CCM
Mlolongo wa Habari za Chama cha Mapinduzi

Serikali, TCRA wanajua simu hizi
SERIKALI kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), inajivunia usajili wa simu za mkononi uliokamilika yapata miezi mitatu iliyopita.

Fikra sahihi ni kuondoa CCM

Sumaye agoma kumchafua Slaa
WAZIRI mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ameingia katika kampeni za mgombea urais wa chama chake kwa sharti la kutomchafua Dk. Willibrod Slaa.

Sera ya elimu bure inawezekana
KUNA wanaotilia shaka sera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kutoa elimu bure, kuanzia ngazi ya chekechea.

Kila uchao ni mbinu chafu mpya, tuzipuuze
KWA muda wa wiki sasa nimekuwa natumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu zangu zikilenga kumkashifu mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

CCM, upinzani wana safari ndefu
CHAMA cha upinzani ni chachu katika kufichua maovu yote ndani ya serikali. Kwa mfano kama isingekuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) masuala ya wizi Benki Kuu (BoT), yasingejulikana.

Yuko wapi aliyemsafi CCM?
VIONGOZI wasafi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanapatikana kwa nadra sana. Sisemi hawapo, la hasha! Wapo lakini ama hutengwa kwa kile kinachoitwa, “Huyu si mwenzetu†au huamua kujiweka mbali kwa kuogopa kuchafuliwa.

Kunadi mafisadi: JK kamdhalilisha Pinda
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete ameendelea kuwanadi wanasiasa wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Kisasa ameandika asichokiamini
TOLEO lililopita la gazeti hili, lilibeba makala ukurasa huu iliyosema, ‘“Hatujakomaa’ kwa midahalo ya kisiasa.” Makala ile iliandikwa na mmoja wa watu waliokulia na kulelewa katika mfumo wa chama kimoja; kufanya kazi katika chombo cha propaganda cha CCM, lakini waliokosa nyenzo muhimu za kuchambulia maisha na mazingira yao.
Mwandishi huyo ni Lucas Kisasa, meneja utawala wa magazeti yanayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi ya Uhuru, Mzalendo na Burudani.

Tendwa alifunikwa kwa rushwa ya bia 2005
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa ameporomosha bomu zito linalojeruhi hadhi yake na kukichafua kabisa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa maridhiano, Amani Karume moto
KWA kuangalia hali halisi ya mwenendo wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu, nathubutu kusifia utekelezaji wa dhamira ya maridhiano katika siasa za Zanzibar.

Njama za kuiba kura hizi hapa
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetwishwa tuhuma nzito za kuandaa mipango ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu ili kionekane kimeshinda, MwanaHALISI inaweza kuripoti.

Ya Kikwete kama ya Mugabe?
YALIYOTOKEA Zimbabwe kwa Robert Mugabe na ZANU-PF, ni kama yale yanayotokea Tanzania kwa Jakaya Kikwete na CCM: Juhudi za kubaki madarakani “kwa gharama yoyote ile.â€

Jua lawachwea Salma, Ridhiwani
KUNA wakati Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) huzusha tafrani kubwa kwenye Idara ya Zimamoto na hospitali mbalimbali inapofanya zoezi la uokozi.

Mkapa, Malecela, Sumaye wamkimbia Kikwete
VIGOGO waastafu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali, wamekacha kampeni za mgombea urais Jakaya Kikwete, MwanaHALISI limeelezwa.

Serikali inataka kuleta vita
KATIKA nchi jirani – Kenya, Tume ya Uchaguzi iliacha kazi yake ya kusimamia uchaguzi na badala yake ikafanya kazi ya kuteua rais.

Mgombea huyu hafai kuwa rais
UKIWAULIZA Watanzania leo ‘popo ni mnyama au ni ndege’ utapata majibu yanayoonyesha kiwango cha uelewa wa kila mtahiniwa. Lakini jibu sahihi ni mnyama.

CCM ni wachovu, wamefilisika kifikra
VIONGOZI na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanashangaza. Huweza kushupalia kupinga, kwa nguvu zao zote, ushauri fulani kwamba haufai, lakini huiga na kutekeleza kesho yake.

Rais anayebeba watuhumiwa hafai
BABA wa Taifa, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema: “Kwa kawaida watu makini wanaogopwa na wala rushwa; serikali ‘corrupt’ – ya wala rushwa – hutumwa na wenye fedha.â€

Kikwete, kura na watuhumiwa ufisadi
JAKAYA Mrisho Kikwete, yule mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameonyesha yuko tayari kumfukua rafiki yake wa siku nyingi, Edward Lowassa kutoka kwenye kifusi.

Kinana mwongo au msahaulifu?
TANGU mwaka 1995, Abdulrahman Kinana amekuwa meneja wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ni mwanasiasa anayejua kupanga na kupangua na kujibu hoja.

Kwa mabango haya, hofu au JK hajulikani?
Kama ilivyo ada, wananchi kwa ujumla wao wametumbukia kwenye jadi yao , wanacheza ngoma waijuayo vizuri. Ni msimu wa kucheza ngoma ya kuongopewa, ahadi nyingi, kuvalishwa fulana, khanga na kofia, zilizosheheni majina ya wagombea.
Kadri siku zinavyokaribia uchaguzi mkuu ndivyo mitaa inazidi kupambwa kwa mabango ya picha za wagombea, harakati za mabango ni kubwa, ipo mitaa na barabara nyingine mtu ukipita unajiuliza maswali magumu kidogo; kwamba nguvu kubwa namna hii ya kusaka kura ni ya nini? Na je, nani analipia mabango na picha zilizozagaa kila kona?

Takukuru mshauri wa CCM
KUMBE Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inafanya kazi zake kwa ushirikiano na Chama Cha Mapinduzi (CCM) badala ya kuwa chombo huru, imefahamika.

Nani kateua mhuni kampeni za CCM?
MTENDAJI mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba ametetea chama chake, kwamba hakihusiki na tukio la kufukuzwa kwa waandishi wa habari, wiki tatu zilipita mjini Bukoba.

Hata CCM ni ‘chama cha msimu’
KINYANG’ANYIRO cha uchaguzi kinaendelea nchini kote. Tayari watu makini wameona sura halisi ya uchaguzi itakavyokuwa.

Sitta atavuna aibu tupu kwa Dk. Slaa
MGOMBEA ubunge jimbo la Urambo, Samwel Sitta, anatafuta aibu. Anadai kuwa anataka mdahalo na Dk. Willibrod Slaa.

Kikwete sasa unapotea njia
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), sasa kimeingia katika hatua mpya ya uwepo wake. Hatua hii si nyingine, bali imezidi kujitambulisha katika alama yake maarufu ya biashara (famous trademark) – ufisadi katika ngazi za juu.

Malipo ya Salma utata
MALIPO kwa ajili ya safari za Mama Salma Kikwete, anayetumia ndege za serikali kwa safari binafsi, yameibua utata mpya, MwanaHALISI limegundua.

Msajili asilalamike tu, achukue hatua
MARA baada ya kuanza kampeni za uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, vyama mbalimbali vya siasa viliwasilisha malalamiko ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini.

Salma Kikwete kortini
SALMA Kikwete, mke wa rais anayemaliza muda wake Jakaya Mrisho Kikwete, aweza kuburuzwa mahakamani kujibu matumizi mabaya ya mali ya umma, MwanaHALISI limeelezwa.