Peramiho, Jenista Mhagama amekana kuwa katika "Mtandao Safisha Lowassa (MSALO)" ambao umeripotiwa kuundwa na baadhi ya viongozi katika serika na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Saed Kubenea's picture

Watuhumiwa wa ufisadi hawasafishiki


Na Saed Kubenea - Imechapwa 24 June 2008

WALE wanaoitwa watuhumiwa wa ufisadi hawajasafishwa. Vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) vilivyofanyika mkoani Dodoma wiki mbili zilizopita, kamwe haviwezi kuwasafisha.

Stanislaus Kirobo's picture

Wapelelezi wa SFO waiumbua TAKUKURU


Na Stanislaus Kirobo - Imechapwa 13 May 2008

HAKUNA ubishi kuwa "ufisadi" ni neno lililochukua nafasi kubwa zaidi magazetini katika awamu hii ya uongozi wa nchi kuliko huko nyuma.

Hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, anayetetea uamuzi wa serikali wa kushindwa kufikisha watuhumiwa ufisadi mahakamani, anafahamu hili.

Katika kipindi cha miezi 28 ya uongozi kwa Rais Jakaya Kikwete, ufisadi limetamkwa na kuandikwa mara nyingi zaidi.

Mwandishi wetu's picture

Genge laundwa kumkabili Kikwete


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 06 May 2008

Lahofia mabadiliko serikalini
Yeye ajiandaa kuwakabili

GENGE la watuhumiwa wa ufisadi nchini linajiandaa kukabiliana na utawala wa Rais Jakaya Kikwete ili kuudhoofisha kabisa, MwanaHALISI limeelezwa.

David Kafulila's picture

Mafisadi wasionewe huruma


Na David Kafulila - Imechapwa 06 May 2008

MAFUNZO ya kivita dhidi ya ufisadi yanazidi kupata waumini. Kilichobaki sasa ni kujenga mahali pa kuhitimishia vita hivyo kwa kuwa baadhi ya mafisadi wanaendelea kuwepo na wanatamba.

Saed Kubenea's picture

Urais ngoma nzito kwa Kikwete


Na Saed Kubenea - Imechapwa 29 April 2008

Wabia wake wamekuwa na nguvu kuliko yeye
Ameendelea kuwabeba mawaziri wenye tuhuma

SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete imechukuliwa na msukule. Wananchi wanajiuliza: "Mbona urais kwa Kikwete umekuwa mgumu kinyume cha matarajio yao?"

Mwandishi wetu's picture

Siri ya Msabaha dhidi ya Lowassa


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 08 April 2008

SIRI nzito moyoni mwa aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha, ndiyo ililazimisha Edward Lowassa kujiuzulu Uwaziri Mkuu kutokana na kashfa ya Richmond, MwanaHALISI limegundua.

Edgar Lengai's picture

Sakata la Richmond: Lowassa kikombe hakiepukiki


Na Edgar Lengai - Imechapwa 26 March 2008

NINAJADILI hapa baada ya kugundua jitihada zinazofanywa na baadhi ya vyombo vya habari kutaka kumsafisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kuhusu uovu wa mkataba wa Richmond, baada ya mweyewe kushindwa kujitetea bungeni.

Saed Kubenea's picture

Sitta amsubiri Lowassa


Na Saed Kubenea - Imechapwa 19 March 2008

SPIKA wa Bunge, Samwel Sitta, anamsubiri aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Edward Lowassa, ili kumjumuisha katika moja ya kamati za kudumu za Bunge, MwanaHALISI limeambiwa.

Malaila Junior's picture

Lowassa hajakomaa kisiasa


Na Malaila Junior - Imechapwa 12 March 2008

MTAALAMU yeyote wa masuala ya siasa, achambue kadri awezavyo, hawezi kukwepa ukweli kwamba siasa ni msingi wa maendeleo kwa watu na taifa lao.