CCM
Mlolongo wa Habari za Chama cha Mapinduzi

CCM Mwanza sherehe, Dodoma uasi
PICHA mbili kinzani zilionekana mwisho ni mwa wiki iliyopita kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Moja nzuri saaaana na nyingine inatisha.
Jijini Mwanza kulikokuwa na kila aina ya shamrashamra za CCM kutimiza miaka 35 tangu kizaliwe, ilionekana katika picha ya kusisimua, kuhamasisha, kukonga nyoyo na kuvutia hata wasio wanachama.
Uwanja wa CCM Kirumba ulitawaliwa na rangi ya kijani na njano. Wapo waliocheza, walioshangilia kwa nguvu, waliopiga vigelegele na mbinja wakafurahia umri wa miaka 35.

CHADEMA yamtega tena JK
RAIS Jakaya Kikwete aweza kukitosa tena Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuhusu uundwaji wa katiba mpya, MwanaHALISI limeelezwa.

Uchaguzi wa CCM, si mwarobaini wa ufisadi
MWAKA 2012 umewadia. Ni mwaka wa uchaguzi wa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kuna mengi yanasemwa kuhusu uchaguzi huu na kuwajengea matumaini bandia wengi wa wanachama wake.
Hata kama kwa kawaida uchaguzi huleta sura mpya na mambo mapya katika taasisi, ni ndoto kutumaini kuwa uchaguzi wa ndani wa chama hiki unaweza kufanya hivyo. Sababu ni nyingi, lakini mbili ni kubwa.

Amjuae msafi na mwadilifu CCM na serikalini amtaje
WATANZANIA walishangaa Desemba 8 mwaka jana Rais Jakaya Kikwete alipowatunuku nishani ya utumishi uliotukuka viongozi kadhaa na wastaafu walio hai na waliokwishakufa ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.
Mshangao huo ulitokana na ukweli kwamba viongozi waliostahili kutunukiwa kwa macho na akili za wananchi hawakuguswa. Waliotajwa kustahili ni pamoja na Spika Mstaafu Samwel Sitta na Waziri Mkuu Mstaafu Samwel Malecela.

CCM ina shahada ya kuzomea
BILIONEA Henry Ross Perot alitikisa Marekani alipojitokeza kuwania kiti cha urais akiwa mgombea binafsi mwaka 1992 na 1996.
Perot mwenye utajiri unaomfanya ashike nafasi ya 99 nchini Marekani, alisisimua kwa kauli, ushauri na siasa huru.
Kuhusu uchumi alisema, “Udhaifu wa shilingi ni ishara ya uchumi dhaifu, na uchumi dhaifu unadhoofisha taifa.”
Aliongeza, “Bajeti lazima iwe kamilifu, hazina ijazwe ‘minoti’, deni la taifa lipunguzwe na maringo ya maafisa wa serikali yadhibitiwe.” Je, kuna la kujifunza?
Juni mwaka huu, baada ya

Mteketa: Tatizo CCM tunaoneana haya
“SIKUWAZA kama ningekuwa mbunge. Kutokana na unafiki, majungu, wivu na fitina zilizojikita kwenye ulingo wa kisiasa, binafsi sikufikiria kwamba ninaweza kujitumbukiza katika ulingo huu wa kisiasa. Ni kwa sababu, kwenye siasa kila mtu anapanga mkakati wa kumharibia mwenzake.
“Lakini ni fitina hizo zilizoninufaisha baada ya baadhi ya watu kunishawishi kuingia kwenye kinyang’anyiro cha ubunge mwaka 2010 na hatimaye nikafanikiwa kushinda.”
Ndivyo anavyoeleza Abdul Rajab Mteketa, mbunge wa Kilombero kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Serikali ya CCM yajivunia silaha
KAMA kuna kitu kimewachefua Watanzania wengi ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kuhodhi shughuli na sherehe zote za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

Waziri kumkimbia Lowassa CCM
WAZIRI mmoja mwandamizi ndani ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete, yuko mbioni kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM), imefahamika.

CCM wamekosea ‘kumshika matiti’ binti yao
KUMKOSEA adabu mtoto wako wa kike, tena mtoto mwenyewe mkubwa aliyekwishavunja ungo, ni kosa kubwa lisilosameheka katika mila za makabila mengi duniani yawe ya Kiafrika, Ulaya, Uchina, Uhindini na hata Marekani.
Kwa sababu hiyo nawaasa wazazi wenzangu, chondechonde, msithubutu hata siku moja, hata kwa bahati mbaya kuwashika matiti mabinti zenu yasije yakawakuta yale yanayomkuta leo mzazi aitwaye Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kwani mnafikiri mambo yanayoisumbua CCM na serikali yake yanatokana na nini?

Kikwete maji ya shingo
RAIS Jakaya Kikwete amebakiwa na njia mbili tu kulinda nafasi yake katika Chama cha Mapinduzi (CCM).

Igunga kwafukuta
- BAKWATA aibu tupu
- Uchaguzi Jumapili hii
- DC ageuka ‘bubu’
FATUMA Kimario, mkuu wa wilaya (DC) wa Igunga, siyo muislam, MwanaHALISI limeelezwa.

Udini isiwe silaha ya uhalifu
KAMPENI za uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Igunga, mkoani Tabora, zinazokaribia kufika ukingoni Jumamosi wiki hii, zimewaibua hata wasiyotarajiwa.

Ni hatari kuilinda CCM kwa silaha ya udini
KAMPENI za uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Igunga, mkoani Tabora, zinazokaribia kufika ukingoni Jumamosi wiki hii, zimewaibua hata wasiyotarajiwa. Walianza Baraza Kuu la Waislamu nchini (BAKWATA), lililozusha mtafaruku kwa tamko lao la kuwataka waislamu wa Igunga waskipigie kura Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kile walichodai, “ni adui wa uislamu na waislamu.”

Ukiua ufisadi utakuwa umeua CCM
ILIPOTANGAZWA kuwapo kwa mradi wa kujivua gamba ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baadhi yetu tulitabiri mapema kwamba hizo ni ghiliba na pengine ni sehemu ya sherehe za kuadhimisha miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM.

Serikali ina ndoa na wakristo?
MAKALA iliyosema “Kikwete amepasua jipu la udini” katika safu ya “Tuseme Kweli” wiki iliyopita imeibua hisia kali. Wasomaji saba kati ya 123 waliotuma meseji zao hawakunipongeza.
Mmoja ameniita mzushi, mwingine amedai inachochea fujo, mwingine amedai nimeathiriwa na mfumo kristo huku meseji tatu zinatuhumu.
Msomaji mwenye simu Na 0767446064 amedai: Ninyi Mwanahalisi ni CHADEMA na makala yako ni mfumo kristo.

CCM wanamhadaa nani?
KATIKA mdahalo wa hivi karibuni uliowakutanisha wawakilishi wa vyama vitatu – CCM, CHADEMA na CUF – mshiriki kutoka CCM alitonesha vidonda aliposema kwamba ana imani itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea inaweza kuwavusha Watanzania kwa miaka 50 mingine

Nani atasimamia nidhamu ndani ya CCM?
BINTI yangu anayesoma darasa la sita, wiki iliyopita, alinishangaa nilipokuwa nazungumza na mtu aliyevaa shati la kijani. Akahoji kwa nini nilikubali urafiki na fisadi!

Hakuna aliyebora ndani ya CCM
SASA Rais Jakaya Kikwete ametingwa. Marafiki zake ndani ya CCM ambao ama amekuwa akishirikiana nao au akitaniana nao hata kushikana ndevu wanakabiliwa na kashfa mbalimbali.

Uhuru wetu umeliwa na CCM
BABA wa Taifa katika siku zake za mwisho kama rais mstaafu aliwahi kukemea tabia ya Ikulu kugeuzwa danguro la wafanyabiashara waovu. Leo hii, ikulu imegeuzwa ndanguro na baadhi ya wafanyabiashara na watendaji wa serikali waliokumbatia rushwa, jambo ambalo limeifanya nchi kuwa na uongozi tofauti na ule uliochaguliwa na wananchi.

Mwigulu: Mtunza ‘mabilioni’ CCM
LAMECK Nchemba Mwigulu (33), ni mmoja wa vijana wanaotarajiwa kuwa hazina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika miaka ijayo. Ni mbunge wa CCM katika jimbo la Iramba Magharibi.

Kamati Kuu ina busara kuliko wabunge wa CCM
MWALIMU Julius Nyerere aliwashangaa wananchi, baadhi yao wanachama wa CCM waliosema 1+1=3. Hesabu hiyo ilihusu muundo wa muungano.

Wenye vituo vya mafuta ni wafadhili CCM, hawaguswi
MWISHONI mwa wiki iliyopita, nilipata bahati ya kukaa kijiweni kunywa kahawa jirani na nyumbani kwangu Tungi, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

CCM imechoka, serikali legelege
JUNI 8 mwaka huu, serikali iliwasilisha bungeni bajeti yake iliyokuwa inaainisha makadirio ya makusanyo ya mapato na matumizi kwa mwaka 2011/ 2012.

Sababu tosha kutenganisha urais na uenyekiti wa chama
“Kamati Kuu inasikitishwa na tatizo la umeme nchini kwani athari zake kwa uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja ni kubwa. Hivyo basi imeitaka serikali kutumia muda iliyopewa wa kurekebisha bajeti ya wizara ya nishati na madini kuja na mpango wa dharura wa kunusuru hali hii na kisha kulimaliza kabisa tatizo la umeme nchini.”
Nimeanza mjadala wangu kwa kunukuu moja ya maamuzi yaliyofikiwa na Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokaa mjini Dodoma 31 Julai 2011ili kuonyesha haja ya kufanyika kwa mageuzi makubwa ya kimuundo nchini.

Kumbe Bunge ni la mashemeji!
Mbunge wa kike kutoka upinzani aliposimama kutoa mchango wake, wabunge wa CCM walimzomea kwa kumwita “shemeji”, “shemeji” ili aone aibu akae.
Nilijiuliza wabunge wa CCM wamefikia kiwango cha chini hivyo? Masikio ya Naibu Spika, Job Ndugai, kama wenyeviti wenzake, hayakusikia utoto, kejeli na mzaha ule ila aliona uvunjaji kanuni wa wapinzani.
Uvunjifu wa kanuni ndiyo kinga iliyobaki kwa wabunge wa CCM. Nje ya kanuni ni aibu tupu.

CCM wanawachukia mafisadi, si ufisadi
MIKUTANO ya Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) vinatarajiwa kufanyika wakati wowote wiki hii mjini Dodoma. Kubwa linaloonekana ni mgawanyiko wa mtizamo katika kushughulikia matatizo yanayokikabili chama hicho.

Wagonga meza, wazomeaji CCM kutunga katiba mpya
MKAKATI mahsusi wa kuwezesha kupitishwa kwa muswada wa marekebisho ya katiba kupitia Bunge hili la sasa lililojaa wazomeaji na wagonga meza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeandaliwa.

Hatuna sababu ya kumpongeza Rostam
SIKUBALIANI na wanaopongeza uamuzi wa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, kwa kujiuzulu. Nawakatalia zaidi wale wanaodai amefanya hivyo kwa maslahi ya taifa.

Posho na umasikini wa ‘kutaga mayai’
KAULI ya waziri mkuu Mizengo Pinda, kwamba serikali “itaangalia upya suala zima la posho,” inaelekea kuzima joto la hoja muhimu.

Serikali yasubiri kuanguka
ALICHOKIFANYA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe bungeni mnamo wiki iliyopita, juu ya tuhuma za rada zinazomkabili Andrew Chenge ni udhalilishaji dhidi ya serikali na wananchi.