Recent comments


 • Wanawapiga, wanawatia vidole makalioni   9 years 2 days ago
  Ndipo askari wa hifadhi hiyo walipoanza cheap dress kuwatoa kwa nguvu ikiwa ni pamoja na kuwapora dhahabu walizopata na mali nyingine.
  linesa
 • Posho ya vikao vya Bunge za Wabunge   9 years 3 days ago
  Hivi jamani mtu akikusimamisha barabarani akakuuliza serikali yako imefanya nini ambacho kimenufaisha taifa kama Hakuna kipaumbele katika miradi muhimu kama kilimo, maji, umeme unapandishwa bei na kila siku nchi ipo gizani, barabara mbovu, mafuta ya kula, ya taa, petrol na diesel bei juu! serikali gan kama gharama za maisha ya walioipa ridhaa yanazidi kuwa magumu na kila kukicha ni heri ya jana! mbona Libya sivyo? mbona Rwanda mambo safi, kwanini Congo ina maendeleo makubwa sababu ya mchango wa madini? kwan sisi hatuna madini au kuna nchi zinaitwa migodi ndani ya TZ ambazo si sehemu ya TZ? Misamaha ya kodi, rushwa na biashara haramu. Hivi..tunahitaji Nini au nani aje kuinyoosha nchi?? Miaka 50 ni mingi tangu uhuru lakini maendeleo ya nchi yanaonekana kupiga hatua mbili mbele, hatua tano nyuma yana hata kobe ana spidi kubwa jamani.
  Nextlevel
 • Posho ya vikao vya Bunge za Wabunge   9 years 4 days ago
  Jamani tufunguke akili kiutendaji, ni kwa nini tuingize sisa kwenye Elimu? Naomba kuuliza chuo kikuu cha Dodoma ni cha CCM au Taifa? Ni kwa nini maamuzi yanaendeshwa kisiasa na sio kielimu au kisayansi? na kuna umuhimu gani wa kusomea fani fulani halafu unakuja kufanya kazi tofauti na fani yako? Hayo ndio mambo yaliyopo Chuo Kikuu Cha Dodoma. Tuamke watanzania tuache kusifu chama na watu fulani weenye maslahi yao binafsi kwa nchi yetu. Iweje nchi ya Tanzania yenye rasilimali nyingi izidiwe kiuchumi na nchi ndogo na yenye vita kama Burundi!!!?
  vincent
 • Unatafsirije CCM kuteka hoja za wapinzani (Katiba mpya, Vita ya ufisadi n.k)?   9 years 1 week ago
  Kiukweli ni jambo ambalo linakuwa mshangazo kwa wananchi,watu ambao wametumwa na wananchi kutetea hali ya maisha ya waliowatuma lakini inakuwa kinyume na matarajio ya walio wengi. Hata kitendo cha kulilia posho nacho hakina uungwana kwa waheshimiwa hawa. waache hizo pesa ziende majimboni na taasisi nyingine zifanye maendeleo yanayoonekana dhahiri kwa kitaifa na hata kimataifa. Tanzania kuendelea kuitwa nchi masikini ni jambo ambalo linasababishwa na hawa tunaowaamini kuwa ndio watasaidia kuepusha balaa hili.
  Isdory Mwesiga
 • Unatafsirije CCM kuteka hoja za wapinzani (Katiba mpya, Vita ya ufisadi n.k)?   9 years 1 week ago
  Si dhani kama wabunge wa CCM wanajua walifanyalo ndani ya bunge,wanaleta ushabiki usiokuwa na maana wakati watanzania tulio wengi tunahitaji maendeleo.
  macrusy
 • Lowassa amkatia rufaa Kikwete   9 years 1 week ago
  MH.LOWASSA nakushauri uachane na siasa za Tanzania. Wasaidie vijana wafanye siasa. Wewe kama wewe sasa hali ni tete na kurudi kwenye upepo wa siasa kutazidi kukugharimu. Natambua watu wa monduli wanakupenda sana kwa sababu ya maajabu uliyowatendea. Lakini watanzania wanasuasua kuhusu ukweli wako juu ya kuwanyonya watanzania. si rahisi kwa sasa wewe kuwaambia tena watanzania lolote wakakusikiliza. Ninachojua mimi ni kwamba VIJANA SASA WAKO MOTO KWENYE SIASA. Vijana wako tayari kuingia upinzani ili kutimiza malengo. Hakuna namna ya kuwarudisha nyuma wala kuwazima. Unajua mh. Siasa zina msimu wake. Na nafikiri msimu wako umekwisha. Kubali matokeo mzee wangu. ushauri wangu ni huo. nikipata muda nitaendelea kukushauri SIR LOWASSA. GOOD LIFE.
  polisi-wa-mkulima
 • Lowassa amkatia rufaa Kikwete   9 years 1 week ago
  MH.LOWASA NI MCHAPA KAZI,KATI YA VIONGOZI AMBAO NILIKUBALI UTENDAJI WAO WA KAZI WAKATI SERIKALI YA AWAMU YA NNE INAINGIA MADARAKANI NI WEWE KILICHOKUPONZA MH.WANGU NI KUTOMTAJA MHUSIKA WA KAMPUNI AMBAYO ILIPELEKEA UJIUZULU WADHIFA WA WAZIRI MKUU,KUKAA KWAKO KIMYA NDO MAANA WENZAKO AMBAO ULIWAHIFADHI WANAKUKABA KOONI KWA KUWA WANAJUA UNA USHAWISHI MKUBWA KAMA UTAAMUA KUINGIA KTK KINYANG'ANYILO CHA URAISI NDANI YA CHAMA CHA CCM.USHAURI WANGU NI KUWA WAANIKE WALIOKUBEBESHA MZIGO WA LAWAMA ILI UJIWEKE KTK MAZINGIRA MAZURI WANANCHI WANAKUMBUKUA UTENDAJI WAKO WA KAZI MH.WANGU.KAZA BUTI.
  NTIWOMI WAIBARA
 • Mbowe ana hoja kukataa kutia amri ya Hakimu wa Arusha?   9 years 1 week ago
  KUKAMATWA KWA MBOWE NI MATUNDA YA SEMINA ELEKEZI ILIYOMHUSISHA JAJI MKUU AMBAYO KUWEPO KWAKE KULITILIWA SHAKA NA GAZETI PENDWA LA MWANAHALISI, LIKIHOJI JAJI MKUU NI SEHEMU YA SERIKALI? JAJI MKUU WA TZ ALIHUDHULIA SEMINA ILIYOWAHUSU WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI CHA AJABU JAJI SI SEHEMU YA SERIKALI SIKU CHACHE BAADAE MBOWE AKAKAMATWA KAMA GAIDI WA KIMATAIFA NA KUSAFIRISHWA HADI ARUSHA KWA GHARAMA KUBWA KUMBE ILIKUWA NI SEHEMU YA MAAGIZO YALIYOTOLEWA KWENYE SEMINA HIYO.SINA IMANI NA CHOMBO HIKI KWANI KINAFANYA KAZI KWA KUAGIZWA NA WANASIASA WASIO NA HATA CHEMBE LA UCHUNGU WA KUFIKILIA UMASKINI WA MTANZANIA BALI MATUMBO YAO PEKEE.
  NTIWOMI WAIBARA
 • Azzan: Wanaonichafua ni Guninita, Ng’enda   9 years 1 week ago
  Mheshimiwa mbunge Azzan anapokea maoni na ushauri wenu hapa http://www.tathmini.com/Pages/Details/7/iddi-mohamed-azzan kuhusu utendaji wake wa kazi. Msimuangushe wananchi
  mcso
 • Lowassa amkatia rufaa Kikwete   9 years 1 week ago
  Mheshimiwa mbunge Lowassa anapokea maoni yenu hapa http://www.tathmini.com/Pages/Details/2/lowassa-ngoyai-edward kuhusu utendaji wake wa kazi
  mcso
 • Mbunge: Katiba imevunjwa   9 years 1 week ago
  Mheshimiwa mbunge Israel anapokea maoni yenu hapa http://www.tathmini.com/Pages/Details/253/natse-yohana-israel kuhusu utendaji wake wa kazi. Msimuangushe wananchi
  mcso
 • Serikali ina kasumba na makocha wa kigeni   9 years 1 week ago
  kasumba ni kitu kibaya sana..fikiria enzi zile barabara hazijengwi mpaka kiongozi aje..tuachane na kasumba,mtanzania akiwezeshwa anaweza..
  OMOTESANDO
 • Lowassa, Rostam kumzima Kikwete   9 years 1 week ago
  Si kwamba Lowasa hana nguvu kama watu wanavyomthania, bali Lowasa anaweza kuwa na nguvu kutoka na support ya watu hasa anakotokea. Pia hatuwezi kumuita Lowasa ni mwizi wakati ushahidi hatuna,chombo pekee kinachoweza kuprove kwamba Lowasa ni mwizi au si mwizi ni Mahakama pekee kam chombo cha kutafsiri sheria.
  fadhili kimanga
 • Tanzania: Aibu tupu Marekani   9 years 1 week ago
  Kweli inchi hii hamnazo..!! Kosa binafsi kwa shughuri binafsi tena za Mama Lishe iweje zifanyiwe mchakato wa kulipia kwa kutumia kodi za raia!!!!??? hapo kuna walakini na utumishi wa UMMA wa Jamhuri hii.
  tall Kahigi
 • Unatafsirije CCM kuteka hoja za wapinzani (Katiba mpya, Vita ya ufisadi n.k)?   9 years 2 weeks ago
  Wamejimaliza kwani hizi hoja zina madhara kwao
  Theo
 • Lowassa, Rostam kumzima Kikwete   9 years 2 weeks ago
  Lowasa hana nguvu kama watu wanavyompamba. Kinachomsaidia ni udhaifu wa Kikwete. Kikwete salama yake na chama chake ni kuwatimua hawa wezi ingawa sina hakika kama naye si mwizi.
  fidodido
 • Lowassa, Rostam kumzima Kikwete   9 years 3 weeks ago
  Mheshimiwa mbunge Rostam anapokea maoni na ushauri wenu hapa http://www.tathmini.com/Pages/Details/1/azizi-abdulrasul-rostam kuhusu utendaji wake. Kazi kwenu
  mcso
 • Lowassa, Rostam kumzima Kikwete   9 years 3 weeks ago
  Hivi kweli nani anao ushahidi wa kutosha kwamba Lowasa ni fisadi?Lowasa alitolewa kafara kwa sababu ambazo ni za kisiasa tu na ni vema jutenge utamaduni wa kujiaminisha kwa jambo kabla ya kuwasulubisha watu. Lowasa mwenyewe anajua vizuri sababu za yeye kutoswa na ndio maana wakati anajiuzulu alisema najua kinachotafutwa ni uwaziri mkuu. Namhurumia sana Lowasa, katendewa mambo mengi mabaya na kunyamaza, sasa ameamua kuamka usingizini na kusema..ameikatalia hata CCM yenyewe na CCM wamenyamaza. Tusimuue Lowasa yule mchapa kazi. Hata mimi nilimlaumu sana Lowasa lakini sasa nimeamua kutafakari upya juu ya ufisadi wa Lowasa..ila Lowasa naye atuambie kilichifichwa chini ya Dowans..hilo tu lakini ukweli umeanza kujulikana juu ya Lowasa, CCM na Kikwete mwenyewe.
  emmanuel1976
 • Ukombozi waja… kipigo chayoyoma   9 years 3 weeks ago
  kazi ipo
  alekiso
 • Lowassa, Rostam kumzima Kikwete   9 years 3 weeks ago
  Katika harakati za kukimegea hekima chama chake alichokiasisi Mwalimu Nyerere aliwahi kuonya, tena muda mfupi kabla hajatutoka kwamba hakuna Rais atakayeingia madarakani kwa njia ya rushwa anayeweza kupambana kikamilifu na rushwa. Haya sasa yamedhihirika baada ya Kikwete kupigiwa kampeni kwa fedha chafu za mafisadi na EPA na hatimaye kupenyezwa madarakani na mafisadi papa ambao vivuli vyao vinamfanya aweweseke hadi leo hii. Inashangaza sana kuona walewale aliokuwa akiwaamini kama watetezi wa kile alichokiamini ndiyo walikuwa wa kwanza kuyafungua makucha yao na kufanya kufuru ya ufisadi wa kutisha mara tu baada ya kifo chake. Ilikuwa kana kwamba walikuwa wakimwombea afe ndiyo wafanye hujuma hiyo. Ni kuanzia baada ya kifo cha mwanamapinduzi huyu CCM ilipoteza kabisa uelekeo na kujitoa kwa wakulima na wafanyakazi na badala yake kuwa chama cha wezi, vibaka, mafisadi na wahujumu uchumi. Ni katika wakati huhu huo mali na amali za taifa zilihujumiwa vya kutisha, kuanzia ardhi hadi nyumba watu waligawana! Sote tu mashahidi wa jinsi CCM ilivyokuwa ikiitisha "Harambee" za kutafuta michango toka kwa wafanyabiashara wengi wao wakiwa wezi, vibakauchumi na mafisadi papa. Haya ndiyo matokeo ya serikali inayomilikiwa na mafisadi waliojipenyeza mpaka kwenye "Injini" ya dira ndiyo chama. Kwa sasa ni vigumu kumpata aliye safi ndani ya CCM, na kama yupo basi hana mahusiano mema na wenzie. CCM imekwenda kinyume cha kila aina ya mafundisho waliyoaswa na mwasisi wao. Aliwaonya juu ya udini na ukabila akisema "kiongozi makini huzungumzia sera za nini atafanya kwa ajili ya nchi yake, lakini kiongozi aliyefilisika atazungumzia udini na ukabila" Je kuna hata chembe ya mashaka kwamba CCM wametenda kinyume cha nasaha hizo? Sisi sote tu mashahidi jinsi walivymdhalilisha kada wao kwa kumwita mwarabu na kumhusisha na mauaji ya aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar! Na leo hii tunashuhudia Rais mzima akipanda jukwaani kuimba wimbo wa udini huku mwangi wake upipaazwa na viongozi wasio makini wa kidini wenye kujipendekeza kwa manufaa binafsi! Laana ya Baba wa Taifa hili inaitafuna CCM na sasa wamelewa na kuviimbiwa sumu ya ufisadi waliyoichangamkia fasta fasta tangu kifo cha muasisi wao aliyeonekana kuwaletea giza na bughudha dhidi ya harakati zao chafu ambazo sasa ndiyo wanahunyahunya kuondokana nazo. CCM wana chaguo mbili tu, nazo ni kufanya usanii sanii na kuachana na sera zao za kujivua magamba ambazo kwa kweli hazitekelezeki kwani karibu wooote wameshaonja ladha ya ufisadi, au wachukue hatua za papara za kuwang'oa maswahiba wao na kuangukia pua mara moja! Waziri Mkuu Pinda alishawahi kusema kwamba mafisadi wana nguvu za kutisha na kupambana nao bila ya tahadhari kunaweza kuiyumbisha serikali. Je sasa wakati umefika wa serikali iliyowekwa na hawa hawa watu kupambana nao na kuikabidhi mikononi mwa umma? Tusubiri, tuone. Muda utaamua. Mungu ibariki Tanzania.
  Nditu
 • CCM wapanga kuhujumu CHADEMA   9 years 3 weeks ago

  Namna hii ya utendaji katika serikali inapatikana katika serikali ya Kikwete na chama chake kichovu cha CCM tu.
  Uko wapi weledi wa Bwana Saidi Mwema aliutuahidi alipoteuliwa kuwa IGP? Utendaji wa Jeshi la Polisi sasa umekuwa ovyo kabisa kuliko wakati wowote tangu nchi hii ipate Uhuru. Polisi katika utawala ovyo wa Kikwete na Vibwetere wenzake wameshaua watu wengi wasio na hatia kinyemela labda kuliko ilivotendeka katika utawala wowote tangu nchi hii ianze kujitawala.
  Sasa Polisi ni rasmi tawi la kiitikadi la chama kichovu kinachokata roho cha CCM. CCM wanaitumia polisi kama taulo la kukaushia uchafu wao na kansa hiyohiyo imesambaa katika vyombo karibu vyote vya dola ikiwemo JWTZ ambalo kabla ya uchaguzi mwaka jana kiongozi mmoja wa juu mshabiki wa Kikwete alikurupuka na kuishangaza dunia kwa uropokaji uliokemewa ndani na nje ya nchi hii! Ni JWTZ iliyotumika kikamilifu kusambaza kura za wizi kwa magari yao utadhani nchi hii ni ya utawala wa kijeshi! Usalama wa Taifa ndiyo kabisa wamekuwa idara mojawapo ya CCM kwani wamekoma kabisa kushughulikia usalama wa taifa na sasa wanahunyahunya na usalama wa chama kibovu hiki, tena kwa gharama tunazolipa sisi!
  IGP Mwema anaweza kulitajia taifa hili gharama zilizotumika kwa sinema ya kijinga ile ya kutumia mamilioni kwa ajili ya mtu maarufu aliyejisalimisha mwenyewe polisi?
  Serikali ya vilaza wa CCM inalialia eti CHADEMA ina njama za kuitoa madarakani, ukweli ni kwamba wachawi wanaoifanya serikali hii ichukiwe wamo ndani ya utendaji wake usio makini na uliojaa usanii. Ndiyo maana CHADEMA wanaposimama jukwaani kuielezea hali halisi wananchi wengi wanawaelewa na kuwaamini. CHADEMA wanapaswa kuitumia vema fursa hii ya ujinga wa chama kichovu hiki kilichosheheni umafia na ufisadi.
  Ni CCM wanaohangaika na kuupaisha umaarufu wa CHADEMA na makada wake.Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa. Kwa
  mwenendo huu kifo cha CCM hakiepukiki. Muda utaamua. Mungu ibariki Tanzania, wabariki viongozi wenye kusimamia ukweli.

  Nditu
 • Lowassa, Rostam kumzima Kikwete   9 years 3 weeks ago
  ni habari njema kwetu..
  fidi
 • Lowassa, Rostam kumzima Kikwete   9 years 3 weeks ago
  KIKWETW HASIMWOGOPE MTU KAMA KWELI ANA NIA NZURI NA CHAMA.
  passian
 • Lowassa, Rostam kumzima Kikwete   9 years 3 weeks ago
  Hii ni habari njema sana, naona sasa tunakaribia mwisho wa CCM. Tuombe tu huu mvurugano uendelee wagawanyike watoke madarakani, nchi ianze kupiga hatua za maendeleo sasa!!
  Babu lao
 • Dk. Kitine: Mtandao wa JK umeivuruga nchi   9 years 3 weeks ago
  Nayaheshimu sana mawazo ya Mzee huyu aliyepata kuwa Mkuu wa Usalamawa Taifa enzi za Mwalimu.CCM inao watu wengi wenye mawazo ya kimaendeleo, laiti wangetumika vema wasingekuwa wamefika hapa walipo sasa. Kwa hakika CCM ni sikio la kufa ambalo kamwe halisikii dawa kwani anapotokea mtu mwenye kuthubutu kuwakosoa akiwa ndani ya CCM mtu huyo huchukiwa, kusakamwa na hata kuhatarishiwa maisha yake. Kuna wakati (Katika awamu ya kwanza ya Kikwete) kina Slaa walipoibua kashfa za Richmond na EPA wananchi waliichukia kwelikweli CCM kiasi cha kuwazomea wabunge wao ambapo hali hiyo ilikuja kutulizwa na kundi la baadhi ya wabunge waliojipambanua baadae kwa kujiita wanaharakati wa mapambano dhidi ya ufisadi wakiwemo Dr. Mwakyembe, Anna Kilango, wakiongozwa na Spika Sita.wananchi walirudisha imani yao hadi CCM kupata kibali tena machoni pa watanzania waliokuwa wamekata tamaa, lakini hebu ona jinsi 'Walivyoshughulikiwa'. Sasa kwa kumuogopa Sita na kumwadhibu wamemweka Makinda ambaye wanaamini atakuwa na kazi moja tu kupokea "Amri" toka Lumumba na Dodoma kwa kina Makamba na sasa Mkama na msanii Nape. Kwa hakika mtunzi wa kifo cha CCM ni CCM wenyewe na CHADEMA wanasingiziwa tu. Maamuzi mengi yanayofanywa sasa na CCM ikiwa pamoja na kushawishi matumizi mabaya ya vyombo vya dola kuwabana wapinzani wanaoonekana wazi kuwashinda CCM kwa hoja yanazidi kuleta kichefuchefu, kuishushia hadhi CCM na kuwakatisha kabisa tamaa wachache wanaoipenda. Sitashangaa na kamwe kama CCM itabadilishana na CHADEMA uwingi wa viti Bungeni ifikapo 2015. Ni CCM waliompa Sita umaarufu uliopindukia, ni CCM hiyohiyo iliyoipa CHADEMA umaarufu mkubwa kwa kuipiga madongo ya udini na ukabila ambayo baada ya wananchi kuyachunguza wamebaini ni ulaghai tu wa CCM na sasa wameamua kushikamana na CHADEMA na kwa njia hii kuiongezea CHADEMA umaarufu mkubwa pengine kuliko walivyostahili, hebu jiulize kabla ya suala la Buzwagi ni wangapi waliokuwa wakiuelewa umaarufu wa Zitto Kabwe? Na sasa wanaupaisha umaarufu wa Mbowe, Slaa, Lema na wengine ambao natabiri ifikapo 2015 watakuwa mwiba mchungu kwa CCM na kuishikisha adabu vilivyo. Hivi hakuna wenye busara waliobakia ndani ya CCM ambao bado hawajaleweshwa na mvinyo wa ufisadi wanaoweza kukishauri vema chama ili kisielekee kuzimu inakokukimbilia? Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
  Nditu