Richmond
Mlolongo wa Habari za kashfa ya Richmond

Sumaye aliifukuza Richmond
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, alimfukuza ofisini kwake Mohamed Gire, anayedaiwa kuwa ni mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Richmond Development Company (LLC), baada ya kutilia shaka uwezo wake kama mwekezaji mwaka 2001, imefahamika.

Sakata la RICHMOND: Serikali kukwaa kisiki
MVUTANO wa aina yake unatarajiwa kuibuka wiki ijayo kati ya bunge na serikali juu ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond, imefahamika.

Edward Lowassa: Rudi uwani
MBUNGE wa Monduli, mkoani Arusha, Edward Lowassa ameibuka. Amesema hakukutana na Rais Jakaya Kikwete barabarani; wala uhusiano alioita "imara walioujenga na Kikwete" hauwezi kuvurugwa na kikundi kidogo cha watu wenye nia mbaya.

Ya Rais Kikwete kama ya Hugo Chavez
TAREHE 23 Mei 1999, Rais wa Venezuela, Hugo Chavez alianzisha kipindi cha kujibu maswali, kutoka kwa wananchi, kwa njia ya televisheni.

Edward Lowassa 'anajua atendalo'
NI nani anaweza kumpinga Edward Lowassa? Ni nani ana uwezo wa kumtenga Lowassa na rafiki yake wa siku nyingi, Rais Jakaya Kikwete?

Njama kumng'oa Spika Sitta zafichuka
- Genge lajipanga kutumia NEC
- Kikwete kuwekwa njia panda
NJAMA za kumwangamiza kisiasa Spika Samwel Sitta zimegundulika kabla waandaaji wake kuzifikisha kwenye vikao vya juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), MwanaHALISI limeelezwa.

Lowassa, Rostam wazimwa
- Ni katika sakata la Richmond
- Bomu la Dk. Mwakyembe kiporo
TUNDU la kutokea la Edward Lowassa, ili akwee upya kwenye uongozi wa juu nchini, tena kwa kishindo, limezibwa, MwanaHALISI limegundua.

Kikwete ang'ang'ania 'zigo' la Richmond
RAIS Jakaya Kikwete amejitwisha upya "zigo" ambalo tayari lilishafika ufukweni. Jumamosi iliyopita, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima alitangaza uamuzi wa serikali wa "kuwabeba" viongozi wawili waandamizi waliokuwa wanatuhumiwa katika sakata la kampuni ya Richmond Development Company (LLC).

Serikali inalipiga Bunge teke
KUNA usanii mkubwa unaendelea nchini juu ya utekelezaji wa maagizo halali ya Bunge. Sasa ni miaka miwili na nusu imepita, tangu Bunge lipitishe azimio juu ya zabuni ya kufua umeme kutoka kampuni feki ya Richmond, serikali bado haijachukua hatua.

Mafisadi wamtishia Kikwete
WATUHUMIWA wa ufisadi, wanaolalamika kuwa Rais Jakaya Kikwete amewatelekeza, wanapanga kumhusisha katika baadhi ya tuhuma zinazowakabili ili kumshinikiza kutimiza matakwa yao, MwanaHALISI limeelezwa.

Mgawanyiko CCM: Kikwete njiapanda
WABUNGE wenye msimamo kama wa mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, na wale wenye msimamo kama wa Rostam Aziz, mbunge wa Igunga, hawawezi kubakia ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wakati mmoja. Sharti wale wa msimamo mmoja watoke ili chama kinusurike.

Dowans ina harufu ya Lowassa
TAREHE 7 Februari 2008 aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa alilazimika kuachia ngazi nafasi hiyo kutokana na kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond Development Company (LLC).

Dk. Rashid, TANESCO na Dowans: Ndoa iliyoshindikana alfajiri
KWA mara nyingine, serikali kupitia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) imetangaza kujitoa katika mipango ya kununua mitambo ya kampuni ya Dowans Holding (Tanzania) Limited.

Majanga 6 ya mwaka 200
KWENYE sherehe za sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kumeibuka tathimini mpya inayoonyesha waziwazi kuwa Tanzania sasa siyo tena “kisiwa cha amani.”

Ikulu ya umma au mafisadi?
EPA na Richmond ni mchezo mmoja wenye waigizaji walewale. Hata Rais Jakaya Kikwete anajua hivyo.

Richmond: Yaliofanyika hayatoshi
KATIKA siku chache zilizopita, serikali ilitamka kwamba imevunja mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura kati yake na kampuni ya Dowans Holdings S.A iliyorithi mkataba huo kutoka kwa Richmond Development Company (LLC).

Taifa linayumba
RAIS Jakaya Kikwete ni kiongozi wa taifa na amiri jeshi mkuu mwenye jukumu la kuwa msimamizi wa ulinzi wa jamhuri na amani ya wananchi katika jamhuri nzima.

Bomu la Mwakyembe lalipuka
- Ni katika Sakata la Richmond
- Mke wa waziri alipigia magoti Kamati
MKE wa mmoja wa mawaziri watatu waliojiuzulu kutokana na sakata la Richmond, alipigia magoti baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge akiomba wamlinde mume wake, imefahamika.

Mzigo wa Dowans tumeutua, wa IPTL lini?
TAARIFA kwamba Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limevunja mkataba wa kununua umeme wa dharura kwa kampuni ya Dowans (T) Ltd, kuanzia Agosti 1, mwaka huu, zinatia moyo. Angalau kilio cha wanachi na wawakilishi wao kwenye Bunge kimeanza kusikilizwa. Mkataba huo ulikuwa ukiligharimu taifa Sh. 152 milioni kwa siku.

Hoja ya Rostam Bungeni hii
Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi hii ya kuzungumza mbele ya Bunge lako tukufu ili niweze kutoa maelezo na vielelezo kuthibitisha hoja nilizotoa katika mchango wangu wa maandishi

Sakata la Richmond: Lowassa kikombe hakiepukiki
NINAJADILI hapa baada ya kugundua jitihada zinazofanywa na baadhi ya vyombo vya habari kutaka kumsafisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kuhusu uovu wa mkataba wa Richmond, baada ya mweyewe kushindwa kujitetea bungeni.

Masikini mama yetu Tanzania, vipi?
MTU akiugua ugonjwa wa kansa na akachelewa kutibiwa hadi ugonjwa ukasambaa mwilini, hukabiliwa na hatari ya kufa, labda itokee miujiza ya Mwenyezi Mungu.