KVTC yajikita Kilombero kuendeleza misitu


Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 28 October 2009

Printer-friendly version

TANZANIA imejaliwa kuwa na rasilimali za kutosha kuendesha uchumi wa nchi, lakini pengine inabaki katika giza kutokana na kukosa watalaamu wa kutosha katika sekta nyeti kama vile madini na misitu.

Kutokana na hali hiyo, watalaamu mbalimbali wamekuwa wakijitokeza kusaidia kuendeleza maeneo husika ama kwa kuanzisha kampuni au kufanya kazi chini ya mwavuli wa serikali.

Kampuni ya Kuzalisha Mitiki au Mivule ya Bonde la Kilombero (KVTC), ni moja ya kampuni ya kitaalamu iliyojimbia katika wilaya ya kilombero Mkoa wa Morogoro, ikiendeleza kilimo cha misitu.

Inakutana na kikwazo kutoka kwa wananchi wanaoona kwamba wanaporwa ardhi yao, lakini kwa kutumia makubalino kati ya Serikali Kuu Shirika la Maendeleo la Nchi za Madola (CDC) ilikubalaliana eneo hilo kuendelezwa.

Wananchi wakapewa elimu ya kutosha juu ya faida ya kampuni ya KVTC iliyoanzishwa mwaka 1992 kwa kufanya kazi kwa pamoja na CDC chini ya mwavuli wa Serikali ya Tanzania , iliyotathimini na kuona kwamba mivule inaweza kuendelezwa mkoani humo.

Baada ya tathimini hiyo, serikali ikatoa hekari 28,132 zilizolimwa miombo ili kuendeleza msitu wa mivule ambayo leo hii imekuwa na soko kubwa na kufaidisha Tanzania kwa kodi na huduma za jamii.

Kwa mfano, hivi karibuni kampuni hiyo ilichangia Sh. 40 milioni katika wilaya za Kilombero na Ulanga kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Vijiji vilivyofaidika na msaada huo ni pamoja na Milola, Igumbiro, Lupiro, Nakafuru, Kidugalo, Iragua, Itete, Mianziani na Mavimba vya Ulanga wakati Namawala na Idete vya Kilombero.

Mradi huo ulikua baada ya kutokea kwa Mfuko wa Kuendeleza Viwanda wa Finland “Finnfund’, ulioingia ubia wa kuendeleza eneo hilo kwa kupata hisa asilimia 23 ili kusaidia miradi ya maendeleo inayosimamiwa na KVTC kwa miaka mitatu yaani kutoka 2000-2003.

Kutokana na ushirikiano huo, KVTC leo hii wanahesabu mtaji wa wa dola 48 milioni za Marekani kutoka CDC, dola milioni tisa kutoka Finnfund huku wakiwa na dola 10 milioni kutoka benki ya CRDB za mkopo.

Hakuna ubishi kwamba mtaji huu, unafanya KVTC kuwa moja ya kampuni kubwa iliyowekeza kwenye sekta ya misitu.

Kutokana  mafanikio hayo, kampuni hiyo, imekuwa ikitumia hekari 7,800 kupanda mitiki tangu mwaka 1993 na kusimamia karibu hekari 20,000 za pori la asili ya miti hiyo.

Kutokana mavuno ya miti hiyo, KVTC imekwenda mbali zaidi katika mafanikio kwa kufungua kiwanda ambacho kinaandaa miti iliyovunwa kabla ya kuifikisha sokoni.

Meneja wa Kampuni ya KVTC, Rican van Wyk, anasema Agosti mwaka huu, wameanza kuvuna mitiki hiyo hivyo kuwa katika nafasi ya kulipa kodi isiyopungua dola 10 milioni kwa mwaka.

Fedha hizo zitatokana nna masoko yake katika nchi za Mashariki ya mbali, Ulaya na Amerika ya Kaskazini.

 Ukiacha kodi, kampuni hiyo imetoa ajira kwa watu wapatao 700 katika mashamba yake. Pia kuna wasimamizi wasiopungua 120 wakati kiwandani kuna wafanyakazi zaidi ya 110.

 "Watu wengi wanaofaidika na ajira hizo ni wakazi wa Kilombero na Ulanga," anasema Wyk.

 Rekodi hiyo ya idadi ya wanaopata ajira, inaonyesha ni namna ambavyo kampuni hiyo imekuwa muhimu kwa wakazi wa Morogoro.

 Kutokana na mafanikio kama hayo, ndiyo maana mwaka 2004, kampuni hiyo ilitambuliwa na shirika la viwango vya kimataifa kuwa moja ya kiwanda kinachotoa bidhaa zenye ubora wa kimataifa hivyo kukidhi soko la dunia.

Walipewa cheti namba ISO14001 na tangu hapo wamekuwa wakibaki kwenye ubora huo hivyo kuendelea kushikilia hati hiyo ya ubora.

Mwaka huu, 2009 Kampuni ya kuandalia ubora wa viwanda-SGS iliituza KTVC cheti kwa ubora wa bidhaa baada ya kununua bidhaa zake kwa kuwa zineuzwa kisheria na kutoka katika kiwanda bora.

Mbali ya upandaji miti, kampuni hiyo pia inajishughulisha na ufugaji wa nyuki huku ikisaidia vijiji vilivyozunguka katika shughuli mbalimbali za jamii kama vile barabara na shule.

0
Your rating: None Average: 4 (2 votes)