CCM
Mlolongo wa Habari za Chama cha Mapinduzi

UVCCM, kiota cha fikra finyu, matusi?
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) tangu zama za TANU umechukuliwa kama kiota cha kulea na kutayarisha wanachama na viongozi wa kisiasa na hata wa kiserikali kwa lengo la kujenga siha njema ya kujitawala.

Lusinde ana hoja, Kikwete hana ubavu
KATIKA siku za karibuni, mmoja wa wanasiasa wakongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Job Lusinde, ametoa kauli kwamba watuhumiwa wa ufisadi wenye nyadhifa ndani ya chama hicho wavuliwe uwanachama.

Ya Chenge yathibitisha CCM chama genge
NI lazima uwe na shahada ya falsafa ili ukielewe vema Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kadri siku zinavyokwenda ndivyo mambo yanavyozidi kudhihirisha kwamba chama tawala ni dude lisiloweza kueleweka.

Siasa-mzaha zinazidisha tu mgogoro Zanzibar
INASIKITISHA sana kuona jitihada zilizochukuliwa na vyama viwili hasimu katika siasa za Zanzibar, zimeishia.

Si bure, Manji ana lake Yanga
"Si Bure, Yussuf Manji ana lake Yanga." Ndivyo ninavyolazimika kuamini kutokana na mambo kadhaa yaliyojitokeza tangu bilionea huyo alipotia mguu Yanga mwaka 2006.

Meremeta, Serikali, na Mafisadi
KILIO kinaendelea kwa miaka mitano sasa katika vijiji sita vya Kata ya Buhemba, Wilaya ya Musoma ambapo kuna mgodi wa dhahabu uliokuwa unamilikiwa na kampuni ya Meremeta.

Jakaya Kikwete 'alivyododa' Butiama
PAMOJA na madaraka makubwa aliyonayo ndani na nje ya chama chake, Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kupitisha kile alichokiamini, alichoombea misaada na ambacho serikali yake imeshiriki kugharimia kwa kipindi cha miezi 14.

CCM kinamfuata Mugabe?
KATIKA uhai wake, akiwa kiongozi wa TANU, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere hakuwahi kupeleka vikao vya chama chake nyumbani kwake, kijijini.

Msuya amvaa Kikwete
- Ataka "mafisadi" wafukuzwe uanachama
- Makongoro Nyerere awasha moto NEC
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) "kimefunga ndoa" na mafisadi kwa kukataa kupokea ushauri wa kuwafukuza kutoka chama hicho.

Makundi CCM hayajaisha
JUMAMOSI iliyopita, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, alinukuliwa akitetea chama chake kwamba hakina makundi.

Kikwete na sauti ya Kolimba kutoka nyikani
MWISHONI mwa wiki hii Watanzania wanatarajia kusikia maamuzi makubwa yatakayofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho kukaa Butiama.