Makamba


Mlolongo wa Habari zinazomhusu Yusuf Makamba

Mwandishi wetu's picture

Makamba, Londa roho juu


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 21 April 2009

UAMUZI juu ya shauri lililofunguliwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yusuph Makamba na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Salum Londa dhidi ya mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee (Chadema), unatarajiwa kutolewa katika mkutano wa Bunge ulioanza hapa jana, imefahamika.

Mwandishi wetu's picture

Makamba atuhumiwa kuchochea migogoro CCM


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 04 March 2009

Kazi ya Kamati ya Bunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushughulikia malalamiko na matamshi ya mbunge wa Mvomelo, mkoani Morogoro, Suleman Sadiq, sasa imekuwa ndogo.

Mwandishi wetu's picture

Makamba, Londa "waingia mitini"


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 04 February 2009

Wakimbia kesi yao dhidi ya mbunge

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yusuph Makamba na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, Salum Londa, wameingia mitini katika kesi yao dhidi ya mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Halima Mdee.

Mwandishi wetu's picture

Ya Mdee, Londa na Makamba


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 21 January 2009

KESI ya aina yake inarindima. Inahusu makada wawili mashuhuri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Katibu Mkuu, Yusuph Makamba na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Salum Londa.

Saed Kubenea's picture

Njama kumng'oa Kikwete zafichuka


Na Saed Kubenea - Imechapwa 07 October 2008

Mwanae Ridhiwani ashiriki njama
Watuhumiwa ufisadi wajipanga

KUNDI la watuhumiwa wa ufisadi limejipanga kumng’oa Rais Jakaya Kikwete ili asigombee urais mwaka 2010, MwanaHALISI limegundua.

Mwandishi wetu's picture

CCM sasa yatota Tarime


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 07 October 2008

Makamba atuma Makongoro kwa JK
Atakiwa kumkabili Enock Chambiri

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimezidi kupasuka wakati huu kinapoelekea katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani wilayani Tarime mkoani Mara.

Ndimara Tegambwage's picture

Tarime: Jumapili njema!


Na Ndimara Tegambwage - Imechapwa 07 October 2008

JUMAPILI ijayo, wananchi wakazi wa jimbo la uchaguzi la Tarime, mkoani Mara, wanaandika historia. Ni kunyakua au kunyang’anywa ushindi. Basi.

Mwandishi Maalum's picture

Makamba, Nchimbi waumbuka


Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 16 September 2008

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuph Makamba wameumbuka.

Mwandishi wetu's picture

Ufisadi mpya waibuka CCM


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 16 September 2008

Wamhusu Kapteni Komba
Makamba adaiwa kumlinda

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yusuph Makamba amezama katika tope jipya baada ya kutuhumiwa kumlinda Kapteni John Komba anayedaiwa kutafuna mamilioni ya shilingi.

Mwandishi wetu's picture

Makamba hatihati


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 16 September 2008

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba amevutwa shati na mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

Saed Kubenea's picture

Nape: Kondoo wa kafara


Na Saed Kubenea - Imechapwa 09 September 2008

HALMASHAURI Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inakutana mjini Dodoma. Huu ni mkutano wa pili wa kawaida tangu chama kilipomaliza kikao cha NEC kilichofanyika kijijini Mwitongo, Butiama mkoani Mara, Aprili mwaka huu.

Saed Kubenea's picture

Lowassa kiboko


Na Saed Kubenea - Imechapwa 02 September 2008

Asaini mkataba pekee yake
Makamba: Tutaita Kamati Kuu

MKATABA wa kitegauchumi cha ujenzi wa jengo la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM) umechukua sura mpya baada ya wajumbe wa Baraza la Wadhamini mmoja baada ya mwingine, kumkana mwenyekiti wao, Edward Lowassa.

Saed Kubenea's picture

Mradi wa UV-CCM, kashifa tupu


Na Saed Kubenea - Imechapwa 22 July 2008

Makamba amdanganya Kikwete
Nchimbi, Isaack wakumbwa na aibu

YUSUPH Makamba, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni mwongo, MwanaHALISI limegundua. Wiki iliyopita Makamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkataba kati ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na mwekezaji ulikuwa haujatiwa saini.

Saed Kubenea's picture

Msumari wa mwisho katika 'jeneza' la Lowassa abakia na 'galasa'


Na Saed Kubenea - Imechapwa 22 July 2008

Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba sasa wanaelekea ukingoni kisiasa.