CCM


Mlolongo wa Habari za Chama cha Mapinduzi

Jabir Idrissa's picture

Migawanyiko CCM inaipeleka Zanzibar kubaya


Na Jabir Idrissa - Imechapwa 07 April 2010

SAUTI ya Tanzania Zanzibar (STZ), stesheni ya redio inayoendeshwa kwa fedha za wananchi, inamnukuu Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha akilaumu watu wanaosema kura ya maoni imeshapita.

Saed Kubenea's picture

Kikwete awaangukia maaskofu


Na Saed Kubenea - Imechapwa 07 April 2010

Awatuma Malecela, Msekwa kuteta
Wenyewe wazidi kutoa maelekezo

MISIMAMO mikali ya makanisa nchini imetikisa serikali na kufanya Rais Jakaya Kikwete kuomba huruma, MwanaHALISI limeelezwa.

Hastin Liumba's picture

Moto wa kampeni chafu wawaka Tabora


Na Hastin Liumba - Imechapwa 30 March 2010

MTAFARUKU unanukia ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Tabora baina ya wanachama na viongozi. Yamezuka makundi matatu makubwa yanayotishia uhai wa chama hicho.

Ezekiel Kamwaga's picture

Kikwete hachaguliki


Na Ezekiel Kamwaga - Imechapwa 30 March 2010

Mzimu wa Lowassa wamtafuna
Migawanyiko CCM yamponza

RAIS Jakaya Kikwete hauziki kama ilivyokuwa wakati akiingia madarakani, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejiridhisha.

Salim Said Salim's picture

CCM na zimwi la Sarwatt


Na Salim Said Salim - Imechapwa 24 March 2010

SERIKALI ya Jamhuri inatenda kama vile iko kwenye mashindano na mahakama. Kila mahakama inapotoa tafsiri za katiba au kufanya maamuzi muhimu yanayogusa maslahi ya kisiasa, serikali haitaki kuheshimu maamuzi hayo.

M. M. Mwanakijiji's picture

Azimio la Arusha: CCM ondoeni matanga


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 24 March 2010

NINAZO habari nzuri na habari mbaya. Habari nzuri ni kuwa hatimaye sasa tunajua kuwa waliozika Azimio la Arusha wamegundua kwamba walifanya makosa. Habari mbaya ni kuwa chama kilichosimamia maziko ya Azimio hilo hakiwezi kamwe kulirudisha.

Mwandishi wetu's picture

Ubunge Mbeya 'vurugu' tupu


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 10 March 2010

KINYANG’ANYIRO cha ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mbeya kimeibua mgawanyiko wa aina yake.

Saed Kubenea's picture

Mtoto wa Kikwete azua tafrani


Na Saed Kubenea - Imechapwa 03 March 2010

Avunja mkutano wa UV-CCM

MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete anatuhumiwa kuvunja mkutano wa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), Masauni Yusuph Masauni, MwanaHALISI imeelezwa.

Ezekiel Kamwaga's picture

Kwa nini sikubaliani na Synovate


Na Ezekiel Kamwaga - Imechapwa 03 March 2010

KWA mara ya kwanza, kura ya maoni ya utafiti kuhusu nani angeshinda urais nchini Marekani ilifanywa mwaka 1824 kupitia jarida la The Herrisburg Pensylvanian.

Mbasha Asenga's picture

Wapambanaji CCM sawa na walevi wa mirungi wa Kisomali


Na Mbasha Asenga - Imechapwa 03 March 2010

RAFIKI yangu mmoja raia wa Kenya alinisimulia siasa za Wasomali kwamba pamoja na kujitia vichwa maji, kuna kitu kimoja tu kinawafanya wawe na suluhu ya muda katika mapambano yao.

Serapion Damian's picture

'Mafahali wa MULEBA: Ni Tibaigana, Tibaijuka, Masilingi


Na Serapion Damian - Imechapwa 24 February 2010

ITAKUWA piga-nikupige mwaka huu katika Jimbo la Uchaguzi la Muleba Kusini; na tayari michuano imeanza kimya kimya kuwania ubunge jimboni humo.

Jabir Idrissa's picture

CCM achieni Zanzibar ijizongoe


Na Jabir Idrissa - Imechapwa 24 February 2010

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinajenga siasa mbaya. Kwa kinavyoyachukulia baadhi ya mambo muhimu yenye maslahi na taifa, hapana shaka kinaelekea katika kukwamisha maridhiano Zanzibar.

Jabir Idrissa's picture

Kura ya maoni inasubiriwa sana Zanzibar


Na Jabir Idrissa - Imechapwa 17 February 2010

KILA niliyekutana naye na kujadili maendeleo ya kisiasa yanayotokea Zanzibar kipindi hiki, aliniuliza ni nini hasa serikali inachotafuta kutoka "kura ya maoni."

Mwandishi wetu's picture

CCM usanii mtupu


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 17 February 2010

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) ni "usanii mtupu." Kelele za kupambana na ufisadi zimeishia kwenye ndoa na watuhumiwa wakubwa.

Ndimara Tegambwage's picture

Kukataa Mgombea binafsi: Ni unyanyapaa wa kisiasa


Na Ndimara Tegambwage - Imechapwa 17 February 2010

WAZIRI Philip Marmo anahaha kutetea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake. Ni kuhusu hoja ya mgombea binafsi katika uchaguzi kwa nafasi za viongozi wa kisiasa.

Ndimara Tegambwage's picture

Sawa, uchaguzi Zanzibar uahirishwe


Na Ndimara Tegambwage - Imechapwa 27 January 2010

MAAFA makubwa yaja Zanzibar. Hii ni iwapo watawala – Bara na Visiwani – watakuwa vichwa ngumu na kupuuzia ushauri wanaopewa.

Nkwazi Mhango's picture

CCM ife, Watanzania wakombolewe


Na Nkwazi Mhango - Imechapwa 27 January 2010

KATIKA harakati za kujinasua (bila mafanikio) kutoka kwenye ufisadi, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekumbwa na migawanyiko ambayo inaonyesha kitazidi kuparaganyika na, hatimaye, kufa.

Innocent Ngoko's picture

Mivutano ya wanasiasa inaitafuna Mbarali


Na Innocent Ngoko - Imechapwa 27 January 2010

KWA muda mrefu Wilaya ya Mbarali imekuwa na matatizo yanayokwamisha kasi ya maendeleo yake. Siasa za makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizochipuka zamani na kudumu hadi sasa ni miongoni mwa matatizo hayo.

Saed Kubenea's picture

Kikwete njiapanda


Na Saed Kubenea - Imechapwa 20 January 2010

CCM kumfia mikononi
Vigogo kibao kutimka

KUNDI la vigogo waandamizi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) limepanga kujiondoa ndani ya chama hicho iwapo masharti yake hayatakubaliwa, MwanaHALISI limeelezwa.

Saed Kubenea's picture

Rashid Kawawa ameondoka na CCM yake


Na Saed Kubenea - Imechapwa 06 January 2010

RASHID Mfaume Kawawa, mmoja wa waasisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na taifa, ameondoka huku akiwa bado anahitajika.

Editha Majura's picture

Mrema atamani kurudia ushushushu


Na Editha Majura - Imechapwa 06 January 2010

Akiri kuwa katika mtandao wa Kikwete
Alenga upya ubunge Jimbo la Vunjo

MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP), Agustine Mrema bado anafanya kazi ya usalama wa Taifa.

Ndimara Tegambwage's picture

'Nyau' wa CCM na Sheikh Yahya


Na Ndimara Tegambwage - Imechapwa 30 December 2009

SHEIKH Yahaya Hussein, yule mnajimu mashuhuri Afrika Mashariki kwa miaka mingi, amefungulia "nyau."

Jonathan Liech's picture

Nani anashauri rais wetu?


Na Jonathan Liech - Imechapwa 30 December 2009

MAAMUZI mengi yaliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete yanaibua maswali kuhusu iwapo ana washauri wa maana au ni yeye ndiye asiyetaka kufuata ushauri.

William Kapawaga's picture

CCM Ulanga waanza kunyosheana vidole


Na William Kapawaga - Imechapwa 23 December 2009

MAKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro wameanza kunyosheana vidole. Ni kuhusu nafasi za ubunge katika majimbo mawili ya wilaya hiyo.

Nkwazi Mhango's picture

Tuunge mkono Kikwete kuizika CCM


Na Nkwazi Mhango - Imechapwa 25 November 2009

ZAMANI kulipotokea mgawanyiko ndani ya chama cha TANU/CCM, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kwa kutumia busara na vipaji vyake, harakaharaka aliitisha vikao vya Kamati Kuu ya chama na kuweka mambo sawa.

Saed Kubenea's picture

Ahadi ya Rais Kikwete kwa vijana ina walakini


Na Saed Kubenea - Imechapwa 25 November 2009

RAIS Jakaya Kikwete amerudia ndweo. Ni marejeo ya nafasi ya vijana katika uongozi na utawala nchini. Anasema katika kipindi chake cha pili cha uongozi, ataweka vijana wengi katika serikali yake.

Mbasha Asenga's picture

Kikwete ameamua kufa na mizigo yake


Na Mbasha Asenga - Imechapwa 18 November 2009

KAMA kuna kitu kimekuwa kinamsumbua Rais Jakaya Kikwete kwa muda mrefu ni uwezo mdogo wa baadhi ya mawaziri wake. Ninaamini kwa kauli zake amekuwa akijilaumu kwa nini amewapa madaraka makubwa watu hao ambao kwa kweli wameshindwa kuleta mabadiliko yoyote katika nchi.

M. M. Mwanakijiji's picture

Mgogoro wa masilahi hautaipasua CCM


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 18 November 2009

MGOGORO wa kiuongozi unaoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) bado haujakomaa kiasi cha kuitwa "mpasuko."

Mwandishi wetu's picture

CCM Mwanza nako kwafukuta


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 18 November 2009

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza hakiko salama. Kimegawanyika. Mgawanyiko umeibuliwa na makundi yanayokinzana ndani ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UV-CCM).

Mwandishi wetu's picture

Batilda, Mrema waigawa CCM Arusha


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 18 November 2009

HARAKATI za kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu mwakani zimeanza katika maeneo mengi hapa nchini, ikiwa ni pamoja na mkoani Arusha.