CCM


Mlolongo wa Habari za Chama cha Mapinduzi

Saed Kubenea's picture

CCM yasaka ngwe mpya bila lolote la kujivunia


Na Saed Kubenea - Imechapwa 23 June 2010

MILANGO ya kinyang’anyiro cha urais wa Jamhuri ya Muungano na ule wa Zanzibar, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefunguliwa katikati ya mazingira magumu ya maisha ya wananchi wengi.

Mwandishi wetu's picture

Synovate wametumwa na nani?


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 23 June 2010

WAKATI mwingine ni vigumu kuamini namna nchi yetu inavyoruhusu mambo yaende kienyeji bila ya kuangalia maslahi ya taifa baadaye.

Jabir Idrissa's picture

Mbio za urais CCM na hatima ya Z’bar


Na Jabir Idrissa - Imechapwa 23 June 2010

KATIKA kipindi ambacho macho na masikio ya wawakilishi wa kibalozi wa nchi za magharibi wanasema waziwazi wangependa kuona Wazanzibari wanaridhia mabadiliko ya mfumo wa kiutawala Zanzibar, inashangaza viongozi wenyewe wa Zanzibar wanajikongoja katika suala hili.

Mbasha Asenga's picture

Bajeti 2010/11: Serikali ni jeuri au kiziwi


Na Mbasha Asenga - Imechapwa 16 June 2010

NI vigumu kuamini kwamba Serikali ya Awamu ya Nne kwa miaka mitatu sasa, ama imekataa au imebeza maombi muhimu ya wafanyakazi ya kuboresha maisha yao.

Jabir Idrissa's picture

Mpinga umoja unaojengwa Z’bar ndiye shetani


Na Jabir Idrissa - Imechapwa 16 June 2010

MAKADA wa Kisonge wanasema: TANU na ASP ndio walioleta umoja wa kitaifa. Hatudanganyiki; hapana hapana.

Joster Mwangulumbi's picture

Anne Kilango: Wanataka kuniua


Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 09 June 2010

VITA vya kuwania ubunge Jimbo la Same Mashariki vimechukua sura mpya baada ya mbunge wa jimbo hilo, Anne Kilango-Malecela kudai mpinzani wake anataka kumaliza maisha yake na uzao wake.

Saed Kubenea's picture

Bajeti ya serikali hii hapa


Na Saed Kubenea - Imechapwa 09 June 2010

KODI! Kodi! Kodi, ndio mwelekeo wa Bajeti ya Taifa inayotarajiwa kutangazwa kesho.

Benson Msemwa's picture

Uozo utaangamiza taifa


Na Benson Msemwa - Imechapwa 09 June 2010

NINASOMA magezeti, kusikiliza redio na kutazama televisheni. Nakuta malalamiko mengi ya wananchi. Kwa wingi huo, unaweza kukubali haraka kuwa nchini mwetu kuna uozo.

Saed Kubenea's picture

Sitta kung’olewa uspika


Na Saed Kubenea - Imechapwa 02 June 2010

KUNA njama za kuwatoa “kafara” wabunge 15 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili kusafisha njia ya urais wa Edward Lowassa, MwanaHALISI limeelezwa.

M. M. Mwanakijiji's picture

Lowassa agombee, asigombee?


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 02 June 2010

MMOJA wa watu ambao naamini wanatakiwa kufikiria sana kama wanastahili kugombea katika uchaguzi mkuu ujao, si mwingine bali ni Waziri mkuu wa zamani na mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.

Mwandishi wetu's picture

Serikali yajifilisi


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 26 May 2010

SERIKALI imeumbuka. Inahaha kukopa fedha benki kujazia bajeti, wakati inatuhumiwa kutumia mabilioni ya shilingi bila maelezo mwafaka.

editor's picture

Serikali ndio mchawi


Na editor - Imechapwa 26 May 2010

SERIKALI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaimba nyimbo isiyowafaa Watanzania. Inapolaumu kunyimwa fungu katika bajeti inajidanganya. Inatakiwa kutambua sababu za uamuzi wa wahisani kuinyima fungu hilo.

M. M. Mwanakijiji's picture

Masha, Chikawe na Msolla wasirudi tena


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 26 May 2010

HAKIKA, kuna wengi waliopewa nafasi na Rais Jakaya Kikwete ya kuongoza wizara na idara za serikali. Hata hivyo, wengi wa waliopewa nafasi wameshindwa kufanya kazi kama ilivyotakiwa.

Mwandishi wetu's picture

Masauni: Mbegu ya viongozi iliyooza


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 26 May 2010

HATIMAYE yametokea. Hamad Masauni Yussuf ameng’olewa uongozi ndani ya Umoja wa Vijana (UV-CCM). Hivyo ndivyo tuliripoti miezi miwili iliyopita.

Mbasha Asenga's picture

Nani kairoga serikali ya Kikwete?


Na Mbasha Asenga - Imechapwa 26 May 2010

SERIKALI ya Awamu ya Nne, inaumwa ugonjwa wa “kupenda sifa.” Hata pale inapokuwa kwenye matatizo, bado viongozi wake hawataki kukiri. Wanaendelea kung’ang’ana kuwa “mambo ni mazuri.”

Mwandishi wetu's picture

Madudu mengine ya Kikwete haya hapa


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 19 May 2010

RAIS Jakaya Kikwete yuko hatarini kubebeshwa kashfa mbili kubwa, MwanaHALISI limegundua.

Kashfa ya kwanza inahusu chaguo lake la Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UV-CCM), Hamad Masauni Yussuf anayetuhumiwa kughushi vyeti vya kuzaliwa.

Padre Baptiste Mapunda's picture

Viongozi wa dini msile njama na CCM


Na Padre Baptiste ... - Imechapwa 19 May 2010

KONGAMANO la siku mbili lililokutanisha viongozi wa dini na serikali jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, haliwezi kupita bila kujadiliwa.

Mbasha Asenga's picture

Kikwete mpindishaji wa maana ya takrima


Na Mbasha Asenga - Imechapwa 19 May 2010

HAKUNA ubishi kuwa mfumo wa siasa unaotumika nchini ni chimbuko kubwa la rushwa. Ndio njia kuu inayoasisi ufisadi. Kuna kila ushahidi kwamba ufisadi mkubwa na mbaya uliopata kufanywa katika taifa hili kwa miaka ya karibuni umeanzia kwenye uchaguzi.

M. M. Mwanakijiji's picture

Hawa wanastahili kurudi bungeni?


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 12 May 2010

MATATIZO mengi yanayoonekana kwenye baadhi ya majimbo yetu ya uchaguzi yanahusiana moja kwa moja na watu wanaotuwakilisha.

Ezekiel Kamwaga's picture

Kawawa na wenzake walipotea hapa…


Na Ezekiel Kamwaga - Imechapwa 12 May 2010

WENGI wetu tuliozaliwa mwishoni mwa miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980, tulipokuwa tukikua, tulielewa kwamba CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi.

editor's picture

Dawa ni kuwapa haki wafanyakazi


Na editor - Imechapwa 05 May 2010

RAIS Jakaya Kikwete juzi alizungumza na wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walioko mkoa wa Dar es Salaam kuhusu mambo mawili.

Ezekiel Kamwaga's picture

Mbunge Chitalilo matatani


Na Ezekiel Kamwaga - Imechapwa 28 April 2010

MBUNGE wa Buchosa – Samwel Mchele Chitalilo – yuko matatani na uwezekano wake kugombea tena ubunge Oktoba mwaka huu, uko mashakani.

Mwandishi wetu's picture

Makundi ya wabunge yajirudia


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 28 April 2010

MGAWANYIKO mpya umeibuka kwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wenye mtizamo wa kizalendo dhidi ya wale wanaofikiria zaidi maslahi ya kibiashara, MwanaHALISI imebaini.

Saed Kubenea's picture

Serikali bado iko ‘chekechea’


Na Saed Kubenea - Imechapwa 28 April 2010

SERIKALI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inaendelea kujifunza. Itaendelea kujifunza na labda bila kufuzu.

Saed Kubenea's picture

‘Mafisadi’ waziteka kampeni za Kikwete


Na Saed Kubenea - Imechapwa 21 April 2010

KAMPUNI iliyopewa kazi ya kukusanya fedha za kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) – Push Mobile Media Limited – inahusishwa na watuhumiwa wa ufisadi nchini, MwanaHALISI limegundua.

Mwandishi Maalum's picture

Wasomi wachokonoa CCM


Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 21 April 2010

Ilishinda kwa fedha za wizi

WASOMI wawili wa Marekani wamedai kuwa angalau sehemu kubwa ya dola 20 milioni (Sh. 25 bilioni) kutoka mabilioni yaliyoibwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilitumika kuleta ushindi katika majimbo mawili ya uchaguzi mwaka 2005.

editor's picture

Serikali ya CCM si sikivu


Na editor - Imechapwa 21 April 2010

KATIKA kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani, mawaziri wanajitahidi sana kusema ‘Serikali ya Chama Cha Mapinduzi’, CCM ni sikivu sana.

M. M. Mwanakijiji's picture

Tuwarudishe wabunge wote wa CCM?


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 21 April 2010

UCHAGUZI ni njia ya kawaida katika nchi ya kidemokrasia ya kuondoa madarakani viongozi wazembe, wasio na maono, wasio na uwezo na ambao ni mzigo kwa taifa. Njia isiyo ya kawaida ni kuwashikia viboko, kuandamana na kuwatimua kama ilivyotokea huko Kyrgyzstan majuzi na kama inavyoonekana nchini Thailand.

Saed Kubenea's picture

Kikwete amevunja sheria yake


Na Saed Kubenea - Imechapwa 14 April 2010

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kujihalalisha kwa fedha badala ya sera.

M. M. Mwanakijiji's picture

Tukijiuliza maswali hatutaichangia CCM


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 14 April 2010

MWISHONI mwa juma lililopita Rais Jakaya Kikwete alizindua utaratibu wa kuchangia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu; utaratibu ambao kwa siasa za Tanzania uliasisiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mwaka jana.