Dk. Ulimboka asimulia alivyochungulia kaburi


Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 18 July 2012

Printer-friendly version

HAYA ni masimulizi ya Dk. Steven Ulimoka, juu ya alivyotekwa na kuteswa kama yalivyochotwa kwenye mtandao wa intaneti wa U-Tube

Nakumbuka ilifika mahali nikawa natoka damu mdomoni, natoka damu kichwani; yaani natoka damu karibu kila mahali…

Eeh, yaani unajua, kwa muda kama siku tatu mfululizo, huyu bwana (Abeid) alikuwa anajaribu kuwasiliana na mimi lakini kwa bahati mbaya kwa ratiba yangu ilikuwa haiwezekani kumwona.

Nilishawahi kumwona zamani, kwenye mgogoro ule mwingine, lakini this time of course (mara hii) alikuwa serious (makini) akinitafuta akisema kwamba anataka some hearing (kupata maelezo) ili aweze kutoa ushauri.

Huyu bwana anafanya kazi ikulu. Aah, mimi namfahamu kutokana na incidence (matukio) za kwanza, sikuwa na muda. Lakini jana aka-insist (akang’ang’ania) sana na akakaa Hugo (hoteli) pale muda mrefu sana, sisi tulikuwa tumekaa Leaders Club.

“Baadaye nikamwambia Deo (Dk. Deogratias Michael) kuna jamaa mmoja, ambaye yeye Deo anamkumbuka sana kwa sababu mara zote huwa tunakwenda naye, anataka kutuona. Basi tukawaacha wenzetu wanafanya kazi nyingine, tukaondoka mimi na Deo around (kama) saa tano na robo usiku.

Naye akatuarifu kuwa pale Hugo alipokuwa amekaa wanafunga, akawa ameenda kule juu sehemu inaitwa Stereo, akanambia yupo pale. Mimi nikawasha gari hadi pale, nikaangalia meza ya kwanza pale sikumuona.

Tulipoingia pale hatukumwona. Nikazunguka sikumwona, nikampigia simu akaniambia nakuja hapo sasa hivi. It took like twenty thirty minutes (Ilichukuwa kati ya dakika 20 hadi 30) tangu aliposema anakuja. Tukaamua kuwasha gari ili kurudi pale Leaders lakini tukaona kama hilo haliwezekani.

Tukaishia pale Tunisia Road; kuna kontena, tukakaa pale, sasa akawa anapiga simu akisema anakuja kuna vitu anamalizia; tukawa tunawaza ni vitu gani?

Basi tukiwa tumekaa, ghafla tukamwona anafika, kwa gari. Akasema uko na Deo, nikasema eeh. Basi tukaanza mazungumzo.

Kitu ambacho nili-notice (niling’amua), while (wakati) tukiwa tuna-discuss (tunajadiliana) naye, akitaka kujua namna gani tuweke understanding (maelewano); matatizo yetu ni yapi, which are the priority areas (maeneo gani ya kipaumbele), eeh, kama alivyosema yeye mwenyewe ili aweze ku-advice (kushauri)…Sisi tukasema mambo yote yanafahamika.

Tukaongea naye kwa muda mfupi tu, akawa anaandika kwenye diary (kitabu cha kumbukumbu) yake; kwa hiyo pia alikuwa very busy communicating (alikuwa akishughulika sana kufanya mawasiliano ya simu). Unaona?

…tukafika kwamba tumemaliza…Yeye alikuwa anakunywa maji; akasema bwana mi naondoka…papo hapo wakatokea watu kama wane, watano hivi; wakasema, wakaja straight (moja kwa moja) kwenye meza yetu, as if they were directed (kama vile walikuwa wameelekezwa). Wakasema tupo chini ya ulinzi, yaani mimi hapa. Kama mtu hakujui hawezi kuja saa 5 usiku kuja kukukamata.

They came direct towards me (walikuja moja kwa moja kwangu), nikauliza kwani kuna kosa gani? Wakanipiga mtama nikaanguka kwenye barabara ya lami. Nilichokifanya kitu cha kwanza ni kutoa simu na kumpa Deo. Sasa they pushed me (wakanisukuma) na kufanikiwa kuchukua simu moja na wallet (pochi) yangu.

Wakaniburuza… hadi kwenye gari ile, ilikuwa haina namba ile, ni kama Starlet hivi. Nikaamua tu kubaki patient (mtulivu/mvumilivu).

Wakafungua lango la nyuma wakanitupa huko. Wakaja wakanitupa huko. Basi mmoja akaingia upande wangu wa kulia mwingine wa kushoto. Wakaanza kunipiga ngumi, wakanipiga ngumi, mwingine akanipiga vichwa, naona, wengine wana kama dude fulani kama la plastiki hivi, wananipiga nalo kichwani. Wananiambia tulia tutakuua sisi. Kama una ndugu zako aga kabisa kwa sababu leo hurudi.

Unatuletea usumbufu sana wewe… tunataka kukomesha hiyo tabia. Wakanipiga huku gari inakwenda mwendo wa kasi sana. Nikafanikiwa kuchungulia (nje) hivi; nikagundua tuko maeneo ya Viktoria.

Baada ya kugundua kwamba tumepita Mwenge, wakajua kama ninaelewa; wakanifunika sweta nyeusi, huku wakiendelea kunipiga kwenye gari. Mmoja alikuwa ana bunduki kubwa sana… wakawa wanaendelea kunipiga weee mpaka tukawa tumemaliza sehemu yenye lami.

Tukaingia kwenye barabara ya vumbi. Tukaenda kwenye umbali mrefu tu. Mpaka kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa sijui ni nyumba ya nani ile. Pale walipaki gari barabarani.

Wakanitupa kwenye, wakanitupa chini. Wakawa wanaulizana ‘kwanini asipitiwe tu na gari huyu wakamkuta tu hapa asubuhi?’

Wakawa wananipiga kutoka kila angle (upande), mpaka nikawa siwezi kutembea. Kwa hiyo nikawa wakinisamamisha hivi, mimi naanguka.

Wakasema eeh, sasa utakula jeuri yako. Baadaye ikaonekana kwamba that was not an idea (hilo halikuwa kusudio). Wakanipakia tena kwenye gari, this time (mara hii) wakawa wameleta gari nyingine, hii gari kama hizi aina ya Noah hizi, ambao wakifungua mlango wa nyuma unafunguka kwa kupanda juu.

Kama siyo Noah basi ile Volkswagon, mlango unafunguka kwa juu. Wakanitupa kule nyuma sasa hapo wakabamiza halafu wao wakaelekea kule mbele. Walikuwa watatu. Gari ikawa inaenda weeeee, wakati huo… siwezi kujua naenda wapi.

Wakafika kwenye nyumba moja hivi wakasimama. Hiyo nyumba hata nikiiona mchana nitaijua. Umeona! Wakanishusha…nyumba imejengwa kama za polisi huku nikipiga kelele… there was no one coming (lakini hakuna aliyejitokeza)... zile nyumba inaonekana no one is living there (hakuna anayeishi pale); nao wao they were confident to take me there (walikuwa na uhakika huo waliponipeleka huko).

Kwa hiyo, I was shouting for help (nilikuwa napiga yowe kuomba msaada), lakini no one (hakuna mtu) aliyetokea. Wakaanza kunipiga pale, kwa hiyo ile sehemu ilikuwa imewekwa aina fulani ya tiles (marumaru) za matofali.

Wakanipiga mateke, wakanipiga kwa kitako cha bunduki, baadaye nikawa nimekimbilia kama kwenye koridoo nimechukua bomba fulani la mbao nikasema atakayenisogelea mimi nampiga.

Basi akatokea jamaa pale, nikampiga kichwani. Wakasema wee jamaa unajua wewe tutakuua, nikasema I know you are going to kill me. But it is not going to be easy (Najua mtaniua. Lakini haitakuwa rahisi).

Wakanipiga, wakanifata pale wakanipiga, baadaye nikafanikiwa kuwaponyoka na nikaanza kukimbia. Unaona! Sikujua kama bunduki yao ilikuwa loaded (ina risasi),. Ndipo nikahisi wangeweza kuniua kwa sababu their gun was loaded (bunduki yao ilikuwa na risasi. Unaona…?

Ikabidi nisimame sasa. Kusimama wakanipiga tena, na hivi ni kama masaa matatu hivi. Nilikuwa napigwa tu, yaani mimi sijawahi kuona mtu anapigwa kwa kiwango kile. Walikuwa wananipiga usoni straight (moja kwa moja), yaani ngumi zinatua usoni ndo maana wakafanikiwa kunivunja meno. Na haya mengine yamelegea…unaona haya mengine ya chini yamepotea. Wamenipiga sana, nikafika mahali nikawaambia kwa hivi mlivonipiga, ni bora mkaniua.

Wakasema we utajua fate (hatima) yako; you know what to tell us (unajua cha kutuambia). Usituambie basi. Wakaniingiza kwenye kombi (aina ya gari)… tukaondoka kwenye zile nyumba mbili …

Wakanifunga miguu…wakakaza ile kamba, mikono yangu ilikuwa imefungiwa mgongoni. Walikaza kamba mpaka nikaona kama huku mikononi kulikuwa kunavimba. Hata miguu wakafunga sana. Basi wakaendesha gari, wakaendesha this time (wakati huu) muda mrefu sana. Sikunajua wanaenda wapi.

Walivokuja kunishusha, wakaanza kunipiga tena. Hasa kwa sababu I was helpless (nilikuwa sijiwezi) nimefungwa, basi nikawa napigwa nageuka hivi, nikigeuka hivi, nikaona wananipiga kwa sikio la huku, wengine wakawa wananipiga sikio la huku walinipiga sana kama half an hour (nusu saa) hivi, and then I think I lost consciousness (na nadhani nilipoteza fahamu). Unaona?

Nilikuwa na bleed (navuja damu) sana wakati ule… nikawa napata feeling (hisia) hawa watu wamenitupa mahali…nikaona kama vile wamenitupa kwenye shimo hivi. Sijui kama wanataka kunifukia? Unaona? Nikawauliza why are you burrying me alive (kwanini mnanizika nikiwa hai?)

Though (ingawa) nilikuwa naona nimepoteza fahamu nilikuwa na uwezo wa kuzungumza. Wakasema aah sasa hapa, ngoja kwanza, wakaenda kudiscuss (kujadili) kwa muda mrefu tu. Baadaye wakaja kunibeba tena, wakanirudisha kwenye gari.

Wakaenda… kule mbele walitembea kwenye pori. Wanakwenda tu porini, nadhani ndo huo msitu wa Mabwepande, mimi I don’t know (siujui). Wakafika mahali nilihisi kama wanataka kunichoma moto.

Wakawa kama wanachukua majani wanajaza pale nilipokuwa nimelazwa; wakajaza majani mengi sana kiasi kwamba it was not easy for me to breath (haikuwa rahisi kwangu kupumua).

Wakanifungua sweta walokuwa wamenifunga usoni, halafu nikaona mmoja anaondoka, anaondoka mwingine, baadaye akabaki jamaa mmoja hivi… Baadaye nikaona jamaa naye ame-disappear (ametoweka).

Nikawa nimekaa pale peke yangu. Baadaye sikujua  kimetokea kitu gani, lakini nikawa nimepoteza fahamu. Basi nilipokuja kushtuka hivi, naangalia nikaona kama kuna dalili kuwa kumeshakucha. Nikaangalia msitu, sioni kama huku kuna dalili ya makazi…nilikuwa nasikia milio ya fisi. Unaona?

Sasa nasema niko wapi… mbuga ya wanyama au ni kitu gani? Basi nikaanza kunyanyuka, kila nikijaribu naanguka. Lakini nikafungua kamba, nikaweza kutoa ile kamba ya miguuni, baada ya kuhangaika kama dakika 40 hivi.

Kwa hiyo nikawa natembea kidogo naanguka. Nikatembea umbali kama wa saa nzima hivi; naanguka naishia kwenye miti, nikafika pale nikasikia mlio wa gari, ndo nikatembea, nikasikia tena mlio wa gari, mpaka nikaweza kutokea barabara ndogo, ambayo nilikuja nayo na wale walionitupa…

Basi nilipofika hapo, nikakaa, nikalala pembeni ya barabara. Muda huo nilioamka nikaona magari yanapita. Ninajaribu kuwashtua wanagoma kusimama, ile sehemu ilikuwa inaonekana kuna mambo ya ujangili sana. People were not ready to stop (Wenye magari hawakuwa tayari kusimama).

Mpaka akapita mwenda kwa mguu mmoja, ndio niliweza kumweleza, akaja kunisikiliza, akahangaika namna ya kunifungua kamba kwa sababu hakuwa na kisu. Basi nikawa relieved (nikapata ahueni) mikononi. Nikagundua nimevimba sana. Magari mengi yalikuwa yanapita tu, jamaa akafanikiwa kusimamisha Suzuki moja.

Akanipeleka mpaka Kituo cha Polisi cha Mabwepande cha Bunju. Bahati nzuri nilikuwa nakumbuka namba (ya simu) ya Deo. Nikawaambia wampigie kumweleza kwamba niko kule. Nilikuwa Mabwepande.

Baada ya hapo, ukiondoa maumivu na huu uvimbe na uso kutoka damu nyingi, lakini sikuwa na shida yoyote. Lakini throughout (wakati wote) kule kwenye gari walikuwa wakisisitiza kuwa wee jamaa umeshatusumbua vya kutosha. Nikawaambia nimewasumbua nini?

Mimi nilikuwa kwenye mazungumzo; sasa kwenye mazungumzo ndo kusaini makubaliano? Wewe unatakiwa kusaini makubaliano. Sasa makubaliano gani? Mimi sijawahi kukaa mahali nikakataa kusaini makubaliano yoyote. Na hakuna popote eti mimi nilikaa na watu ku-discuss (jadiliana) kitu halafu ikashindikana kukubaliana.

Nikawaambia if you want to kill me just kill me (kama mnataka kuniua basi niue tu) lakini siyo kwa sababu nimeshindwa kusaini makubaliano yoyote. Dereva yule, bwana mmoja mnene, na ukiangalia wao walikuwa wamenyoa wote… walinyoa kama all were soldiers (wote ni askari). Na hata walipokuja kuniambia niko chini ya ulinzi nikajua nimekuja tu kukamatwa. Lakini I was surprised (nilishangaa) mle ndani nilikuwa napigwa muda wote.

Kwa hiyo nadhani at the end of the day (hatimaye) walichofanya siyo sahihi, na kwa hiyo wamenikamata mahali ambapo watu wamewaona wakaniambia tunajua katika mazingira ambayo no one will ever trace you (hakuna atakayeweza kukutafuta na kukuona).

…kwa hiyo stori, kwa kifupi, ilikuwa ni hiyo. Lakini kwa kweli mimi sijawahi kupigwa kama nilivopigwa kwenye hiyo safari, wala sijaona mtu anapigwa kiasi kile. Nilipigwa kama hivi mpaka unafika mahali unajaribu kuangalia unaona giza. Huoni kilichoko mbele yako, yaani giza, wakati huku una fahamu zako, huoni.

Wanakupiga na vitu vizito, huku wamebana na koleo… Walikuwa wananibana huku kwa mfano kama kuna vitu nakataa kusema, kwa hiyo wanasema yaani wewe kwanini husemi, nikawaambia mimi, mpaka unapokubaliana nao wanakuachia.

Kwa hiyo ukikaa kidogo walikuwa wanabana kucha, ndo maana nyingine wamenyofoa nyingi. Utasema leo, jamaa wanakutisha kama dude fulani huku chini, wanakubana… wanasema wewe unaonekana ni jeuri sana…

Zaidi …maswali yalikuwa ni kwamba wewe mbona ni msumbufu sana? Kwanini unatusumbua yaani? Hayo ndo maswali walikuwa wanauliza. Nikawaambia kwani nani anawasumbua? Wakaniambia unajua wewe nani anatusumbua.

(Wakawa wananiambia) utaenda kukaa mahali ambako no one will be able to trace you (hakuna atakayeweza kukugundua). Nakumbuka ilikuwa imefika mahali natoa damu mdomoni, natoa damu kichwani, yaani natoka damu karibu kila mahali… That was horrible life (yalikuwa maisha ya kuogofya).

0
Your rating: None Average: 4 (1 vote)