Mramba


Mlolongo wa habari kumhusu Basil Mramba

M. M. Mwanakijiji's picture

Chenge, Mramba, Karamagi na Rostam wasirudi bungeni


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 19 May 2010

KWANZA, ni lazima ifahamike kwamba tunapotaka kujenga demokrasia katika taifa, msingi mmoja mkuu ni viongozi kufahamu kuwa uongozi ni utumishi.

Katika msingi huo tulirudia mara kwa mara mawazo kuwa “cheo ni dhamana.” Mawazo haya yote yalitaka kutuonesha kwamba anayetaka kuwa kiongozi wa umma ni lazima atambue kuwa anataka kuwa mtumishi wa umma.

Katika utumishi huu wa umma jambo kubwa zaidi ni imani ya wananchi kwa viongozi wao. Endapo wananchi wanaanza kupoteza imani na viongozi wao, basi viongozi hao wanakuwa hawana mahali tena pa kusimamia.

Ezekiel Kamwaga's picture

Mramba aingiza Meghji matatani


Na Ezekiel Kamwaga - Imechapwa 20 January 2010

UKAIDI wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Basil Mramba, ndio ulisababisha kuteketea kwa Sh. 10 bilioni zilizotolewa na serikali kufufua kiwanda cha General Tyre East Africa (GTEA).

Alloyce Komba's picture

Kesi za ufisadi ziendeshwe kwa Kiswahili


Na Alloyce Komba - Imechapwa 14 January 2009

KUNA msemo katika masuala ya utoaji haki mahakamani uendao hivi: “Haki siyo tu itendeke, bali pia ionekane imetendeka.” Huu ni msemo maarufu katika mwenendo mzima wa usilizaji kesi au shauri.