Kagoda


Mlolongo wa Habari za kashfa ya Kagoda

Mbasha Asenga's picture

Kufunika Kagoda ni kuandaa janga


Na Mbasha Asenga - Imechapwa 07 September 2011

WAZIRI wa Fedha na Uchumi wa zamani, Zakia Meghji, alipoahidi kwamba serikali ilikuwa imeridhia kufanywa kwa ukaguzi wa Akaunti ya Fedha za Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) hakusema hivyo kwa tabasamu na bashasha, bali alilazimika kwa kuwa hakuwa na namna wala jinsi.

Saed Kubenea's picture

Msemakweli ama hajui asemacho au anatumiwa


Na Saed Kubenea - Imechapwa 07 September 2011

MTU huyu anatumika kuficha ukweli. Ni Kainerugaba Msemakweli. Anasema mabilioni ya shilingi yaliyokwapuliwa na kampuni ya Kagoda Agriculture Limited (KAL), ndani ya Benki Kuu ya taifa (BoT) hayakutumika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Anasema wezi wa Kagoda walichota fedha BoT, Februari 2006, na kwamba uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani ulimalizika Novemba 2005. Yote haya yanaonyesha jinsi Msemakweli, ama anavyotumika bila kujijua, au anavyotumiwa na watu wenye malengo binafsi.

Kile ambacho wengi hawajakifahamu, ni nani anayemtumia Msemakweli.

Mbasha Asenga's picture

Kumfunga Maranda bila wezi wa Kagoda ni bure


Na Mbasha Asenga - Imechapwa 25 May 2011

 WIKI hii mavuno ya kwanza ya haki kwa wezi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) Katika Benki Kuu (BoT) yameanza kujitokeza. Lakini hisia za watu zimeonyesha wengi kutokufurahishwa na kiwango cha adhabu.

Ndimara Tegambwage's picture

Ya DPP Feleshi, Kagoda na wasomaji


Na Ndimara Tegambwage - Imechapwa 18 May 2011

DPP Eliezer Feleshi amedai kuwa hana taarifa na ushahidi kuhusu kampuni ya Kagoda Agriculture Limited inayodaiwa kuiba zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka Benki Kuu (BoT). Wiki iliyopita, kwenye ukurasa huu, Ndimara Tegambwage alimpa orodha ya wanaosadikiwa kujua Kagoda, kuidhamini na hata kuidai, ikiwemo serikali. Je, Feleshi anashindwaje kujua Kagoda? Ufuatao ni mrejesho wa wasomaji kwa njia ya sms:

Ndimara Tegambwage's picture

DPP aweza kupoteza heshima, kazi 


Na Ndimara Tegambwage - Imechapwa 11 May 2011

UKITAKA kujua jinsi mwenye madaraka anavyoweza kupoteza heshima na hata kazi yake, msikilize Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Eliezer Feleshi.

Ezekiel Kamwaga's picture

Kizunguzungu cha Kagoda


Na Ezekiel Kamwaga - Imechapwa 02 March 2011

MFANYABIASHARA Yusuf Manji, aliyedai kuidhamini kampuni tata ya Kagoda kurejesha serikalini mabililioni ya shilingi iliyoiba, sasa anasema anashitaki Kagoda kwa kutomrejeshea fedha zake.

Saed Kubenea's picture

Wizi wa Kagoda


Na Saed Kubenea - Imechapwa 09 February 2011

YUSUF Manji, mfanyabiashara wa Dar es Salaam, ni miongoni mwa walionufaika na mabilioni ya shilingi ambayo yalikwapuliwa na kampuni ya kitapeli ya Kagoda Agriculture Limited kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), MwanaHALISI limegundua.

Balibati Kangungu's picture

Rais anayebeba watuhumiwa hafai


Na Balibati Kangungu - Imechapwa 29 September 2010

BABA wa Taifa, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema: “Kwa kawaida watu makini wanaogopwa na wala rushwa; serikali ‘corrupt’ – ya wala rushwa – hutumwa na wenye fedha.”

Saed Kubenea's picture

Zakia Meghji kuunda 'kagoda' yake?


Na Saed Kubenea - Imechapwa 30 March 2010

MASKINI Zakia Meghji. Amepewa kazi iliyotaka kumuangamiza. Amebebeshwa zigo ambalo mwaka 2005 lilikuwa limebebwa na mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.

Nkwazi Mhango's picture

Nani ataokoa Kikwete?


Na Nkwazi Mhango - Imechapwa 04 November 2009

UKIANGALIA jinsi mambo yanavyokwenda, utaona kama vile Rais Jakaya Kikwete hajali kutumbikiza serikali yake katika kashfa.

Nkwazi Mhango's picture

Kikwete ameshindwa, ameangusha umma


Na Nkwazi Mhango - Imechapwa 01 November 2009

NIMEVUTIWA na mjadala unaoendelea juu ya utendaji kazi wa Rais Jakaya Kikwete. Niseme kuwa Tanzania haijawahi kupata rais mwenye kutatanisha na aliyekatisha tamaa kama huyu wa sasa.

Saed Kubenea's picture

Kagoda yamwakia Kikwete


Na Saed Kubenea - Imechapwa 15 September 2009

Wahisani washinikiza ukaguzi
Misaada ya wafadhili yakatwa

SERIKALI imesalimu amri. Imerudisha nchini maodita wa Deloitte & Touche kutoka Afrika Kusini kufanya tena ukaguzi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), MwanaHALISI limegundua.

editor's picture

Kagoda? Tufike tamati


Na editor - Imechapwa 26 May 2009

WATANZANIA wakiulizwa wanachokitaka kuhusu ufisadi wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, tunaamini watasema kwa sauti kali, “kamata hao, shitaki hao sasa.”

Jabir Idrissa's picture

Serikali inajenga mapinduzi


Na Jabir Idrissa - Imechapwa 26 May 2009

SHAHADA mara tatu. Lakini kampuni ya Kagoda Agriculture Limited imetajwa zaidi ya mara mia. Bado inaendelea kutajwa kama moja ya kampuni zilizonufaika na fedha zilizokwapuliwa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

M. M. Mwanakijiji's picture

Mgawanyiko CCM: Kikwete njiapanda


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 25 March 2009

WABUNGE wenye msimamo kama wa mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, na wale wenye msimamo kama wa Rostam Aziz, mbunge wa Igunga, hawawezi kubakia ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wakati mmoja. Sharti wale wa msimamo mmoja watoke ili chama kinusurike.

Saed Kubenea's picture

Rostam kinara wa Dowans


Na Saed Kubenea - Imechapwa 11 March 2009

Anajuana na Dowans, Kagoda
Serikali yamwangalia tu

MWANASIASA na mfanyabiashara Rostam Aziz ana siri kubwa kuhusu makampuni ya Dowans na Kagoda Agriculture Limited yanayotuhumiwa kwa kuhujumu uchumi.

Saed Kubenea's picture

Serikali yanywea


Na Saed Kubenea - Imechapwa 25 February 2009

Ni katika sakata la Kagoda
PM, DCI, DPP waweseka

SERIKALI imeshindwa kusema lolote kuhusiana na kushiriki katika wizi wa mabilioni ya shilingi kupitia kampuni ya Kagoda Agriculture Limited.

Saed Kubenea's picture

Siri ya Kagoda hii hapa


Na Saed Kubenea - Imechapwa 18 February 2009

Mkapa na Rostam watajwa
Peter Noni, Malegesi wamo

USHAHIDI wa kwanza na muhimu kwamba fedha zilizoibwa na Kampuni ya Kagoda kutoka Benki Kuu (BoT) uliidhinishwa na viongozi wakuu nchini, sasa umepatikana, MwanaHALISI limeelezwa.

Mbasha Asenga's picture

Tusikubali kamwe Kagoda itushinde


Na Mbasha Asenga - Imechapwa 28 January 2009

ZIPO simulizi nyingi zinazoelezea hatari mbalimbali. Wapo wanaotumia joka hatari kama nondo mla watu; wengine hutumia mijitu ya miraba minne inayoishi mapangoni; na wengine hutumia majina ya wanyama wakali.

Saed Kubenea's picture

Nyaraka EPA zaibwa


Na Saed Kubenea - Imechapwa 14 January 2009

Zimo za Kagoda, Deep Green
Jinamizi lazidi kutanda BoT

UWEZEKANO wa serikali na Benki Kuu (BoT) kufanikiwa kupata ushahidi wa kuwatia hatiani waliokwapua mabilioni ya shilingi ni mdogo kufuatia taarifa kuwa nyaraka muhimu zimeibwa.

Stanislaus Kirobo's picture

Mwenye Kagoda anafahamika


Na Stanislaus Kirobo - Imechapwa 14 January 2009

NANI mmiliki wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limetd? Serikali ina uswahiba gani na kampuni hiyo hadi inashindwa kutaja mmiliki wake?

Mwandishi wetu's picture

Wizi wa mabilioni BoT: Kikwete alidanganya


Na Mwandishi wetu - Imechapwa 09 September 2008

RAIS Jakaya Kikwete hakuwa na haja ya kuunda Timu ya Kuchunguza Wizi wa fedha za EPA kwa kuwa anajua kilichotendeka, MwanaHALISI limegundua.

Mafaili ya Benki Kuu yamejaa mawasiliano juu ya udanganyifu mkubwa, hasa uliofanywa na kampuni ya Kagoda Agriculture ambayo pia yatakuwa mikononi mwa Timu yake.

Rehema Kimvuli's picture

Hivi tutalindana mpaka lini?


Na Rehema Kimvuli - Imechapwa 08 July 2008

UKISIKILIZA kipindi cha bunge, wakati mwingine unatamani kufunga redio au televisheni. Utakuta mbunge huyu anamtetea yule na yule anamtetea mwingine. Muda mwingi unapotea kwa kazi moja tu: Kuteteana!