CCM wajiaibisha


editor's picture

Na editor - Imechapwa 08 February 2012

Printer-friendly version
Maoni ya Mhariri

KWA kile kilichoonyeshwa hadharani kama onyesho maalum la Sungusungu, mara tu ugawaji wa kadi kwa wanachama wapya ulipokoma, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimechoka.

Baada ya ratiba iliyovuta watu katika kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM, kilichoshuhudiwa ni maafa.

Kama kuwapanga sungusungu ndio mtaji wa chama hiki, basi uwekezaji huo hauna maana yoyote. Chama hakiwezi kupata wafuasi kwa maonyesho ya silaha za jadi.

Onyesho lile limerudisha fikra za watu kwa makundi ya vijana waliodhaminiwa na vyama tawala katika eneo la Afrika Mashariki. Youth Kenya, Interahamwe (Rwanda) na Janjaweed (Zanzibar).

Makundi hayo yalitumika kuvuruga uchaguzi na hivyo kudhoofisha dhana ya demokrasia ya vyama vingi. Pia harakati za makundi hayo zilisababisha mauaji ya raia.

Ilichofanya CCM kuonyesha sungusungu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, ni kubariki vitisho dhidi ya wapinzani wake.

Watanzania wanajua tu sasa kwamba wakizubaa na kuisema CCM hadharani au hata kifichoni, adabu yao ni kukong’otwa na sungusungu.

Tunaamini kilichofaa kuonyeshwa ni vijana waliofunzwa maadili ya uongozi, itikadi, stadi za maisha na kazi za amali ili kuwa chachu ya fikra mpya za vijana kujiajiri, badala ya kusubiri kuajiriwa serikalini.

Kuonyesha silaha na nguvu ya kuzitumia, hata kama ni za jadi, kunajenga taswira kuwa chama tawala sasa kinategemea zaidi misuli katika kuendesha siasa.

Kwamba kwa CCM, siasa siyo tena ushawishi wa itikadi unaoendeshwa kwa lugha ya kiungwana, bali ni matumizi ya nguvu na vitisho. Haiwezekani.

Hizo ni siasa za kijambazi ambazo hazijawahi popote pale duniani; isipokuwa kuzidisha usugu na vuguvugu kwa wale wapinzani wa chama husika.

Je, CCM katika umri wake wa miaka 35 imewekeza katika kuamsha hisia za vurugu nchini? Kitapigishaje kwata vijana wa sungusungu.

Ni aibu ya kihistoria kwa chama kinachojitahidi kurudi kwenye asili yake – kulinda maslahi ya wanyonge; wafanyakazi na wakulima.

0
Your rating: None Average: 3.5 (2 votes)
Soma zaidi kuhusu: