Recent comments


 • Mafisadi CCM wageuka mbogo   9 years 4 weeks ago
  MTANDAO UMEIGHARIMU CCM.
  passian
 • Askofu KKKT katika tuhuma nzito   9 years 4 weeks ago
  TANZANIA NA UTAMADUNI WA UFISADI Miaka ya hivi karibuni neno ufisadi limekua neno maarufu sana midomoni mwa watu na kwenye magazeti nchini Tanzania ,nadhani imefika wakati sasa watu wameshazoea kuona hili neno magazetini na wengine hawashtuki tena wakisikia habari za ufisadi kwani kila kukicha habari mpya za ufisadi zimekua zikiibuliwa, hii ni kuonyesha namna gani gani ufisadi umetamalaki katika ofisi zetu za Tanzania iwe ya umma au binafsi ama mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kifupi ngo, ninabaki najiuliza: je huu ufisadi ni utamaduni wetu? au ni ugonjwa tu umeingia ambao unatakiwa kutibiwa mara moja kwa njia ambazo wengi wamezisema na wengine kuzitumia ? Najiuliza maswali haya kwa kuangalia namna gani wamejaribu kutatua hili tatizo na mafaniko yake katika kutatua hili tatizo yamefikia wapi; njia ya kwanza ni kuwafukuza mafisadi wote, kuna watu wanasema hawa mafisadi wafukuzwe iwe kwenye ofisi au chama ama nafasi za juu za serikali ama za chini na kuna mifano mingi ambayo tumeona hawa mafisadi wakifukuzwa na wengine wakijiuzulu, lakini je mafisadi wameisha nchini Tanzania? je hilo limekuwa suluhisho la kudumu?je hamna mafisadi wengine waliozaliwa au kuanza ufisadi hata baada ya wengine kuwajibishwa jibu ni hamna mafanikio Njia ya pili ni kuwatangaza hadharani mbele ya wananchi kama tunavyoona Chadema wanavyofanya na baadhi ya magazeti Ambayo yamekua yakitangaza habari na kuibua taarifa mbalimbali za ufisadi kila kukicha ambazo zimewashtua wananchi na kuwasononesha wengine ,lakini je ufisadi umepungua ?je hao waliotangazwa kufanya ufisadi wameacha?la hasha Njia ya tatu na ya mwisho ni kuwazomea mafisadi hii njia tumeiona wakati wa uchaguzi ambapo wananchi waliwazomea baadhi ya wagombea ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi na wengine walidirki hata kumzomea raisi mstaafu mheshimiwa Benjamin William mkapa ambaye anatuhumiwa kwa ufisadi mwingi na wa kutisha kipindi cha utawala wake na yote hayo yamefanyika lakini tunarudi katika swali letu, je ufisadi umeisha nchini? Njia zote tatu zimeonekana kushindwa katika mapambano dhidi ya ufisadi , kwa maana nyingine tumeshindwa kulitatua hili tatizo ndugu zangu watanzania pamoja na kuliona tatizo na kujaribu kulitatua kwa njia zote hizo inaonekana imeshindikana,kwa nini?inaonekana ni mfupa uliotushinda Jibu lipo wazi tunajua tatizo lakini hatujui chanzo cha tatizo.Ni kama mfano wa bomba ambalo linavuja maji,tunajua linavuja maji na ni tatizo na tunajaribu njia zote za kufanya ili kutatua tatizo la kuvuja kwa maji kwenye bomba kwa kuweka viraka, kufunga na mpira pale panapovuja na hata tumejaribu kuweka bomba jipya lakini imeshindikana kwani bado kila baada ya muda fulan wakati tunadhani tumetatua tatizo, bomba letu linaanza kuvuja, tena kwa fujo zaidi Ndugu mtanzania chanzo cha ufisadi ni utamaduni wetu,ambao tumeujenga ,tumeulea na kuupalilia.lakini labda wengi hawaelewi utamaduni ni nini,ningependa kuwasaidia ili tuweze kwenda sambamba na kitu ninachokiongelea.kwa Kiswahili rahisi tu utamaduni ni aina ya maisha ya kila siku ambayo kikundi cha binadamu wanafanya katika maisha yao ili kuweza kuishi kama kikundi ama ninaweza kusema utamaduni ni mazoea ambayo binadamu au kikundi Fulani kinafanya ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha Kutokana na tafsiri ya neno utamaduni kama mazoea tunaona kwamba kwa watanzania ufisadi umekuwa sehemu ya utamaduni wake,yamekuwa maisha yake ,wale wanaofanya ufisadi wanaonekana ni wajanja machoni mw a watu na kila mtu anayepata nafasi ya kushika uongozi anajaribu kufanya ufisadi wa hapa na pale hata kama ni mdogo kiasi gani basi ataufanya ili kuonyesha kwamba yeye ni mtu mkubwa na ana ofisi kubwa ,ni mazoea tu kwani anaogopa kwenda kinyume na utamduni ambao utamcheka mwisho wa siku atakapopoteza uongozi na watu wataanza kusema “jamaa alikuwa mtu mkubwa serikalini lakin saizi anaishi maisha magumu ni mjinga kabisa ona wenzake wanavyoishi”Ni misemo ya mtaani tu lakini yana maana kubwa ,yanabeba fikra za wananchi ,fikra za taifa na binadamu wote wanaoishi katika jamii ile,sio maneno ya kudharau hata kidogo Huo ni mfano wa neno moja tu kati ya lukuki yanayoendelea mtaani na hata viongozi wengine wanashawishiwa na ndugu na marafiki wafanye ufisadi asije kuonekana ni mjinga atakopotoka ofisini hana kitu wala kamradi Hili jambo sio dogo hata kidogo ni suala la kukaa chini na kutafakari namna gani ya kulitatua moja kwa moja bila kurudia makosa kwani ufisadi unaonekana tulianza kuulea kipindi cha hayati baba wa taifa mwalimu Julius.K.Nyerere ambapo waliovurunda walihamishwa kutoka ofisi moja kwenda nyingine,kwa kipindi kile kutokana na uhaba wa wataalamu tunaweza kuelewa kidogo, ila miaka ilivyozidi kwenda kipindi cha awamu ya pili cha rais mstaafu mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi ambapo tulishuhudia makampuni mengi na mashirika yakifilisiwa na mafisadi na mchezo ukazid kuendelea kwenye kipindi cha Raisi mstaafu mheshimwa Benjamin William Mkapa ambapo ufisadi wa kutisha umetokea serikalini na kipindi hiki cha awamu ya nne ndo usiseme mambo ya ufisadi yanaendelea na yanaota mizizi ambayo yamekomaa Pamoja na kelele za wadau mbalimbali ambao wanapinga ufisadi ama kwa lugha nyingine wanapinga huu utamaduni ambao umejegeka miongoni mwa watanzania bado kazi ni ngumu kwelikweli kufanikwa kuuondoa ama kuupunguza kasi kwa mwendo unaokwenda kwani juhudi zote zinazofanywa zinaonekana hazilengi kwenye chanzo bali kwenye tatizo Ushauri wangu kwa watanzania ni kwamba ili tufanikiwe kuutokomeza ufisadi inabidi twende kwenye chanzo, kwenye namna watanzania wanavyofikir kwa kubadili mitaala ya elimu ama kuongeza somo la maadili na uzalendo katika shule za msingi kwenda elimu ya juu . Kubadili jinsi watanzania wanavyoheshimu wazee walioishi maisha yasiyo ya kifisadi na kuwapa nafasi zaidi kutoa michango mbalimbali katika jamii bila kusahau kuwapatia maisha mazuri na pia kuongeza juhudi kwenye kuwapongeza na kuwatuza wote wanaofanya vizuri makazini na sio kusubiri mpaka anastaafu na kufa ndio mnamkumbuka Na mwisho vilevile kuboresha maisha ya mtanzania kwa kutokuwa na wasiwasi ana postaafu ataishi vipi kwa kumhakikishia anapata pensheni nzuri na isyochelewa wala kuwa na matatizo kwani wengi wetu tuna wasiwasi tukiacha kazi tutaishi vipi kama sitakuwa na kimradi kakunisukuma uzeeni,hii inakua ni kitu ajabu sana kwani badala ya kustaafu kazi na kupumzika inabidi utafute mtaji wa kufanyia kazi tena kumsukumia maisha yake atakapostaafu hii ni hatari na ni moja kati ya sababu nyingine ya kufanya ufisadi usiishe.
  mwana anthropolojia
 • Bangi haifai, haifai!   9 years 4 weeks ago
  Nimesoma tahariri yako na kuhisi inawezekana hawa wabunge ni miongoni mwa wazalishaji maana haiwezekani kuwa hawaoni madhara ya zao hilo mpaka wanapendekeza hivyo, kweli mla nawe si mfa nawe bali mzaliwa nawe.
  MAEDA
 • Mbowe ana hoja kukataa kutia amri ya Hakimu wa Arusha?   9 years 4 weeks ago
  HUU UKABILA NA UKANDA KATIKA WIZARA NA MASHIRIKA SERIKALINI UTAISHA LINI JAMANI..WIZARA ZIMEJAA WATU WA MAKABILA FULANI FULANI HIVI MPAKA KERO..NILIWAHI KWENDA OFISI MOJA KUFANYA KAZI YA KUJITOLEA SASA NIKASHANGAA MFANYAKAZI MMOJA AKANIULIZA HIVI WEWE NI KABILA GANI NILIVYOMJIBU NIKAONA KAMA HAKUWA NA INTEREST TENA HAKUVUTIWA NA LILE KABILA NILILOKUWA NALO PENGINE NINGEKUWA KABILA LAKE ANGEWEZA KUJITOLEA ZAIDI..NILIPATA KAZI WIZARA MOJA HIVI SASA BAADA YA MUDA MKUU WANGU WA IDARA AKANIULIZA HIVI WEWE NI KABILA GANI?NIKAMJIBU AH HAKUENDELEA ILA MIMI NIMECHUNGUZA SANA NAONA HII NI SUMU KUBWA SANA KTK MAENDELEO YA TAIFA LETU USIPOKUWA MHAYA AU MNYAKYUSA AU MNYATURU AU MCHAGA HUPATI KAZI WALA KUONGEZWA CHEO AU KUPEWA TRIPS ZA KWENDA SITE!!!TUACHENI JAMANI HUU UBAGUZI..LEO UKIENDA TRA UTAKUTA KINA MUSHI NA KIMARIO KIBAO MPAKA WANAAMUA KUBONGA KIKWAO OFISINI,UKIENDA WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAKAZI UTAWAKUTA KINA RUTASHOBIA KIBAO NA RUTABANZIBWA,KABUSINJA,RWEGASIRA,MWAKANYAMALI KIBAO MPAKA UTASIKIA KICHEFUCHEFU HIVI HILI TAIFA LIMEFIKIA PABAYA KIASI HIKI MAANA AKE NINI..NDO MAANA YULE JULIUS NYERERE ALIWAHI KUSEMA MAKABILA MAKUBWA YASIPEWE UONGOZI WA JUU WA NCHI NI HATARI WANAEZA KUIPINDUA NCHI NA KUTUGEUZA WENGINE WATUMWA KTK NCHI..THE MAN WAS RIGHT 100%
  mchanaji
 • Askofu KKKT katika tuhuma nzito   9 years 4 weeks ago
  TAMKO LA WAISLAMU MWANZA DHIDI YA MFUMO KRISTO Ç`»uH÷q§9$# ÉOÏm§9$# TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU JIJINI MWANZA KUHUSU HALI YA KISIASA, KAULI ZA MAASKOFU, NA MUSTAKBALI WA NCHI LILILOTOLEWA JUMAPILI TAREHE 23 JANUARI, 2011 KATIKA VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI MBUGANI (MUSLIM SCHOOL), JIJINI MWANZA UTANGUZI: Mwaka 2010 ulikuwa mwaka wa Uchaguzi wa viongozi wa ngazi mbali mbali wakiwemo madiwani, wabunge, wawakilishi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar. Kabla ya Uchaguzi huo, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), kupitia Idara yake ya Kichungaji ya Tume ya Haki na Amani, lilitoa Waraka wa Kichungaji lililouita "MPANGO WA KUHAMASISHA HUDUMA YA KICHUNGAJI KATIKA JAMII KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2010 na baada ya muda wakatoa walichokiita ILANI YA UCHAGUZI NA VIPAUMBELE VYA TAIFA. Huu ulikuwa mweleko mpya wa Kanisa kuingia katika siasa mia kwa mia kwani huko nyuma Kanisa halikuwahi kutoa Waraka wenye maudhui kama hiyo na halikuwahi kutoa Ilani ya Uchaguzi na Vipaumbele vya Taifa. Kwa kuelewa hatari ya Waraka na Ilani hiyo ya Kanisa, waislamu walipinga kwa nguvu zote mwelekeo huu mpya wa Kanisa. Hata baadhi ya wanasiasa wenye upeo, akiwemo Mzee Kingunge Ngobale Mwiru, walikemea mweleko huo wa Kisiasa wa Kanisa Katoliki lakini wakabezwa kwa kuambiwa kuwa wamezeeka na kufilisika kisiasa na hata kutakiwa wanyamaze kimya. Baada ya waislamu kuona kuwa wamepuuzwa, na kwa kuelewa nafasi yao kwa waislamu, Shuura ya Maimamu Tanzania, ikatoa maelekezo kwa waislamu kupitia "MWONGOZO KWA WAISLAMU" ili waislamu "Wasidhulumu wala wasikubali kudhulumiwa" kama Qur'an inavyoagiza (Qur'an 2:279). Wakati wote wa Kampeni za Uchaguzi, msimamo wa Maaskofu kutoka takriban Makanisa yote ya Kikristo nchini ulikuwa ni kuunga mkono Mgombea Urais wa Chadema na wagombea wengine wa chama hicho nchi nzima. Makanisa yakatumika kumnadi mgombea huyo kama Waraka wao wa Kichungaji ulivyoelekeza wazi kwa kusema;- "Mungu anakuhitaji, haya si maneno tu, bali ni uamuzi wa makusudi wa Mungu anayetukabidhi wajibu huu. Kutopokea mwaliko huu unaotoka kwa Mungu ni kushindwa kutimiza wajibu wetu, ni dhambi ya kutotimiza wajibu wa wito wetu wa kikristo. Wito wa kutimiza wajibu wa Kijamii, ambao ni kutia chachu ya tunu za Injili na Mafundisho ya Kristo katika masuala na shughuli za kijamii, kiuchumi na kisiasa ya taifa letu". (Tazama: Mpango wa Kuhamasisha Huduma ya Kichungaji Katika Jamii Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010, Uk. 2). Kwa kuwa Padri Slaa aliamini kwamba yeye ni chaguo la Kanisa, alijiridhisha yeye binafsi, wafuasi wake, viongozi wenzake wa Chadema na Maaskofu kuwa lazima atashinda na akasema wazi kuwa hatokubali matokeo mengine yoyote kinyume na ushindi wake kwani wakristo walishaambiwa kuwa kutokutekeleza waraka wa Maaskofu ni dhambi. Ni muumini gani ataambiwa na viongozi wa dini yake kuwa kutokufanya jambo fulani ni dhambi kisha asilifanye? Mfano hai, huko Sumbawanga, Kanisa Katoliki liliwatenga waumini wake kwa kile lilichodai kwenda kinyume na maelekezo ya Kanisa kuhusu wagombea wa chama gani wapigiwe kura. Hali hiyo imepelekea Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Kayanza Pinda kuwaomba radhi Maaskofu kwa niaba ya Serikali na Chama chake kwa kile alichodai "kuwaudhi Maaskofu hao wakati wa Kampeni za Uchaguzi"! Hatimaye tarehe 31 Oktoba, 2010, taifa lilifanya Uchaguzi Mkuu na tarehe 5 Novemba, 2010, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikamtangaza Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mshindi wa kiti cha Urais na akaapishwa tarehe 6 Novemba, 2010. Wagombea wote wa kiti cha Urais walikubali matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi isipokuwa Padri Wilbrod Slaa wa Chadema na chama chake waliyakataa matokeo hayo na hata siku ya kutangazwa na siku ya kuapishwa Rais si yeye Padri Slaa wala viongozi wengine wa Chama chake cha Chadema aliyeshiriki. Hata siku ya Rais Kikwete kuzindua Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, wabunge wote wa Chadema walitoka nje ya Ukumbi wa Bunge kuonesha kuwa hawamtambui Rais aliyetangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Baada ya kuona kuwa mpango wao wa kushika madaraka kupitia mgongo wa Chadema umeangukia patupu, Maaskofu na chama wanachokiunga mkono wakaamua kuhakikisha kuwa nchi haitawaliki. Tunachoshuhudia sasa ni kutolewa kauli mbali mbali dhidi ya Uongozi uliko madarakani hata kwa mambo ambayo hayakufanywa na uongozi huu uliopo sasa bali yalifanywa na awamu zilizotangulia. Kwa mfano, mikataba mibovu ya migodi ya madini inayolalamikiwa ilifanywa wakati wa awamu ya Mkapa, Kuuzwa mashirika ya umma kwa bei za kutupwa kulifanywa wakati huo huo wa Mkapa, kuuzwa kwa nyumba za serikali katika maeneo ya serikali kwa bei ya kutupwa kiasi kwamba baadhi ya viongozi wa serikali hivi sasa wanaishi nyumba za wageni (guest house) kulifanywa wakati wa Mkapa. Aidha, uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu, Kufukiwa wachimba dhahabu Bulyankulu, mauaji ya raia wasio na hatia – Mwembechai, Zanzibar, Pemba, Morogoro, ufisadi na rushwa, Kuvunjwa maadili ya Uongozi, Kashfa za EPA, Meremeta, Kagoda, Net Group Solutions yote hayo hayakufanyika katika awamu hii bali wakati wa awamu ya Mkapa. Wakati wa awamu ya Mkapa, hatukusikia Maaskofu wakijitokeza kuyakemea haya wala kulaani mauaji ya raia wasio na hatia kama wafanyavyo hivi sasa ila wamekuwa mbogo wakati wa Uongozi huu kama walivyokuwa mbogo wakati wa awamu ya pili ya Mzee Mwinyi. Kinachowasukuma si kingine bali kuogopa ile waliyoiita "dhambi" ya kutokutekeleza wito wao wa Kichungaji wa kuhakikisha kuwa "Tunu za Injili na Mafundisho ya Kristo vinaonekana katika masuala na shughuli za kijamii, kiuchumi na kisiasa za taifa". Laiti isingekuwa hivyo, basi wangesimamia uadilifu wa kukemea maovu katika jamii wakati wote. Aidha, kwa kuona kuwa mawakala wao wameshindwa kushika nafasi walizoamini kuwa ni haki yao, Maaskofu na chama wanachokiunga mkono hivi sasa wamehamishia juhudi zao zote kudai katiba mpya ya Tanzania kwa nguvu zote (By all means possible) ikiwemo hata kumwaga damu. Mmoja wa viongozi wa juu wa Chadema, Mabere Marando, amesikika akisema wazi katika Mdahalo wa Katiba Mpya Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu Dar es Salaam siku ya Jumamosi tarehe 15 Januari, 2011 kuwa "Damu iliyomwagika Arusha ndiyo wino wa kuandika dibaji ya Katiba Mpya Tanzania". Watu waliotayari kumwaga damu za watanzania kwa malengo ya kisiasa na kudai katiba mpya ni hatari kwa amani na usalama wa nchi yetu kwa sababu katiba huandikwa kwa wino wa kalamu wala si kwa damu ya raia. Hii inaonesha mwelekeo wa hatari wa kundi hili la Maaskofu na wanasiasa kwa amani na usalama wa Taifa letu. Katiba ya nchi haiwezi kuandikwa kwa damu ya watanzania. Aidha katiba ya nchi haiwezi kuundwa katika mazingira ya vurugu, fujo, uasi kwa viongozi, dharau, kibri, uchu wa madaraka na ubinafsi. Katiba itakayoundwa katika mazingira haya, haitokuwa kwa maslahi ya taifa bali kwa maslahi ya Kanisa. Hatari nyingine kubwa inayolinyemelea taifa letu, ni ile ya viongozi wa Chama kilichopo madarakani na wale wa serikali kupingana kauli katika mambo ambayo wangepaswa kuwa na kauli moja (Collective responsibility). Mwenendo huu unatishia mustakbali wa nchi yetu kwa sababu utawala uliogawanyika hauwezi kutekeleza majukumu yake kwa raia wake, na ndivyo Maaskofu wanavyotaka iwe. Rais mmoja wa Marekani alipata kusema "A house divided can not stand by itself"-yaani nyumba iliyogawanyika haiwezi kusimama yenyewe. Tunaamini kwamba kugawanyika huku kwa Mawaziri wa serikali iliyopo madarakani ni kazi ya kundi hili hili la Maaskofu na mawakala wao katika Chama tawala na Serikali. TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU JIJINI MWANZA. Kwa vile, Baadhi ya Maaskofu wamejitokeza wazi wazi kuupinga uongozi uliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati walikuwa kimya kipindi chote cha awamu ya tatu, Na kwa vile, mwelekeo na kauli za Maaskofu hao vinapelekea kuiyumbisha nchi ili isitawalike wapate kudai kuwa Rais aliye madarakani hafai bali chaguo lao Padri Slaa ndiye anayefaa, Na kwa vile, tayari madhara ya mwelekeo huu yameshajitokeza huko Arusha kwa kuuawa watu katika vurugu zilizotokana na uchu wa madaraka ya Umeya wa Jiji hilo na kuchangiwa na kauli za Maaskofu kutomkubali Meya huyo, Na kwa vile, waislamu ni watu wapenda amani, haki na usawa kwa watu wote bila kujali rangi, jinsia, kabila, dini wala itikadi za kisiasa, Na kwa kuwa, kuna kila dalili ya kutoweka kwa amani kupitia kauli na vitendo vya Maaskofu kuunga mkono Chama maalum cha siasa, Na kwa kuwa, baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Rais Kikwete wameonesha wazi kuipinga Serikali yake, Sisi waislamu wa Jiji la Mwanza tunatamka yafuatayo;- 1. Tunaunga mkono mia kwa mia yote yaliyoandikwa katika tamko la Waislamu lililotolewa Diamond Jubilee Dar es Salaam siku ya Jumamosi tarehe 15 Januari, 2011. 2. Maaskofu kuunga mkono Chama kinachopinga matokeo ya Urais ni kitendo cha Uhaini, U-dini na ni hatari kwa mustakbali wa Taifa letu. Hali kadhalika ni kukiuka hata maandiko ya Biblia yao wenyewe yasemayo "Heri walio wapatanishi kwa maana wataitwa wana wa Mungu. ( Mathayo: 5 msitari wa 9 ). Tulitaraji viongozi wa dini, Maaskofu wakiwepo, wawe wapatanishi pale wanasiasa wanapogombana. Inapokuwa wao ndiyo sehemu ya ugomvi huo ni nani atawapatanisha wana siasa? Kama Maaskofu wamekuwa wagomvi, watakuwa wana wa nani kama si wa Shetani? 3. Tunawaonya Maaskofu waache kuivuruga Serikali kwa matamshi yao yaliyojaa chuki za U-dini kwani watapelekea amani ya nchi hii kuvurugika kama walivyochangia mauaji ya Kimbari ya Rwanda mwaka 1994. 4. Kwa kuwa Kauli za Maaskofu huko Arusha kutomtambua Meya aliyechaguliwa kwa kufuata taratibu zote za kisheria, zilichangia kuuawa kwa watanzania wasio na hatia, tunaitaka Serikali kuwafikisha Mahakamani Maaskofu wote waliotoa kauli hizo za uchochezi. Hakuna mtu aliye juu ya sheria. Kama Masheikh hufukishwa Mahakamani na wengine hata kuswekwa kizuizini bila kupelekwa mahakamani, Mfano Al Marhum Sheikh Al Amin Abdallah wa hapa Mwanza na Masheikh wengine mwaka 1964 na wengine kuswekwa ndani kwa kesi za kubumba, Maaskofu wametenda kosa hili la uchochezi wazi wazi hivyo kwa nini sheria isichukue mkondo wake dhidi yao? 5. Kama uchu wa madaraka ya Umeya wa Jiji la Arusha tu umesababisha maisha ya watanzania watatu kupotea, damu za wengi kumwagika na mali kuharibiwa pamoja na kusimamisha shughuli za kiuchumi katika Jiji hilo la kitalii, hali itakuwaje kwa uchu wa kutaka kiti cha Urais? Ni watanzania wangapi watapoteza maisha yao na damu za watanzania wangapi zitamwagika ili Padri Slaa aingie Ikulu? Wakati wa ziara ya Papa Yohana Paulo wa Pili nchini Tanzania mwaka 1990, Kanisa Katoliki lilimtaarifu kuwa linayo Tume ya Majeshi. Hivi jeuri hii ya Maaskofu ni kwa kuwa wanayo hiyo tume ya majeshi? Hata kama wanayo hiyo tume ya majeshi, sisi waislamu kamwe hatuiogopi kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema: 4óOßgtRöqt±ørBr& 4 ª!$$sù ,ymr& br& çnöqt±ørB bÎ) OçFZä. úüÏZÏB÷sB ÇÊÌÈ "Je, mnawaogopa? Basi Allah anastahiki zaidi ninyi kumuogopa ikiwa mu-waumini wa kweli" (Qur'an 9 : 13). Pamoja na hayo, tunarudia kuitaka Serikali kuueleza umma wa watanzania tume ya majeshi ya Kanisa ni ya nini? Au hawayaamini majeshi yetu ya ulinzi na usalama? 7. Waislamu tunamtaka Rais Kikwete awawajibishe mara moja Mawaziri wote wanaoipinga Serikali yake kama Mwalimu Nyerere alivyomfanya Kambona alipopinga sera ya Utaifishaji ya serikali yake mwaka 1967. Tunamtaka Rais asiwaonee haya hata kidogo Mawaziri hawa wanaoipinga Serikali yake kwani waswahili husema "Mchelea mwana kulia, hulia mwenyewe" na "Mchelea mwiba, mguu huota tende". 8. Baadhi ya vyombo vya habari vimechangia sana kuzorotesha hali ya amani nchini kwa kuandika au kutangaza habari za uchochezi na hivyo kupelekea kuvunjika kwa amani. Tunavitaka vyombo hivyo vya habari kuacha mara moja kushabikia U-dini na vitende haki. Vinginevyo waislamu tutavitangaza hadharani na kuwahimiza waislamu wasivinunue, kusikiliza au kuvipa matangazo. Tukumbuke pia kuwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalichangiwa sana na vyombo vya habari. 9. Vyombo vya dola navyo, Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Jeshi la Wananchi vitende haki kwa kufanya kazi zao kwa uadilifu, kwa ukweli na uzalendo na kutokupendelea Chama au kundi jamii fulani kwani kwa kufanya hivyo vitasababisha kutoweka kwa amani nchini. Kwa mfano, inapokuwa jambo linahusu Masheikh au waislamu, vyombo hivyo, husuusan Jeshi la Polisi, huwa na ujasiri wa kuwapiga na kuwasweka ndani waislamu lakini ujasiri huo hatuuoni kwa Maaskofu na viongozi wengine wa Kikristo wanapovunja sheria. 10. Kwa wanasiasa na wanaharakati wa mashirika ya kijamii, tunawataka waache kutoa kauli za uchochezi na vurugu kwani amani itakapotoweka hakutakuwa na wanachama wa kuwaongoza. Tumieni busara zenu kujadili mambo kwa hoja na msiporidhika pelekeni malalamiko yenu Mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. 11. Waislamu tunaunga mkono tamko la Rais Jakaya Kikwete kuhusu kuundwa kwa Katiba mpya. Pamoja na hayo, kwa mwenendo wa Maaskofu na Chama chao wanachokiunga mkono, tunamtahadharisha Rais kwamba amebeba dhamana kubwa ya usalama wa watanzania wote hivyo asisite kuwachukulia hatua wale wote watakaotaka kutumia mjadala wa katiba mpya kwa njia zitakazohatarisha amani au kudhoofisha Serikali. 12. Kwa kuwa mchakato wa Katiba mpya ndiyo kwanza unaanza, waislamu tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwani sasa kupitia Katiba mpya tutadai haki zetu zote ikiwemo ya Mahakama ya Kadhi kuwepo katika katiba kama ilivyo nchini Kenya, Nigeria, Ethiopia, Gambia, Zanzibar na hata Uganda. 13. Tunataka Katiba mpya itamke wazi kuwa Tanzania inaamini kuwepo kwa Mungu Muumba, serikali haina dini ila wananchi wake ndio wana dini mbali mbali. Katiba ya sasa haitambui kuwepo kwa Mwenyezi Mungu jambo ambalo linaifanya Tanzania kuwa nchi ya Kikafiri. Katiba za nchi nyingi duniani zimetamka kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na hata baadhi kusema wazi "In God We Trust" – Tunategemea kwa Mungu. Kama hatuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu kwa nini watu huapishwa Mahakamani? Kwa viongozi, kwa nini waapishwe kwa kutumia vitabu vya dini, Ikulu na Bungeni na kwa nini kuwepo dua ya kuliombea Bunge? Ni Mungu gani huyo anayeombwa hapo? 14. Tunataka Katiba mpya ya Tanzania iweke mgawanyo wa madaraka kwa uadilifu kwa kutamka wazi kuwa Rais akiwa Muislamu, Waziri Mkuu awe Mkristo na Rais akiwa Mkristo, Waziri Mkuu awe Muislamu kama ilivyo Nigeria na Lebanon ili kuepuka U-dini. Na vivyo hivyo kwa ngazi zote za madaraka mgawanyo uwe nusu kwa nusu. 15. Tunataka iundwe Wizara Maalumu ya Mambo ya dini ili ishughulikie masuala ya dini kuliko kuyaacha kama yalivyo sasa hayana Wizara inayoyashughulikia. Kama mambo ya kipuuzi tu kama vile muziki na maagizo yana Wizara maalum, vipi dini zisiwe na Wizara yao? 16. Tunataka Katiba mpya isiruhusu Serikali kuingia Mkataba wa upendeleo na kundi jamii moja kama ilivyofanya kupitia Makubaliano ya Maridhiano na Makanisa ya Kikristo mwaka 1992, makubaliano ambayo yanatekeleza andiko la Bibilia "Mwenye nacho ataongezewa na asiyekuwa nacho atanyang'anywa hata kile kidogo alicho nacho"(Luka 8 msitari wa 18). Wakristo walikuwa na shule, hospitali, Vyuo vya Ualimu, Vyuo Vikuu n.k huku waislamu wakiwa hawana kitu. Badala ya kupewa Waislamu wasiokuwa na rasilimali hizo wakapewa Wakristo na hivi sasa wanaongezewa kupitia Makubaliano ya Maridhiano kati yao na Serikali. 17. Kwa kuzingatia tamko namba 16 hapo juu, tunaitaka Serikali iache mara moja kutekeleza Maridhiano hayo batili kati ya Serikali na Makanisa na pia ituambie hadi sasa imeshayapa Makanisa ya Kikristo Mabilioni mangapi tangu mwaka 1992? Aidha tunataka watendaji wote wa serikali waliohusika kuandaa na kupitisha Maridhiano hayo ya U-dini wachukuliwe hatua za kisheria kwani huu nao ni ufisadi kama ule wa EPA, Kagoda, Meremeta, Dowans n.k. 18. Sambamba na hilo, tunaitaka Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikabidhi kwa waislamu Shule ya Msingi Mbugani (Muslim School) mara moja kama alivyoagiza Rais Mkapa miaka kumi na tano iliyopita. Hali kadhalika tunaitaka Serikali irejeshe shule zote zilizokuwa Muslim Schools ambazo zilitaifishwa wakati waislamu walikuwa na shule chache kulinganisha na Wakristo waliokuwa wakipata misaada kutoka serikali ya Kikoloni na sasa kupitia Makubaliano ya Maridhiano na Serikali tuliyoyaeleza hapo juu. 19. Tunataka Katiba Mpya itamke wazi kuwa Siku ya Ijumaa nayo ni siku ya mapumziko ili waislamu nao waweze kwenda kusali sala ya Ijumaa kwa utulivu pasina kuhofia kufukuzwa kazi au kukosa masomo kama ilivyo sasa ambapo kwenda kusali ijumaa ni fadhila tu. Kama hilo halikubaliki, basi siku zote tatu Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ziwe siku za kufanya kazi nusu siku ili sote tuwe sawa. Mkao wa sasa wa mapumziko Jumamosi na Jumapili unaonesha kuwa nchi hii ni ya Kikristo. 20. Tunataka wimbo wa Taifa uliopo ufutiliwe kwa mbali kwani unaonesha wazi Tanzania ni nchi ya Kikristo kwa sababu hakuna asiyejua historia ya wimbo huo kuwa ulianzia Kanisani huko Soweto Afrika ya Kusini. Kwa Kizulu wimbo huo unaitwa "Nkosi Sikeleli Afrika". Pia hakuna asiyejua kuwa upo katika kitabu kiitwacho "Chuo Kidogo cha sala na Maombi cha Kanisa Katoliki". Hata Mashahidi wa Yehova huko Mbeya waliwahi kuukataa. 21. Tunataka Katiba Mpya itamke wazi kuwa Rais akitoka Bara, Raisi wa awamu nyingine atoke Zanzibar ili kuwatendea haki Wazanzibari. Tayari hivi sasa, Tanzania bara imeshatoa Marais mara tatu, Mwalimu Nyerere, Rais Mkapa na Rais Kikwete. Ni Rais Mwinyi tu ndiye aliyetoka Zanzibar kwa hiyo Rais ajaye lazima atoke Zanzibar kutoka chama chochote kile kiwacho. 22. Tunamtaka Rais Kikwete aongoze mchakato wa kuleta Katiba mpya kwa amani, haki, ujasiri, bila woga wala upendeleo wowote. Katu asiruhusu dharau kutoka kwa kiongozi yeyote awe wa kisiasa ndani au nje ya Serikali yake au hata kiongozi wa kidini. Na pale atakapoona mazingira ya nchi hayapo katika utulivu na amani, ni kheri ausitishe mchakato wa Katiba mpya kwani Katiba haiandaliwi katika mazingira ya vurugu, chuki na uhasama kama tuliyo nayo hivi sasa. HITIMISHO: Nchi hii ni ya Watanzania wote. Hakuna aliye na haki zaidi ya mwingine. Kama taifa, watanzania tunafanana na watu walio katika merikebu. Hivyo tunapomuona mmoja wetu anataka kuitoboa merikebu yetu, hatupaswi kumwangalia tu atimize azma yake kwani akifanikiwa tutaangamia sote. Tunawataka watanzania wote kwa makundi jamii yao, vyama vyao, dini zao na tabaka zao mbali mbali kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwanza. Aidha tunawataka Maaskofu kuheshimu imani za dini nyingine katika kutekeleza wito wao wa kichungaji. Si lazima umkandamize mwingine asiendelee ili wewe uendelee. Tukumbuke kuwa hakuna mahali pengine ambapo watanzania wanapategemea kuishi wao na vizazi vyao hivyo tuilinde nchi yetu kwa faida yetu na vizazi vijavyo. Kama ambavyo waislamu walimlinda Mwalimu Nyerere dhidi ya wakoloni na tukavumilia madhila yote tuliyofanyiwa ili kulinda na kudumisha amani, sasa tunasema wazi wazi kuwa hatutakuwa mhanga wa agenda za Maaskofu na Mfumo Kristo bali tutakuwa tayari kuitetea dini yetu kwa hali na mali. Waislamu kamwe si wachokozi. Lakini hapa tulipofikishwa na Mfumo Kristo, tunapenda Maaskofu na mwingine yeyote yule aelewe wazi kuwa waislamu nchini Tanzania hivi sasa tuko tayari kufa kuliko kuishi huku tukiiona dini yetu ikidhalilishwa kwani hatuna cha kupoteza- Kwetu ni mawili tu, ima Ushindi Dhidi ya Dhulma au Kuuwawa Tupate Pepo. Na Mwenyezi Mungu Ndiye Mjuzi na Muweza wa Yote. Wabillaahi Tawfiiq. Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi.
  mchanaji
 • Askofu KKKT katika tuhuma nzito   9 years 5 weeks ago
  hivi nashindwa kuelewa jinsi magazeti ya kitanzania yasivyo na kazi za muhimu za kufanya. mbona mambo mnayofuatilia ni ya binafsi sana???. tukianza na ninyi mnaolalamika askofu ana dhambi je mnaweza kujiuliza ninyi mna mambo mangapi mliyofanya na mnayoendelea kufanya ambayo ni kinyume na maadili????????? tuje wewe mwandishi wa habari ni nini wamekupa hao wambea ili uandike habari hii???? lakini pia wewe ni msafi kiasi gani mbele za Mungu na mbele za wanadamu mpaka umhukumu binadamu mwenzio???? nafasi za uongozi makanisani sasa hivi zinagombaniwa lakini wewe umeegemea upande mmoja, kama wewe ni mtoa habari za kweli kwa nini waliokueleza hawapo tayari kutajwa?? na kwa nini hukuonana na Askofu Malasusa ili uandike kitu kamili, and what is special with iringa lutheran diocese mbona tumesikia padri kabaka morogoro na hamuoni kama ni issue au je kuna watu mnawapigia debe kwenye nafasi ya uaskofu iringa?????
  Mendela
 • Ayi, ayi, ayi, CCM   9 years 5 weeks ago
  Nape unaona mambo yanavyokwenda? Mubarak, Saddam Hussein, Gaddafi, walifanya hivohivo na Museveni alitaka kufanya hivyo kwa kumtayarisha mwanaye lakini sasa kasoma nyakati!
  rich
 • Askofu KKKT katika tuhuma nzito   9 years 5 weeks ago
  Tuhuma nzima inashangaza, inasikitisha kuona kiongozi wa kanisa katika ngazi ya juu namna hii, akionyesha kukengeuka kwa kiasi cha juu namna hii. Kwanza kabisa ukisoma habari hapo juu ni majibu anayotoa katika mahojiano, ni vigumu sana kuamini kuwa huyu ni kiongozi wa kiroho, anaegemea sana kuwa mafia. Nimejaribu kugoogle profile yake, nabakia na maswali mengi, sifahamu anaelimu kiasi gani, maana hekima yake na jinsi anavyojielezea anaelekea kuwa kama mafia, na si kiongozi wa kiroho. Maneno kama "kufanyizia", "nakwambia hakuna wa kuning'oa" si maneno ya mtu yeyote mwenye akili timamu ambaye ni kiongozi wa kanisa. I think he is a terrible case, he has absolutely lost credibility among his flock and I think the only good thing he would do for the body of Christ is to step down as a leader. He has become so good in his mind, and that is a dangerous spot to be as a leader. Because as Christians that reminds us of one being who became so good and even desired the position of his master, Lucifer. I am not calling this guy satan, no, i am not in position to do that, but the spirit of evil is crouching on him, and he has a chance to do good, he is not all lost, but it will take for him to humble himself, and behave Christ like. It is appalling to see a person deeming himself innocent but shunning the investigation, that raises a lot of questions. The sad part is that an individual has so much power that no one can do anything about his misconducts. This is not Christian like, how does a church as a standard bearer teach the society about responsibility if the spiritual leader cannot take responsibility himself? I hope someone within the church stands up to this? I feel sorry for the church that it could be dragged into this madness. It makes me wonder, how as a church do we elect these leaders? what are the standards? because the Bishop seem not to have adopted these types of excesses instantaneously, it seems to me at least that he had potential to culminate to what he has become . But the bottom line is we think clearly this man has lost his credibility according to the holly book: Here is What the book of 1Timothy 3:1-7, Above Reproach - An accusation of sin won't stick to him. Husband of One Wife - He must be faithful to his wife. He adores his wife and doesn't flirt with other women. Self-Control - He is the master of his behavior. His behavior doesn't control him. Lives Wisely - He makes good choices. Has a Good Reputation - People at church and in the community think highly of him. He is respected. Hospitable - His home is open to others. He Can Teach - He has gifted insight into the scripture and communicates well those insights to others. Not Addicted to Wine - He never gets drunk or over-indulges in alcohol. Not Violent - He resolves conflict peacefully. Gentle - His manner and words are not abrasive ...he has a good "bed side manner." Loves Peace - Is someone who works toward peace in every relationship he encounters. Does Not Love Money - He is not consumed with his retirement fund or the price of gas. Manages His Home Well - His family and home are in order, not in chaos. His children are polite and respectful. His finances are in order. Not a New Christian - He has proven experience as a faithful follower of Jesus. With these i think this man has nothing remaining for him to hang on the power, but again time will tell.
  pburettajr
 • Tango: TRA wamenihujumu   9 years 5 weeks ago
  Nadhani kauli ya kwamba "Kila mtu ufanyalo hulipwa", lina hashiria hukumu zaidi ya tafakari. Ni ukweli unafohamika kuwa wanadamu wengi huwa hatupendi watu wanapofanikiwa, hisia za kwanza kabisa mtu akifanikiwa ni kwamba alitenda mambo mabaya, kwa hiyo mabaya makimsimbu uwa hakuna mtu wa kumhurumia kwani fikira zetu ni kuwa analipizwa ubaya. Huu nauita wivu na kutokukomaa kiakili. Kama kuna mtu ambaye kazi yake ni kulipa watu ubaya kwa mabaya waliyoyatenda katika maisha yao, basi mtu huyu kama ni Mungu He must be the most unfair being, He must be so impartial that it makes no sense to believe in Him. Lakini, la hasha Mungu hayuko hivyo nitamtetea kwa hilo. Verani naamini hana dhambi nyingi kuliko mimi na wewe tunaonyoosha vidole vya hukumu, Verani ni victim wa system mbovu ambayo inawafanya mamilioni ya watanzania kuishi below poverty line. Na kuanguka kwa Verani hakusaidii maisha ya mtu yeyote yule mimi na wewe mtoa hukumu kuwa rahisi, alifanya kazi kwa bidii, ni mtanzania mwenzetu ambaye hakuficha pesa za misaada au EPA katika mabenki ya nje, aliitumia system an akatajirika, bila elimu wala nini. He is a true Entrepreneur, lakini system ni mbovu. Labda hakutaka kuwapa kitu kidogo wat TRA, watu wangapi wanadaiwa mabilioni lakini hawafuatwi, iweje Tshs. million tano, ambayo hata lori moja tu linge tosha ilete shida ya namna hii. Elewa kuwa bado tuko nyuma sana, zaidi ya watu 60 wamepoteza ajira kwa upuuzi kama huu, na mtu yuko hapa anadai , oh malipo duniani. Angalau aliunda kazi, ingekuwa kama marekani ninapoishi, mtu kama huyu serikali ingetafuta jinsi ya kuresolve shida bila ku halt hizi operations, lakini waafrika ujinga umetujalia hata hatuelewi consequences za hatua zetu. Kwa hiyo tumuonee huruma Verani, na watu waliopoteza ajira zao kwa ujinga wa TRA, in the end you benefit nothing by pointing your fingers, because we are not any better than Verani, we are all sinners and deserve a little bit of god's grace. These kind of mind set do not encourage innovation in our society, so if you think you are standing firm that you can judge some one, i say this not so fast sir, take a little inventory of yourself, do a little soul searching may be you will tune down your opinion a little bit down.
  pburettajr
 • Tango: TRA wamenihujumu   9 years 6 weeks ago
  Kila mtu ufanyalo hulipwa hapapa duniani.........Kumbuka Verani ulifanya nini kwa watu. Machozi ya watu.
  meku
 • Ukatili hujibiwa kwa sheria   9 years 6 weeks ago
  ifike mahala sasa sharia za inchi ya Tanzania ilinde raia wake, mambo makubwa huanzia udogo hivyo kama hilo limeonekana leo na nikwa mtu asiye na rungu kupigana, vp kesho kwa yule mwingine?. Maisha ya wa Tamzania hutegemea sana sheria walizo zitunga hivyo sharia hizo ziwalinde wote sawa.
  kibaso
 • Uongo wa Nape, Ridhiwani utamaduni wa CCM   9 years 6 weeks ago
  Ukombozi wa nafsi,roho na akili wahitajika kama sivyo tutakosa mwelekeo na nini hatima yake kama sio maangamizi makubwa yaliyopaliliwa kwa muda mrefu.Kumbuka Unaweza kusema uongo lakini si wakati wote. Waweza kuwadanganya wengi lakini si watu wote.Ipo siku,ukweli na uongo havitakubali kukaa pamoja tena na siku hiyo haiko mbali, kwani hakuna marefu yasiyo kuwa na mwisho na njia ya mwongo siyo ndefu. Mtu mmoja hapo zamani aliwahi kunena kuwa dunia inatawaliwa na 4H tu. Yaani H-uruma,H-aya, H-ila na H-adaa. 2H zimeondaka na 2H zimebaki. H-uruma H-aya hakuna zimebaki H-ila na H-adaa. Una hiari ya kukubaliana na maneno haya au kutokukubaliana nayo kabisa. Binafsi najiuliza kwa nini wanadamu wanasema uongo? Kujitetea au woga? kutaka sifa? kwa watu gani. Kuwafurahisha watu? watu wepi hao na kwa nini? Nimewahi kusikia watu wakinena kwa kulinganisha(Comparison) kwamba "Heri mchawi kuliko mwongo" Kwanini iwe afadhali mchawi kuliko mwongo?
  4jml
 • Awamu nne, vioja vinne   9 years 7 weeks ago
  Muelekeo wa Taifa letu upo mikononi kwetu au mwao...?
  TASER
 • Kikwete kuitwa mahakamani   9 years 7 weeks ago
  Kesi ya Profesa Costa Ricky Mahalu, Watanzania yetu macho.
  Mwl. Mashare Constantine
 • CCM yafyata kwa mafisadi   9 years 7 weeks ago
  Barua ya Wazi kwa Mh Rais JK juu ya Vikwazo vya Elimu Tanzania Mimi ni mwalimu mzoefu wa miaka takribani 25,nimekuwa nikikerwa na vikwazo vinavyorudisha maendeleo ya elimu nyuma hapa nchini. Kwa kawaida wananchi wengi baadhi ya vikwazo wanavyovijua ni pamoja na upungufu wa walimu,uhaba wa majengo na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia, uwajibikaji mdogo wa baadhi ya walimu na wadau wengine muhimu,nk. Pamoja na vikwazo hivyo nakupongeza wewe na serikali yako kwa jitihada zilizokwisha fanyika ikiwa ni pamoja na kupeleka uendeshaji wa shule za sekondari TAMISEMI suala lililoondoa ukiritimba na urasimu uliokuwepo kabla. Mh JK, pamoja na hayo ziko sababu zingine zinazokwamisha elimu ambazo maafisa walioko wizara ya elimu hawakwambii ama kwa maksudi au malengo binafsi. Naomba nikuume sikio, nitataja sababu mbili tu. Ya kwanza ni mfumo mbovu wa uteuzi wa maafisaelimu ngazi mbalimbali ambao ndio wasimamizi wa elimu huko. Katika hili mazingira ya rushwa,udugu na urafiki ndiyo hutawala. Wafuatao ni maafisa wachache walioteuliwa kwa mfumo huo.1. H.Batinoluho ambaye ni afisa elimu Karagwe- aliwekwa na Bw Kagolo wa wizarani kwa lengo la kusimamia mashamba yake huko kijijini Karagwe,huyu tayari ana kesi mahakamani ya wizi wa fedha ya serikali, 2. G.Fabian aliwekwa katika nafasi na Bw Kagolo kuwa afisaelimu Bukoba- wilaya ambayo ni ya mwisho kitaaluma katika mkoa licha ya kuwepo mazingira mazuri 2. O.Rujuba ambaye ni afisa taaluma Ngara aliwekwa na Bw.Ndabise wa wizarani kwa lengo la kusimamia mashamba yake kijijini, licha ya kwamba alifeli mtihani wa dipoloma ya ualimu. 3. Elian Yowel- licha ya kwamba ana vyeti vya kughushi lakini aliwekwa katika nafasi ya uafisa sayansi kimu na kaka yake wa wizarani aitwaye Elia Kibga, 4. Afisa Elimu Rombo alihamishwa kinyemera ili kukimbia kesi ya wizi wa fedha ya serikali, sasa amerudishwa kujibu kesi. Mh JK hawa ni mfano tu lakini wako wengi nchi nzima. Je, tutafika? Ningependekeza uteuzi wa maafisa elimu pia upelekwe TAMISEMI na Maafisaelimu Mikoa wahusike katika mchakato kwani wao ndio wanajua utendajikazi wa maafisa walioko chini yao. Mh JK tatizo la pili ni mfumo wa baraza la mitihani unaoruhusu uvujaji wa mithani.Nampongeza Dkt Ndalichako na vijana wake, kwa jumla wanajitahidi lakini mfumo huo ni wa zamani sana , unahitaji marekebisho uli uweze kuhimili mzigo mkubwa wa watahiniwa waliopo sasa tofauti na zamani. Ningependekeza uanzishwaji wa kanda maalum za mitihani katika mikoa mbalimbali ili kuimarisha uratibu wa mitihani. Mh JK, nakusudia kuendelea kutoa maoni moja kwa moja kwako ili kuepuka upuuziaji wa taarifa na maoni ya wananchi unaofanywa na baadhi ya watendaji wako wakuu katika wizara ya elimu na mafunzoa ya ufundi. Mwl Mhoro Joseph, Morogoro
  mhoro joseph
 • CCM yafyata kwa mafisadi   9 years 8 weeks ago
  Lowasa unasubiri nini? Hivi unafikiri mzee wa kaya anampango na wewe au anavuta muda tu huku akikupa matumaini, ukweli ni kwamba wewe umeshika mpini kwa uhai wa chama mimi nakushauri toka hadharani maliza kazi ili tujue moja
  fredmlay
 • Mkapa kutinga kortini   9 years 9 weeks ago
  Tokea mwanzo wa sakata la Mahalu nilikuwa na shaka kama iliwezekanaje kufanya hujuma anayotuhumiwa nayo akiwa peke yake. Shaka zangu zilitokana na ukweli kwamba kulikuwa na "players' wengi katika urasimu wa ununuzi wa nyumba sasa iliwezekanaje yeye pekee awe muhusika katika kesi ile? Halafu ni kwa nini kesi ile ilikuwa ikisuasua? kumbe shaka zangu zilikuwa za kweli kwani kadiri siku zinavyoenda tunazidi kuona kwamba hakuwa peke yake. Ni dhahiri kwamba Balozi asingeweza kufanya anavyotuhumiwa bila ya kumshirikisha waziri wa mambo ya nje ambaye kwa wakati ule alikuwa Kikwete, na kwa ngazi fulani hata Rais. Kwa maana haiingii akilini kabisa kuona Rais makini kama Mkapa angeweza kuongopewa kirahisi namna ile! polepole ukweli unafichuka; naona kwamba wote, Mkapa na Kikwete walihusika! ndiyo maana sasa tunamsikia Mkapa akitetea ununuzi wa nyumba ile ati kufanywa kwa kufuata taratibu zote! Laiti tungekuwa na TAKUKURU huru kama wenzetu wa Ulaya, Marekani na Asia ambako vyombo kama hivyo viko huru na mara kadhaa tumesikia vikiwabana hata viongozi wa nchi hadi kujiuzulu! Tanzania pia tungegundua uvundo mkali unaofnikwa funikwa na viongozi mafisadi hawa.
  Nditu
 • Dk. Slaa amweka pabaya Kikwete   9 years 9 weeks ago
  Haya yote yanatokana na ukosefu wa maadili na pia kutokumwogopa Mungu.Nawaomba waislam watembelee www.islam.freeforums.org
  Kaka Mkuu
 • Dk. Slaa amweka pabaya Kikwete   9 years 9 weeks ago
  mm nasema kwamba hata huyo slaa pia anahitaji maslai yake binafsi hana uchungu kiasi hicho cha nchi hii tukimuweka ayatakuwa yale yale au mabaya zaidi viongozi wengi wamekaa kimaslai zaidi tuone mfano wa libya
  mwinula
 • Dk. Slaa amweka pabaya Kikwete   9 years 10 weeks ago
  hakuna jipya.....!!!!nyimbo na ngonjera zilezile....haja zaliwa mkpmbozi wa Tanzania.hata Slaa yuko kimaslahi zaidihakuna uzalendo zaidi ya visasi!!!1?
  SIEGFRIED
 • Kikwete, Lowassa wamekosana nini?   9 years 10 weeks ago
  WATANZANIA HASA BARA( TANGANYIKA) TUMEKUWA TUKIFUMBIA MACHO HAKI ZETU ZA KIMSINGI. NDIO MAANA AHADI ZA BARABARA NA HUDUMA NYINGINE ZA KIJAMII AMBAZO NI HAKI YETU TUNAONA KAMA FADHILA KUTOKA KWA WATAWALA. NA JAMII YETU ILIJENGEKA KWA MTINDO WA KUSIFIWA WEZI WAKUBWA. UTASIKIA JAMAA MJANJA KAPIGA KAJENGA GOROFA. NDIO MAANA WANZANZIBARI WANAONA NI BORA WAJIONDOE KWENYE MUUNGANO FEKI. NAAMINI ZANZIBAR WANGEKUWA KIVYAO WANGEKUWA MBALI SANA KIMAENDELEO HAYA MAGAMBA NA SUMU YANAWAGHARIMU. ANGALIA RWANDA, BURUNDI WAKIIGA RWANDA WATAKAA PAZURI NDANI YA MUDA MFUPI
  Mtanganyika
 • Dk. Slaa amweka pabaya Kikwete   9 years 10 weeks ago
  USHAURI KWA VYAMA VYA UPINZANI HASA CHADEMA! Mimi naumia sana kuona hakuna lolote la maana liliwatokea hawa mafisadi toka hizi kashfa zilipoanza kuibuliwa. Kutokana na hilo sasa CCM wanatumia mwanya huo kuiba HOJA za upinzani na kujinufaisha nazo. Mkumbuke ni watanzania wachache sana wenye uelewa mzuri na kuweza kupambanua mambo, nakutambua mbivu na mbichi. TUNAHITAJI ACTION sio kila siku kuwataja tu majukwaani HUO WIMBO UTAZOELEKA NA MTAONEKANA HAMNA JIPYA. Lazima tuende hatua nyingine. Japo bado tunahitaji watajwe ili tuache kuwaheshimu. Nape wewe ndiye unayetumika si Dr. Slaa. Kuondoa magamba ni rahisi kazi ngumu kuondoa SUMU. "MTI HAUKATWI MATAWI"
  Mtanganyika
 • Dk. Slaa amweka pabaya Kikwete   9 years 10 weeks ago
  Suala la kutolewa fedha za ruzuku kutokana na mtikisiko wa uchumi wa dunia ambao ulisababisha kuanguka kwa makampuni na baadhi ya vyama vya mazao ya biashara wahusika hasa kwenye zao la kahawa hawakutendewa haki. Hadi leo kuna baadhi ya vyama vya uzalishaji kahawa na wafanyabiashara kusini mwa tanzania wana matatizo kutokana kutopata ruzuku kulingana na makali ya tatizo. Ruzuku ilitolewa kukidhi madeni ya benki(CRDB) yaani wale wafanyabiashara walioshindwa kulipa madeni walisaidiwa kulipiwa madeni baada ya ukaguzi mkali ambao haukuwa sahihi sana kwa upande wa wafanyabiashara. Kama watu hawakutendewa haki kwa sababu ya UFISADI na TAMAA za wachache kuna kila sababu wahusika washitakiwe badala ya kila siku kuhubiri majukwaani. Mbona Mch. Christopher Mtikila ameshawahi kuishitaki SERIKALI mara nyingi tu. Kuanzia sasa CHADEMA na vyama vingine vya siasa kambi ya upinzani kama ushaidi hupo ni bora mkaenda mahakamani wananchi wazalendo tupo nyuma yenu.
  Mtanganyika
 • Tujifunze kutoka kwa Maria Nyerere   9 years 10 weeks ago
  Umesema kweli,kweli tupu,hii inaonesha namna gani Afrika hasa Tanzania,madaraka yanachukuliwa kama ni ya familia kitu ambacho si sahihi hata chembe,tuyakatae haya Tanzania.
  felix
 • Kikwete, Lowassa wamekosana nini?   9 years 10 weeks ago
  Kila lenye mwanzo lina mwisho wake, Mhhhhh!!!!!!!!! Yetu, macho, Ee Mungu atunusuru wasije wakatutumbukiza pabaya.
  WAGUMA