Nyerere


Mlolongo wa Habari zinazomhusu Mwalimu Julius Nyerere

Alfred Lucas's picture

Tutafikia siku kuambiwa Mwalimu Nyerere aliishi Kigamboni


Na Alfred Lucas - Imechapwa 07 December 2011

KABLA ya kuanza safari yake ya kwenda kupandishwa kwenye kilele cha Uhuru cha Mlima Kilimanjaro, Mwenge wa Uhuru ulipitishwa kwa mbwembwe nyingi mkoani Dar es Salaam kama sehemu ya kuenzi kumbukumbu ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.

Mwenge ulipitia wilaya zote tatu – Ilala, Kinondoni na Temeke. Ukiwa Kinondoni, ulipitishwa mtaa wa Ifunda, Magomeni, ambako Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliishi wakati wa harakati za kudai uhuru.

Katika nyumba hiyo ambayo sasa ni sehemu ya ofisi ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mwalimu aliishi kwa miezi mitano tu ndipo akaenda Ikulu.

Anthony Kayanda's picture

Miaka 12 bila Nyerere, taifa limengamia


Na Anthony Kayanda - Imechapwa 23 November 2011

MIAKA 12 bila Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kimefundisha mengi. Kwanza, wado wananchi wanakumbuka Zanzibar ilipojiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) mwaka 1994. Ulitokea mvutano mkubwa bungeni, lakini Nyerere aliweza kuumaliza.

Akashinikiza Zanzibar ijiondoe OIC. Hakuishia hapo.

Mbasha Asenga's picture

Aibu; tunamuenzi Nyerere kwa staili ya nyani


Na Mbasha Asenga - Imechapwa 19 October 2011

WENGI tunamjua nyani. Ni mnyama mwerevu. Kuna simulizi kwa ajili ya watoto inayosema hapo kale waliazimia kujenga nyumba. Walifikia hatua hiyo baada ya kuonja jeuri ya mvua usiku.

M. M. Mwanakijiji's picture

Wangeanza hawa taifa lingekuwaje?


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 22 June 2011

MASHAMBULIZI dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere yameendelea kwa nguvu katika mitandao ya intaneti. Binafsi, siamini kuwa wanaochafua Nyerere wametumwa na watawala.

M. M. Mwanakijiji's picture

Nyerere atakumbukwa, wengine watapuuzwa!


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 15 June 2011

NDANI ya mitandao ya mawasiliano mbalimbali kumeibuka wimbi la watu wanaomshabulia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na yale aliyotuachia.

Joster Mwangulumbi's picture

Urithi wa Nyerere ni Muungano tu?


Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 04 May 2011

KINGUNGE Ngombale-Mwiru, mmoja wa makada wakuu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametoa wito.

Mwandishi Maalum's picture

Aliyosema Nyerere yaanza kutokea


Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 10 November 2010

WAKATI wa uhai wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, tulisikia mengi ambayo sasa tunayakumbuka.

Nkwazi Mhango's picture

Miaka 11 bila Nyerere: Ni fitina, unafiki mtupu


Na Nkwazi Mhango - Imechapwa 13 October 2010

KESHO ni Oktoba 14, siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa taifa, Julius Nyerere kilichotokea Uingereza mwaka 1999.

Nkwazi Mhango's picture

Tujifunze kutoka kwa Maria Nyerere


Na Nkwazi Mhango - Imechapwa 21 April 2010

NAKUMBUKA. Nilianzisha mjadalala juu ya utata kuhusu shughuli na maisha ya wake wa marais – First Ladies – katika nchi za Afrika.

Mwandishi wetu's picture

Butiku akana madai ya Sabodo


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 20 January 2010

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku amesema hataki malumbano na mfanyabiashara Mustafa Jaffer Sabodo wa Dar es Salaam.

Mwandishi wetu's picture

Nyerere alivyomwona Kawawa


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 13 January 2010

RASHID Mfaume Kawawa ni kiongozi wa nchi changa, ndogo. Lakini ni kiongozi adhimu sana. Ana moyo wa ajabu. Katika wadhifa wa kitaifa amekuwa ni mtu wa pili au hata wa tatu. Lakini katika utendaji wake amekuwa wakati wote na mahali popote ni mtu wa kwanza.

Mbasha Asenga's picture

Kawawa kamfuata Nyerere, ole wake CCM


Na Mbasha Asenga - Imechapwa 06 January 2010

WATANZANIA walifunga mwaka 2009 kwa msiba mkubwa wa mwanasiasa mkongwe, Rashid Kawawa. Ni vigumu kuzungumzia harakati za uhuru wa Tanganyika, kuundwa kwa serikali ya wazalendo na harakati zote za kujitawala tangu uhuru mwaka 1961 hadi sasa bila kutaja mchango wake.

editor's picture

Wanaoshutumu MNF wamelegea


Na editor - Imechapwa 30 December 2009

MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema, ameibuka na mbiu mpya. Anawashutumu vikali wale wote waliotoa kauli zao kwenye kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF).

Aristariko Konga's picture

Mwalimu pokea ujumbe huu


Na Aristariko Konga - Imechapwa 23 December 2009

NIMEAMUA kukuletea ujumbe huu Mwalimu. Ninafanya hivyo huku nchi yetu ikiwa na ukame na njaa kwenye baadhi ya maeneo na sehemu nyingine zikiwa zimeathirika na mafuriko kwa kiasi fulani. Wananchi wa Same ni mashahidi wa janga hili.

M. M. Mwanakijiji's picture

Nyerere kaondoka na CCM yake


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 11 November 2009

MIAKA 10 baada ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuaga dunia, imedhihirika kuwa ameondoka na chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwandishi Maalum's picture

Samahani Mwalimu Nyerere, nilikuenzi kivyanguvyangu


Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 04 November 2009

NAITWA Mchumiatumbo mwana wa Tapeli. Ingawa, kwa makusudi, nimechelewa kuwasiliana nawe ili kukupa nafasi ya kutafakari mengi uliyoambiwa, acha nikuandikie. Kwa sasa una muda wa kutosha kuyatafakari yangu niandikaye nikiwa kwenye kiza kinene.

Saed Kubenea's picture

Wanaotaka kumuua Nyerere hawatafanikiwa


Na Saed Kubenea - Imechapwa 01 November 2009

Fikra zake zingali na thamani kwa taifa
Nafsi yake bado imebeba tunu adimu

MWALIMU Julius Kambarage Nyerere, bado yu hai. Hili nililisema 14 Oktoba 1999, mara baada ya Rais Benjamin Mkapa kutangazia ulimwengu kuwa Mwalimu Nyerere amefariki dunia.

Aristariko Konga's picture

Mwalimu Nyerere na miaka 13 ya pensheni


Na Aristariko Konga - Imechapwa 01 November 2009

ULIKUWA ni mwaka wa 13 tangu Mwalimu Julius kambarage Nyerere aache madaraka ya urais. Nilipata fursa ya kuwa mmoja wa watu waliokuwa wamemtembelea Aprili 1998 kijijini Butiama wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuifutia madeni Tanzania.

Aristariko Konga's picture

Kifimbo cha Nyerere na imani za kale


Na Aristariko Konga - Imechapwa 01 November 2009

KWA miaka mingi watu wamekuwa wakitoa maelezo kadha wa kadhaa kuhusu kifimbo ambacho Mwalimu Julius Nyerere alibeba kila alipokwenda.

Alfred Lucas's picture

Nani anamuenzi Mwalimu Nyerere?


Na Alfred Lucas - Imechapwa 01 November 2009

LEO ni miaka 10 tangu mwasisi wa taifa hili, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere afariki dunia. Alifariki 14 Oktoba 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas, nchini Uingereza.

editor's picture

Tuishi kama Nyerere


Na editor - Imechapwa 01 November 2009

WATANZANIA tunamkumbuka sana Mwalimu Julius Nyerere. Alijenga taifa lenye mshikamano. Hata makabila yake mengi yametumika kuibua utani miongoni mwa wananchi na siyo mifarakano.