Kauli za wananchi juu ya mgombea urais wa CHADEMA


Ndimara Tegambwage's picture

Na Ndimara Tegambwage - Imechapwa 04 August 2010

Printer-friendly version
Dk. Willibrod Slaa

Ufuatao ni mrejesho wa baadhi ya wasomaji 417 waliotutumia ‘sms’ juu ya mwandishi, maudhui ya makala na somo lenyewe – Dk. Willibrod Slaa.

NIMEFURAHIA kusoma “msimu wa mashushushu…” Tumwombe Mungu Watanzania wasidanganywe na vijizawadi vya kijinga. Gamaliel P. Kileo. 0655975239

Kama wanasema Dk. Slaa ni choice ya Wakatoliki, je, tuseme nini kwa Kikwete? Chaguo la Waislamu? Hawa watu wanataka kuleta udini katika nchi yetu. CCM kama KANU kuna siku itafika mwisho maana wanakuja wasiotaka rushwa. Ev. Kimangi Cyprian wa Arusha.

Naumia sana kuona watu makini kama Dk. Slaa wanapakaziwa ujinga. Naomba zifanyike juhudi za dhati, kuwaomba Lipumba na Mtamwega na wengineo kumsapoti Dk. Slaa awe mgombea pekee upinzani. 0713710422

Makala yako ina mashiko. Nina uhakika muda wa mabadiliko unakaribia. Uchaguzi wa mwaka huu unaweza kubadili historia kama wapinzani wataungana na kumuunga mkono Dk. Slaa. 0755254583

Dk. Slaa anafaa kuwa rais wa wanyonge. Sera ya Kilimo Kwanza haina maana yoyote kwa wananchi. Ni uzushi wa CCM tu. Badala ya kuleta trekta wameleta genereta. Hiyo ni danganya toto. Slaa ndiye tunamtaka. 0655565711

Nasoma makala yako. Ni kweli. Kumsikiliza Mrema (Augustine wa TLP) ni sawa na kupunguza uzito wa mijadala ya hatima ya maisha ya Mtanzania. Watanzania tuamke. Hongera Slaa. Naitwa J. Gwau. 0713765061

Umenena mzee. Hata sisi wapigakura wa Karatu tuliomchagua Dk. Slaa kwa misimu mitatu, tuliishaletewa mashushushu (wakidai) kuwa dokta hawezi kuongoza…lakini tuliwakataa (CCM) mpaka wakawa wapinzani na hicho chama chao cha mafisadi (Halmashauri ya Karatu inaongozwa na CHADEMA). 0716240608

Nimefurahishwa na makala yako. Natoa wito kwa wapenda maendeleo tumuunge mkono Dk. Slaa…hata tupate wabunge wengi wa upinzani. 0612389120

Huyo ndiye mkombozi tuliyekuwa tukimsubiri ambaye ni chaguo la kila Mtanzania lakini siyo mafisadi. 0753679837

Tafadhali waulize CCM: Kwa nini askofu wa Katoliki (Methodius Kilaini) aliposema Kikwete ni chaguo la Mungu walikaa kimya na haikusemwa kuwa Kikwete ni chaguo la Kanisa Katoliki? 0754486612

Nilidhamiria kutopiga kura…lakini kwa dokta huyu, msimamo wangu nimeulegeza na kura yangu ni kwake tu. 0757908170

CCM imebweteka mama ilivyokuwa KANU. Tuungane tulete mapinduzi ya kweli; Dk. Slaa ashinde. 0715943243

Even Michelle de Nastradamus didn’t know about tomorrow. This time will be like French revolutionists unless they do mob psychology and steal our votes. Revolution is now! 0753989617

Nakupongeza kwa makala hii. Nitafunga na kuomba nione CHADEMA ikisinda kwa kishindo. Amen. 0754269840

Makala yako imejaa ukweli mtupu. Hongera. Mimi nitamchagua mtetezi anayejua wanyonge, Dk. Slaa.

Ninaona uchungu kila siku pale serikali ya CCM ilivyokatisha pensheni yetu eti mpaka tufikie miaka 56 wakati ni wao waliotupunguza kazini…Je, tutakula nini ili tufikie huo umri? Hii ilikuwa sawa na kusema tufe. 0688552392

Asante kwa kutufungua macho. Tunawaunga mkono… mabadiliko ya kweli yanawezekana. Jamii inatutazama sisi. 0762085189

Tunawaomba nyinyi MwanaHALISI msinunuliwe kirahisi kama magazeti mengine; ongezeni nguvu…tunaomba ratiba ya Dk. Slaa Mbeya. 0767212020

Asante kwa makala yako. Napata uchungu kwa nchi yetu kuendelea kuwa masikini wakati tuna raslimali za kutufanya tuondokane na na dimbwi la umasikini. Tatizo ni uongozi mbaya wa CCM…Sasa Watanzania tutake nini?

Dk. Slaa ni kiongozi shupavu, msema kweli; najua anaweza kutufanya tufurahie kuzaliwa. Shime wana-CCM wenye machungu na nchi yetu; mpigieni Slaa kura Oktoba. Ni kiongozi wenu. 0789558395

Ningependa kukwambia kuwa kuna watu wanajali mchango wako na gazeti hilo unaloandikia. Tupo nyuma yenu. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika. Lucas, Dar. 0718555909

CCM wamechemka. Dk. Slaa chaguo la Mungu. Kama sheria inaruhusu, Lipumba awe mwenza…pamoja na tume yao watachemka. Mpenda mageuzi, Bagamoyo. 0767115203

Wazazi wamechoshwa na mzigo mzito wa ukali wa maisha. Wanafunzi siyo government priority anymore; wasomi hawaridhishwi na utendaji mbovu wa serikali.

Wafanyakazi waliishaambiwa hizo kura zao laki tatu hazitakiwi na watukuka, wakulima wamechoshwa na takwimu nyingi zisizokuwa na tija kwao. Slaa anayajua haya. 0712845241

Bravo…! You have indeed spoken for the silent majority. God bless you! 0784851992

Kwa jinsi hii Mungu alivyoipenda Tanzania, ndio maana amemtuma mwanae wa pekee Willibrod Slaa aje kuwakomboa Watanzania na umasikini na ujinga. Amina. 0652229500

Waambie CHADEMA hakuna kazi rahisi na mafisadi siyo mchezo; kila mtaka mapinduzi kwa imani yake amwombee Slaa ushindi aingie ikulu awang’oe mafisadi. Asante. 0658276636

Mungu akujalie afya njema, uzima na ulinzi siku zote katika jitihada za kuunga mkono michango ya viongozi wenye kiu ya maendeeo ya kweli na wenye uchungu na taifa hili

Kiongozi mzuri ni yule anayefanana na St. Martin de Tours anayemuomba Mungu; kama watu wanamhitaji basi kazi hiyo hawezi kuikataa, kwani si kwa matakwa yake tena bali matakwa ya watu; si kwa mapenzi yake mwenyewe bali kwa mapenzi ya Mungu. Dk. Slaa anafanana na St. Martin. 0714832696

Dk. Slaa inawezekana akawa ndiye chaguo la Mungu kwa ajili ya kuwakomboa wanyonge wa nchi hii. Tunamsubiri kwa hamu. Bisigoro, Mwanza. 0755735633

Kaka hongera…napenda unavyoandika makala zako bila woga. Mungu aendelee kukupa afya njema ili Watanzania wazidi kupata habari za uhakika. Naitwa Patrq. 0767007300

Hongera kwa makala ya leo. Je, Watanzania wanayafahamu haya? Ongezeni juhudi kuwaamsha; siku moja watatoka usingizini na kutambua jinsi viongozi wao wanavyowasaliti. Wanakula hata mbegu!

Mkurugenzi (wa shirika la umma kulipwa shilingi milioni 25 kwa mwezi – sawa na mishahara ya walimu 83 wanaopata Sh. 300,000 kwa mwezi. Rais anayajua haya? Wasaidieni Watanzania kupitia kalamu zenu ili tusiendelee kudanganyika. Mungu awabariki. 0655880544

Nimesoma makala yako. Mimi ni mmoja waliokuwa wamekata tamaa kupiga kura. Lakini baada ya Dk. Slaa kuchukua fomu, hakika nimepata matumaini mapya. 0763640336

Nimekusoma. Dk. Slaa, mbali na kuibua kasha mbalimbali, ndiye kiongozi, mbunge pekee aliyetaka wabunge wapunguziwe mishahara kwani ni ya juu. Slaa ni mtu wa utu. Okayo. 0754689684

Watake wasitake, ipo siku wataondoka hapo walipo. Wananchi tumechoshwa na hao watu. 0776638263

Ni muhimu CHADEMA na CUF waungane kumpigia kura dokta. Kama una namba za Mbowe na Lipumba, nitumie nishiriki kuwashawishi. 0713635819

…Mbowe na Lipumba wazunguke nchi nzima kuwanadi wagombea…0713801248

Hongera kwa andiko. Jiungeni waandishi mnaojali ukombozi wa nchi hii na siyo vijisenti ili mwandike ukweli kuhusu Dk. Slaa na chama chake…0784887475

Bwana Ndimara, A luta continua! Kama vyama makini vikiunganisha nguvu na raia wanyonge, nakuhakikishia kwa uwezo wa Muumba, Tanzania itakombolewa kutoka CCM! 0784452626

Makala zako nzuri. Tuko nyuma ya Dk. Slaa kuhakikisha anaingia ikulu. Dharau za Kikwete dhidi ya watumishi wa umma na Tucta si za kuvumilia hata kidogo. 0784505759

Hongereni kwa makala zenu zilizosheheni ukweli wa kina. Mpe pole Kubenea ila amtegemee Mungu kama mlinzi wake… 0715702005

Dk. Slaa…kateuliwa na Mungu kuja kuokoa kondoo waliopotea kwenye jangwa…tusipige teke maendeleo. Hongera Ndimara kwa makala nzuri…endelea kuelimisha bila kuchoka. 0717935721

Kwa sasa kauli inayotoka kwa watu kuhusu Dk. Slaa ni “Na mimi nitampa kura yangu’: kauli iliyoko kwa vijana wengi waliopoteza kura zao mwaka 2005 kwa kufuata mkumbo.

Lakini pia ni kauli ya wafanyakazi waliofananishwa na mbayuwayu. Ni kauli ya wakulima wasiofaiudika na nguvu zao mashambani na kauli ya wanafunzi vyuo vikuu waliodanganywa kuwa hawatafukuzwa kwa kukosa ada.

Ni kauli ya wastaafu wanaoteseka kwa kukosa mafao yao baada ya kulitumikia taifa kwa uadilifu na uzalendo. Hii ni kauli itakayobadili historia ya nchi hii hapo 31 Oktoba. 0716754307

Ubarikiwe Ndimara. Tafadhali andika juu ya wajukuu zangu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao hawatapiga kura kutokana na kuchelewa kufungua muhula huu. 0735613218

Dk. Slaa anaweza kuwa rais. Tunahitaji kushikana na kushikamana ila tatizo lipo kwa waandishi; wengiwenu ni vibaraka wa CCM. Mungu mbariki Slaa. Mapinduzi daima. 0712257975

Mimi naamini Dk. Slaa ni makini sana na Tanzania ingekuwa better off akiwa president. Lakini haya ya ushushushu yaliyosemwa juu ya CUF wakati huo, yaliungwa mkono na makanisa na waandishi wa habari kama nyie hamkuitetea CUF wakati ule mnasema leo?
0776651983

Hongera kwa makala yako ya uchambuzi. Tafadhali endelea na juhudi zako za kuelimisha umma wa Tanzania. 0658280132

Mimi ni mzazi. Naunga mkono kugeuza CCM kuwa upinzani. Tanzania ya mageuzi inawezekana. 0715552300

Wakati ni huu. Tuongee na vyama makini tuungane CCM inang’oka. Dk. Slaa ana rekodi safi. Tusonge mbele, umma utaamua. 0756318842

Hakika wewe umetumwa na Mungu. 0715808283

A luta continua! Kuna siku Mwenyezi Mungu atatupa rais ambaye ana uchungu na nchi (yetu). 0787015656

Ndimara, uchambuzi wa leo umefundisha mengi. Watu wengi wanataka daftari la wapigakura lirejeshwe ili wajiandikishe; sababu ya Dk. Slaa.0784925484

Naomba kulishukuru gazeti la MwanaHALISI kwa kunitoa ukungu machoni. 0784557065

Ndugu Ndimara, uko karibu na viongozi wa CHADEMA? Kama ndiyo, waambieni watoe ile namba yao kupitia mitandao ya simu ili sisi wananchi wenye uchungu na nchi tuweze kuchangia chama hicho. 0715509774

Kwani mnajua kundi kubwa la wanafunzi hatutapiga kura kwani tulijiandikishia vyuoni na wakati wa kupiga kura tutakuwa nyumbani? Piganieni hilo mtusaidie. 0719393430

Tanzania bila CCM inawezekana. Kwa nini nyie wataalam wa siasa hamshawishi vyama vya upinzani vikasimamisha mtu mmoja kama Dk. Slaa tukang’oa ufisadi Tanzania? 0712110353

Dk. Slaa chaguo halisi. Watanzania tuache unafiki. Hakika Mungu katupa chaguo bora. Nilitaka nisipige kura ila Slaa kanipa imani. Nitampigia. 0658614696

Inzi na nyuki hufa kwa kulazimisha kupenya kwenye kioo angavu. Ndivyo watakavyoangamia wasomi, wafanyakazi, wakulima, waandishi wa habari na wahariri wanaolazimisha ndoto zao kupitia CCM.

Kikwete aliingia kwa mbinu atoke kwa mbinu. Pambazuko na mkombozi ni Slaa.

Ni jukumu letu sote kumfanya Dk. Slaa kuwa rais Oktoba; kwa manufaa ya Watanzania na siyo CHADEMA. Naamini Dk. Slaa hawezi kusema foleni (za magari) za Dar ni maisha bora…atatafuta njia ya kuzimaliza; na huyo ndiye rais tunayemtaka. 0713351957

Wakati ndio huu…tusisubiri shamba la bibi libaki mabua matupu ndio tuwatafute nyani. Kwa nini tusiwazuie kabla? 0719083529

Watanzania wamekata tamaa. Wameishia kujifariji kuwa baada ya miaka 20 ndio upinzani utashika nchi. Hawajui wakati ndio huu. Kisu tumeshika wenyewe… 0719083529

Kwa mtu makini kwa nchi yake kama Dk. Slaa, nitampa kura yangu. Mungu bariki maamuzi ya wananchi. 0713326314

…Tunaomba CHADEMA wafanye mipango tuchange kupitia simu za mkononi. Wanahitaji pesa nyingi – ni operesheni kuing’oa CCM! 0754360781

Kama kweli Dk. Slaa katumwa na Kanisa, wanavyosema hawa mashambenga, basi waumini wote wa Katoliki wampigie kura na yangu ikiwemo; mimi Mwislamu, msomaji wa MwanaHALISI. 0713450966

Congratulation pour le message d’aujourd’hui, c’est impeccable, merveilleux (Hongera kwa ujumbe wako wa leo, ni thabiti, maridhawa) 0654316767

Safari hii nilikuwa nisipige kura. Si kwamba sijui umuhimu, lakini ningempigia nani? Sasa kura yangu, kwa haki kabisa, nitaiweka kwa SILAHA (Dk. Slaa) 0757222270

Nakupongeza kwa makala nzuri. Jamani ongeeni wa wapinzani waungane kumsimamisha mmoja (Slaa). 0715948697

Msihi Dk. Slaa amshawishi Lipumba amwachie na amuunge mkono katika kugombea urais. 0763859485

Kweli CUF waungane na CHADEMA kwa bara na kwa Visiwani wote waungane na CUF kwa nafasi ya urais. 0713423616

(Wapinzani) zaidi ya umoja, kampeni za urais fikeni angalau tarafani. Mtashinda. 0784706732

Msimu wa mashushushu huu hapa. Maoni yangu: Mrema anastahili zawadi. Nayo ni kadi ya CCM. Godfrey, Ukonga. 0654184135

0
No votes yet
Soma zaidi kuhusu: