Recent comments


 • Siri za CCM, CUF zavuja   9 years 13 weeks ago
  kimtazamo wangu ni muda muaafaka wa kujiuliza kila mmoja wetu tumetoka wapi,nini kilichopelekea waasisi kupingana na wakoloni wa kizungu na kwa nini sasa hivi tuna wakoloni weusi?je katiba mpya itakuwa suluhisho ya matatizo yetu?je nchi wahisani wanamchango gani na matatizo ya ndani ya nchi?je vyombo vya kimataifa vya fedha vinachangia vipi kurudisha nyuma mipango ya maendeleo yetu?je kuna siri gani ambazo serikali na wadau wa dunia wanaingia ili kufilisi nchi?na la mwisho naomba katiba mpya iweke misingi ya msimamo wa nchi na watu wake katika kufanya maamuzi sahihi na si kuingiliwa na wahisani au na kundi dogo la wezi litakalo hodhi serikali kwa wizi wa rasimali.
  kamanda
 • Mabilioni yatengwa kumsafisha Lowassa   9 years 13 weeks ago
  Watanzania tuangalie viongozi bora na sio pesa walizo nazo TUWE MAKINI WATANZANIA WENZANGU NJAA ISITUPONZE!!!
  KANCHI
 • Furaha ya Rostam kuzimwa?   9 years 14 weeks ago
  Kweli serikali ya JK haina msimamo....
  fademark
 • Msilale, CCM hawajaanza kugombana leo   9 years 14 weeks ago
  Ahsante sana kwa historia nzuri. Naomba ufafanuzi zaidi, Oscar Kambona alikuwa bado nchini wakati wa Operesheni ya vijiji vya ujamaa?
  Fadhy Mtanga
 • Msilale, CCM hawajaanza kugombana leo   9 years 14 weeks ago
  Bwana Kamwaga, Asante kwa habari nzuri na yenye mtiririko mzuri wa historia ya migogoro na kusalimika kwa chama tawala (TANU kisha CCM) tangu kuanzishwa kwake. Nionavyo mimi, mazingira ya sasa ni tofauti na ya wakati ule, hasa ukizingatia uwepo wa siasa za mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini ulianzishwa mwaka 1992 na kukua kwa uhuru wa habari. Kwa pamoja, mambo haya yamepelekea kuongezeka kwa kwa uhuru na ujasiri wa kujieleza na uthubutu wa kutenda mambo miongoni mwa wananchi ambao haukuwepo wakati ule. Nikumbushe kwa ufupi tu, nikiwa mdogo, miaka ya sabini wakati wa enzi za mwalimu, nakumbuka tulipokuwa tunaongea au kurudia mambo ya nchi au viongozi tuliyoyasikia kwenye radio, mama alikuwa anakuja haraka na kutukanya kwa sauti ya chini kabisa kwa kusema,"nyie nyamazeni, mkisikiwa mtafichwa, marufuku kuongea hayo". Yaani wakati ule, ulitakiwa kukaa kimya, au kusema; na kama uliamua kusema, basi ulipaswa kusema mambo mema na yenye kusifia chama vinginevyo ondoka nchini. Ilikuwa ni kosa kupingana na Jeuri ya chama. Ni jambo lililo wazi kwamba, katika mazingira yale ya siasa za mfumo wa chama kimoja uliombatana na kujenga uoga na hofu ya hali ya juu kwa raia kuanzia ngazi ya familia mpaka kwa wawakilishi wao (wabunge) walioaminishwa kwamba, chama ni kikubwa kuliko Bunge, basi ilikuwa ni lazima wavuke salama migogoro iliyowakumba. Lakini, leo tunashuhudia Tanzania nyingine, yenye watu, taasisi, au mashirika ya kiraia wanaothubutu kukosoa au kumkosoa wazi wazi Rais wa nchi, chama tawala, serikali na taasisi zake kupitia vyombo vya habari, mikutano ya ndani au hadhara au maandamano. Pia, haishangazi kuona hata watoto wadogo wanamshabikia kiongozi wa upinzani kwa utashi wao wenyewe kabisa na hakuna wa kuwaonya nyamazeni nyie mtafichwa. Kwa kifupi, tuko katika wakati mwingine kabisa wa uhai wa taifa letu, siasa zake na uhuru wa raia kujieleza na kudai haki zao. Nikirejea kwenye baadhi ya mifano uliyotoa, nashawishika kuamini ni vigumu mambo yale kutokea wakati huu na CCM ibaki salama. Yalikuwa ni mawimbi mazito sana lakini chama tawala kilibebwa na mazingira ya wakati uliokuwepo. Mfano, ingekuwa wakati huu, nafikiri Kambona asingekimbilia Uingereza bali angejitoa kwenye chama na kuahamia upinzani kuendelea na madai yake. Hivyo hivyo ingekuwa kwa akina Kasela Bantu na wenzake saba, wangehamia upinzani kuendeleza mapambano yao wakiwa huko. Swali la kujiuliza hapa ni kwamba, je CCM ya sasa inaweza kuhimili wimbi la kuondokewa na katibu mkuu wake leo wa calibre ya Kambona (siyo Makamba). Je inaweza kuhimili wimbi la kuondokewa na wabunge jasiri nane (ambao kwa mawazo yangu ni zaidi ya akina Mwakyembe sasa maana kupingana na mwl na mfumo wa wakati ule ilibidi uwe jasiri kweli kweli)?? Ni wazi katika mazingira haya ya sasa ya uhuru na uthubutu wasingeondoka peke yao bali na wafuasi wao jambo ambalo sina hakika kama CCM ingeweza kuhimili wimbi hili kubwa. Pia, naamini, moja ya makundi yanayohasimiana ndani ya CCM; kundi la sitta au Rostam likiamua kujitoa kwenye chama leo, basi linaweza kuwa wimbi kubwa kwa chama kuliko ambavyo ingekuwa miaka ile ya mwl. Kwanza ingekuwa ni wakati ule, ni wazi kundi moja lingekuwa limeshatimuliwa. Lakini kwa kuzingatia wakati tuliopo, CCM imeamua kuyakumbatia makundi yote ingawa ni dhairi haipendezwi na kundi mojawapo au yote. Hii inatoa picha kwamba, pamoja na sababu nyingine nyingi, wimbi la kupasua chama linategemea wakati na asili yake kwa maana ya chanzo, ukubwa na uzito wake kuweza kuhimiliwa na chama Kwa upande mmoja, nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa kwamba, wapinzani hawapaswi kulala katika swala zima la ujenzi wa vyama vyao wakiamini au kuvizia CCM itapasuka kwa migogoro na wao kuchukua dola kirahisi. Nafikiri, kuvizia tu, siyo approach nzuri, inabidi wavizie na kufanya kazi kweli kweli. Lakini kwa upande mwingine, sikubaliani na wewe kwa kiasi fulani kwamba, historia itaendelea kuilinda CCM isipasuke kutoakana na migogoro, kwani mazingira ya wakati tuliopo ni tofauti na ya wakati ule wa chama kimoja, ambapo sehemu kubwa ya hoja yako imejengwa. Ni vizuri kuitazama historia, lakini naona kama mazingira yaliyokibeba CCM wakati wa mawimbi yale hayapo tena sasa. Kama nilivyosema wimbi la kupasua chama (au mageuzi) linategemea wakati na asili yake, basi naona hali halis inaonyesha kama wakati umeshawadia ila bado wimbi stahili tu ambalo linaweza kuja muda wowote kama wataendelea kutengeneza migogoro. Ebu tujikumbushe na kilichokuwa chama tawala kwa miongo mingi kule Kenya, KANU. Chama hiki kilivuka vikwazo vingi mpaka kufikia hatua Rais wa wakati huo Daniel Arap Moi kuitwa Profesa wa siasa kwa uwezo wake wa kukivusha chama salama kwenye misukosuko. Lakini kwa kutotambua au kuupuza alama za nyakati au kutekwa na historia ya kuvuka salama migogoro, Moi alitengeneza wimbi la mgogoro liliopelekea KANU kushindwa vibaya katika uchaguzi, kupoteza dola na kupotea kabisa katika siasa za ushindani za Kenya. Hakukuwa na kichaka cha historia cha kuwasitiri, wimbi lilikuja kwa wakati wake na wakazolewa, basi. Naamini, CCM haina kinga ya asili (Natural immune) katika hili na kama wataendelea na migogoro,tena katika mazingira haya ya uhuru wa habari na wananchi kuanza kujua wajibu wa serikali kwao na haki zao za msingi, basi siku moja wanaweza kutengeneza wimbi zito ambalo litawazoa na katu historia haitawalinda. Dadisi. Naomba kuwasilisha, Asante na kazi njema
  Common mwananchi
 • Furaha ya Rostam kuzimwa?   9 years 14 weeks ago
  Tafadhali TANESCO silale. Hakikisheni haki inatendeka
  Papa
 • CCM ikivuliwa gamba itavuja sana   9 years 14 weeks ago
  Samahani Bwana Lukaza; japokuwa ulikuwa ukihitaji kujibiwa na Saed Kubenea, lakini pia naweza kukujibu kwa nilivyoelewa mimi. Ifahamike kwamba Mh. John Pombe Magufuli ni waziri aliyepewa dhamana ya kusimamia Ujenzi zikiwemo barabara. Kwa mujibu wa kiapo chake anatakiwa kutembea ndani ya reli za sheria na ndicho alichoapa sikuile ikulu, huku akishika Biblia kuashiria kumaanisha kwa imani yake. Sheria yetu inabainisha umbali stahili kwa ujenzi wa kando ya barabara na pia ujenzi huo uheshimu master plan ya mji. Sasa suala la ufisadi kwenye ardhi na mambo mengine Magufuli sio mhusika wake. Pia wale watakao bomolewa kwenye makazi yao halali watafidiwa na kiutaratibu serikali hutenga maeneo kabla ya kuwafidia ili wapatapo pesa zao wakajenge huko. Na hii si sheria ya Magufuli bali ni serikali ya CCM na magufuli anatakiwa kuitetea huku akihakikisha ilani ya chama zikiwemo ahadi za JK zikitekelezeka. Sina sababu ya kukukumbusha umuhimu wa barabara katika uchumi wa taifa na tunahitaji akina magufuli wengi ili mambo yaende. Hebu Lukaza nenda kule kwetu Ulanga kwa Kombani ukaone watu wanavyoteseka kwa usafiri. Wanasafiria mafuso huku wakikwepa matawi ya miti kama Ngedere. Je kungekuwa na barabara nzuri nani angesita kupeleka mabasi au Hiace? Kimbo ya mchele (= kilo moja na nusu) wakati wa mavuno huuzwa kati ya 300 na 500, fikiria mara mbili. Watu wanapewa umaskini kwa makusudi na watawala wa nchi hii. Usafiri ni shida na transaction cost au gharama za uendeshaji ni juu mno kutokana na kukosekana kwa barabara bora. Kama kikwete na Pinda wanaona sheria hiyo ni mbaya wanatakiwa kuandaa muswada wakaupeleke bungeni ili sharia hiyo irekebishwe kuliko kumfanyia majaribu mtu mwingine na kumpa amri mbele ya wapigakura wake. Pili suala la CCM kujivua gamba sio tatizo au kubadili rangi sio suluhisho. Kinyonga ni kinyonga tu hata awe mweusi au wa bluu. CCM inatakiwa kubadili tabia na kupata viongozi wenye dhamiri safi kwa taifa. Rejea hotuba ya mwalimu na historia ya muasia aliyetangaza kwamba serikali ya Nyerere iko mfukoni mwake; hapo utajua yupi ni kiongozi wa wanyonge na yupi ni mtawala wa wanyonge. Nduguyangu Lukaza tunapaswa kumwambia rais wetu kwamba he should not take Tanzanians for granted. A day will reach that even a lizard will turn to be a snake. God forbid. Who knew that KANU will turn to be an opposition party? Who knew that strong leaders like Ben Ali, Mubarrack and Gadafi will be in trouble today? time will tell and it never tell lies. Imeandikwa kwenye biblia kwamba; Aonywae mara nyingi akishupaza shingo yake atavunjika shingo na wala hatapata dawa. Ngoja tusubiri tuone. Ni mtazamo tu mzee.
  Lucas Mndewa
 • CCM ikivuliwa gamba itavuja sana   9 years 14 weeks ago
  kubenea, kwa mtazamo wang mimi naona bado kikwete amefanya vizuri coz hajasema kwamba barabara hazitajengwa ila muda ni muhim ili mambo ya msing yawe ymefanywa kwanza. Kwa mfano wananchi kupewa fidia hasa wale ambao barabara zimewafuata wao,hakuna mantiki kuwabomolea hawa thn wakaishi kwa shida kwa lengo la kupata mtaji wa siasa kwamba natimiza ahadi alizotoa wakati wa uchaguzi,kama nimekuelewa vizur bwana Kubenea ni kwamba unajaribu kusema kua kikwete ametoa agizo la kusimamisha bomoa bomoa kwa lengo la kujipendekeza kwa wananchi ili waone serekali inajali..hebu kua mkweli na nafsi yako kubenea katika kunijibu swali hili..'je usingeandika negative kweli kama serekali ingebomoa nyumba bila kulipa fidia na wananchi wakiwa kwny matatizo ya ukosefu wa makazi?'..mimi naamin hii ingekua mada kubwa sana kwenye gazeti hili na mengine mengi. Kuhusu suala la barabara zikianza kujengwa kabla miaka 3 baadae hazitamalizika kwa muda pia sioni mantiki hapa, kwanini..mzee wang kubenea 'NIA NJEMA HULIPWA' inatosha kabisa kujenga baada ya miaka 3 kutoka sasa kama kufanya hivyo ni kwa ajili ya manufaa ya wananchi.L a msing barabara zitajengwa na wananchi watakua wapo kwenye makazi mengine salama na fidia zao,inawezekana Kikwete ana kasoro lakini si kweli hata kidogo kua hana mazuri anayofanya na kwang mimi hili la kuzuia ubomoaji ili wananchi walipwe fidia ni mojawapo wa jambo zuri..masalam bin nuur
  lukanza
 • Sura mbili za matatizo ya walimu   9 years 14 weeks ago
  Kiukweli hali ni ngumu sana katika shule hizi tatizo kubwa ninaloliona ni ukaguzi mbovu unaofanyika katika shule hizi, kwani umekuwa ni ukaguzi wa maandishi2 na si reality inayokuwapo katika shule hizi.
  Budodi
 • Kweli Mkulo ameshiba, sasa anatukejeli   9 years 14 weeks ago
  Inasikitisha kusikia taarifa au matamko kama haya. Lakini tukumbuke hii ndiyo kawaida ya wanadamu. Nimemsikia mheshimiwa Sumaye akitoa mawaidha mazuri kwa CCM. Lakini alipokuwa amekalia kiti cha uwaziri mkuu, alikuwa na maneno ya aina gani? Mawaziri uliowataja wote wana majina yenye herufi zilizoanzia na M, sijui hii ndiyo imechangia?
  Barometer
 • Serikali inapokwenda kwa ‘Babu Loliondo’   9 years 14 weeks ago
  tunaamini mungu yupo pamoja nasi basi tutashinda na haya mahangaiko yote ya tanzania na kuhusu serikali kuingilia ni kwamba serikali yetu haiko imara yani viongozi wake ni wa kukurupuka kwenye mambo na kuhusu tiba katika vituo vyetu vya afya hapo napo ni tatizo kdgo by the way KWA IMANI TUNAPONA
  T-Wiiii
 • Zitto ana maslahi yapi NSSF?   9 years 14 weeks ago
  kubenea jaribu kuandika bila hisia mbaya kwa mtu..hii makala yako tayari inaonyesha unawaza nini juu ya zitto..mimi nadhan ungefuatilia kwanza thn ndio ungekuja na makala iliyokamilika juu ya nn maslah ya zitto NSSF.kwa hili me naweza kutabiri nini utakachoandika..lol. good luck bruv
  lukanza
 • Vijana CCM wamgeuka Kikwete   9 years 14 weeks ago
  CCM ni chama cha wafanyakazi na wakulima. Trend inaonyesha kuwa CCM kina viongozi wachache wanamdanganya Rais na chama kinaonekana sasa kama ni chama cha matajiri na wala rushwa na vijana wamejigawa kwenye makundi mawili, ni aibu kuona Bashe anatetea wale wote ambao wanahusishwa na ufisadi! hapo kuna jambo. Ridhiwan ndiye aliweza kutoa wazo mbadala na linalofaa, wengine wote kwenye secretariate wafukuzwe uanachama wa CCM.
  richard bura
 • ‘Dhahabu ya damu’ ya Bulyanhulu   9 years 14 weeks ago
  Hawa ndugu zetu waliofukiwa ipo siku damu zao zitalipwa.Serikali imekuwa Kama vile imewageuza raia ni kitegauchumi chao maana Sheria hazifuatwi kila kitu mvurugano.Wananchi wanahamishwa maeneo yao kwa usimamizi wa Polisi na kuwafukia raia live!!!!,na hakuna hata mmoja alieguswa na hilo.Maji yanayotiririka kutoka ktk baadhi ya migodi yana sumu picha na video za waathirika tuliona wote lakini hakuna hatua iliyochukuliwa zaidi ya Serikali kusema inakwenda kuyafanyia uchunguzi Kama yana chemical zinazoweza kumdhuru binaadamu,majibu hatujayasikia na Kama yalishatoka yamebaki kuwa siri Kama walivyozoea kuwa wasiri kwa mambo makubwa.Mungu yupo ni vile sina uwezo Ila nntamlilia Mungu awe refa juu ya Watz wenzetu waliofukiwa na magreda ya mgodi chini ya usimamizi wa Polisi.
  Bepari
 • Kweli Mkulo ameshiba, sasa anatukejeli   9 years 14 weeks ago
  me ninona hawa viongozi wanadhalilisha taaluma zao kwa kweli na ss wananchi tunafikra mgando za aman cjui pumba ka hzo ni za kutuambia sie wananchi kweli yan sehemu nyingne watu zaman washakinukisha bt simaanishi vita imean lazma awajibike lakin kwa bongo nadhani hakuna hko kipengele cha kuwajibishwa bs tu tunamshukuru mungu kwa kila jambo
  T-Wiiii
 • Rais mtarajiwa ni mzushi   9 years 15 weeks ago
  Mimi ni mtanzania nilisheherekea kupatikana kwa uhuru Tanganyika mwaka 1961, wakati huo nikiwa darasa la tatu! Nimekuwa nafuatiliaya matukio mengi ya wanasiasa lakini matukio haya ya serikali ya awamu ya nne yanatisha! ufisadi, rushwa, kutokuambiwa na ukweli na serikali, as a result kuna dalili zote zinaonyesha kuwa chama tawala kimekosa dira. Watoto wa wana CCM wameanza kuvuta bangi na kutumia cocaine. The would be new presedential asperants wanapashwa kusema ukweli ndiyo waweke misingi mizuri. Mafano, uv-ccm secretariate inabidi kujihuzulu waende for rehabilihation kwani sasa watoto wamefiakia hatua ya kutoa (orders) amri kwa wazazi badala ya kuomba ushauri kwa wazazi - hii ndiyo cocaine, bangi--hawafai kuwa kwenye uongozi wa cahma mpaka proved by medical doctor kuwa wamepona else miaka ijao tutapa serikali mbaya au upinzani utachukua kwa ulaini. Ndiyo ushauri wangu kwa ccm.
  richard bura
 • Mikataba ya Mwinyi, Kikwete kufilisi nchi   9 years 15 weeks ago
  NAOMBA HILI GAZETI LIHESHIMU CHAMA TAWALA.
  joshua
 • Mikataba ya Mwinyi, Kikwete kufilisi nchi   9 years 15 weeks ago
  Hivi bado CCM wanamtafuta mchawi anayetishia usalama wa serikali yao ya kinyang'au? Bado wanang'ang'ania kuendelea kututawala kwa kutubebesha mizigo ya misumari ya moto? Haiingii akilini kuona Marais wote baada ya Nyerere kuiingiza nchi kwenye mikataba ya kuinyonya, kuifilisi na kuiangamiza nchi kiasi hiki! CCM lazima iwajibike kwa hujuma iliyoifanyia nchi hii na vinara wote wa ufisadi huu wawajibishwe kisheria. Ni budi watanzania wote kwa pamoja kuamka na kupambana na vibaka hawa walioshika dola Kijanjajanja kwa kuchakachua ili kujihami dhidi ya umma wenye hasira. Wapo wapumbavu kadhaa kwa kutumiwa na vibakauchumi hawa wanaotaka kuyapotosha malengo yetu ya kuikomboa nchi hii kwa kusingizia udini. Hivi kuna udini gani hapa kama maovu yaliyofanywa na Mwinyi, Mkapa na huyu mhuni Kikwete yanaonekana waziwazi? Wamehujumu kila kilichoanzishwa na mwenzao wa awamu ya Kwanza Nyerere, wamegawa viwanda vyetu bure kwa matapeli waliouza mitambo na kugeuza majengo godowns za kutunzia mitumba ya nguo, baiskeli, scrapper na hata chupi toka ughaibuni, wameeuza hadi nyumba za serikali nyingine zikiwa zimejengwa kabla ya hata wao kuzaliwa! Na kama kwamba hiyo haitoshi wameiingiza nchi kwenye mikaataba ya kijinga, kipumbavu na ya kishenzi wanayonufaika nayo wao na vibaka wenzao. Wameliaibisha taifa kwa kuliingiza taifa kwenye mikataba ambayo hata kijana wa darasa la saba angesomewa kwa kutafsiriwa angeikataa, wametufanya kichekesho mbele ya uso wa dunia. Wananenepesha matumbo yao na nyuso zao kunawiri huku watanzania wengine wakizeeka kabla ya wakati kwa shida na suluba zinaazowakabili. CCM na uoza wao wote ni lazima waende. Shime jamani tuungane kuwaondoa hawa. Uwe mwislamu kama mimi, mhindu, Mkristo, muumin wa dini za asili na hatakama huna dini tuungane kuisimamisha hali hi angalau kwa faida ya kizazi chetu kijacho. Mungu aibariki nchi yetu.
  Nditu
 • Majeshi ya Gaddafi yafurusha waasi   9 years 15 weeks ago
  Mwandishi Baybah Wald Amhadi alisema gari la timu ya waandishi wa Al-Jazeera arab clothes lilishambuliwa kwa risasi kutokea nyuma wakati wanarudi kazini kusini mwa mji huo.
  haosai123
 • Dhahabu inapokuwa Karaha, Balaa na Matanga   9 years 15 weeks ago
  Hebu fikiri ndugu mwandishi, mgodi umo katika vijiji vya Mavota na Mkukwa. Vijiji vyote hivi vinatumia zahanati vêtement moja na shule moja ya msingi. Zahanati ina mganga mmoja na manesi wawili tu. Sasa dhahabu ina faida gani kwetu?”
  haosai123
 • Wananchi washtukia usombaji makaa ya mawe   9 years 15 weeks ago
  Hata katika vijiji vya Ngaka, Mbalawala na Mburuya, vilivyo eneo la machimbo, mjadala ni juu ya mkaa wa mawe “unavyosafirishwa wholesale nchi za nje” bila wananchi kushirikishwa wala kunufaika na lolote.
  haosai123
 • Babu wa Loliondo na ‘Kuomintang 2015’   9 years 15 weeks ago
  Nina uhakika pia kuwa nchi yetu itapata mapato makubwa kwa sababu magonjwa haya yameathiri watu wengi duniani. Kama dawa hiyo inaponya kweli, na serikali ndiyo electronics yenye kazi ya kuthibitisha hili, watu watatoka kote duniani kuja kuinunua.
  haosai123
 • Wanawapiga, wanawatia vidole makalioni   9 years 15 weeks ago
  Bakari anasema kutokana na eneo hilo kuwa na madini mengi, watu wamegoma kuondoka. Ndipo askari wa hifadhi hiyo walipoanza kuwatoa kwa nguvu ikiwa ni pamoja na kuwapora dhahabu walizopata na mali nyingine.
  haosai123
 • Dowans wasilipwe   9 years 22 weeks ago

  Laiti kama ningelikuwa na uwezo wa kuingia kwenye kichwa cha kila mtanzania na kumfanya aweze kuonja aza ninayoipata kutokana na uozo huu ningefanya hivyo. Jamani inaumiza sana. kwanini fedha zihamishwe kutoka mikononi mwa watanzania walio masikini na kuingizwa katika mifuko ya mafisadi? hivi tuna rais wa nchi au we have the walking corpse? Iam tired my fellow sons and daughters of this land. Why don't we wake up and fight for our dearly country and resources.

  patricwanga78
 • Dowans wasilipwe   9 years 22 weeks ago

  Laiti kama ningelikuwa na uwezo wa kuingia kwenye kichwa cha kila mtanzania na kumfanya aweze kuonja aza ninayoipata kutokana na uozo huu ningefanya hivyo. Jamani inaumiza sana. kwanini fedha zihamishwe kutoka mikononi mwa watanzania walio masikini na kuingizwa katika mifuko ya mafisadi? hivi tuna rais wa nchi au we have the walking corpse? Iam tired my fellow sons and daughters of this land. Why don't we wake up and fight for our dearly country and resources.

  patricwanga78