Nchimbi
Mlolongo wa Habari zinazomhusu Emmanuel Nchimbi

Songea Mjini wamkalia kooni Nchimbi
JIMBO la Songea Mjini ni miongoni mwa majimbo sita ya uchaguzi yaliyopo katika Mkoa wa Ruvuma. Emmanuel John Nchimbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndiye mbunge wake.

Nchimbi aingizwa kikaangoni Songea
DURU za kisiasa mkoani Ruvuma zinaonyesha kwamba kuna wanasiasa ambao tayari wameanza harakati za maandalizi za kuwania Jimbo la Songea Mjini. Wamo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Oliver Mhaiki, wabunge wa Viti Maalum, Devotha Likokola na Injinia Stela Manyanya .

Digrii za Nchimbi, Kamala 'zaota mbawa'
- Sasa waamua kurejea darasani
- "Maprofesa" kibao nao wavuliwa wasifu
MAWAZIRI wawili wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, miongoni mwa sita waliotajwa kujipa wasifu wa elimu wasiyokuwa nayo, wameanza kutekeleza mkakati wa kujisafisha.

Makamba, Nchimbi waumbuka
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuph Makamba wameumbuka.

Nape: Kondoo wa kafara
HALMASHAURI Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inakutana mjini Dodoma. Huu ni mkutano wa pili wa kawaida tangu chama kilipomaliza kikao cha NEC kilichofanyika kijijini Mwitongo, Butiama mkoani Mara, Aprili mwaka huu.

Lowassa aumbuka
- Mkataba wake watinga kwa Kikwete
- Ni ule wa mradi tata wa UV-CCM
KUNA ushahidi wa kutosha kwamba Baraza la Wadhamini la Umoja wa Vijana (UV-CCM) chini ya Edward Lowassa limeingiza umoja huo katika mkataba wa utata na bila kufuata utaratibu.

Mradi wa UV-CCM, kashifa tupu
- Makamba amdanganya Kikwete
- Nchimbi, Isaack wakumbwa na aibu
YUSUPH Makamba, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni mwongo, MwanaHALISI limegundua. Wiki iliyopita Makamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkataba kati ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na mwekezaji ulikuwa haujatiwa saini.

Nape awania uenyekiti UV-CCM
MWANASIASA kijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amechukua fomu ya kugombea uenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UV-CCM).

Uchaguzi UV-CCM waingia dosari
UCHAGUZI mkuu ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM) umeanza kuingia dosari kutokana na kubainika kuwa baadhi ya wagombea wametoa taarifa za uwongo kuhusu umri wao wakitarajia 'kutetewa na viongozi ngazi ya taifa.'

Dk. Nchimbi: Tulia tu!
KAMA kuna kiongozi mwenye bahati kubwa ni Dk. Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.