Membe asilishe watu siasa chafu

Isaac Kimweri's picture

Na Isaac Kimweri - Imechapwa 16 March 2011

Printer-friendly version
Tafakuri

MAWAZIRI wawili, Sophia Simba na Bernard Membe, wametoa tuhuma nzito kuhusu ustawi wa siasa nchini. Kwa nyakati tofauti, Membe na Simba wametuhumu mataifa ya nje kuwa yanajiingiza katika siasa za ndani ya nchi kwa kufadhili chama kimoja cha siasa ili kifanye vurugu na kuvunja amani ambayo imetamalaki nchini kwa miaka mingi.

Membe ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati Sophia ni Waziri wa Maendeleao ya Jamii, Jinsia na Watoto. Wote walipata nyadhifa za uwaziri wakati wa serikali ya awamu ya nne; kwanza Sophia alikuwa waziri kamili na Membe alianza kama naibu waziri katika wizara ya Mambo ya Ndani na baadaye Madini.

Aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje kufuatia Dk. Asha-Rose Migiro kuteuliwa kuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).

Sophia wakati wa ngwe ya kwanza alianzia hapo alipo, kisha akaenda ofisi ya rais - Utawala Bora na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana amerejea alikoanzia Januari 2006.

Nimetaja kwa kifupi tu nafasi walizoshika viongozi hao ili kuwathibitishia wasomaji wetu kwamba wamo ndani ya serikali kwa muda sasa na kwa hakika wanajua kila kinachoendelea serikalini na kwa mataifa rafiki.

Nitangaze mapema kwamba sitajadili kauli ya ‘mataifa ya nje kusaidia chama cha siasa’ nikimlenga Sophia ingawa ndiye aliyeitaja CHADEMA waziwazi.

Nitaelekeza nguvu kwa Membe kwa sababu nyingi tu za kimsingi. Huyu ni kachero aliyebobea, hasa tukikumbuka alivyoshughulika na suala la Dk. Hans Kitine, na sakata lake la kudanganya kwamba mkewe alikuwa mgonjwa na kutibiwa kwa Sh. 60 milioni nje ya nchi, kumbe kiini macho. Kwa maneno mengine Membe anatazamwa kama waziri makini.

La pili ambalo ni la umuhimu wa juu zaidi, Membe ni Waziri wa Nje, ana fursa nyingi mno za kukutana na mabalozi, anasafiri sana nje ya nchi, ana nafasi nzuri sana ya kujifunza na kutambua dunia kwa sasa ikoje na kwa kweli taifa lake kiuchumi likoje hasa likilinganishwa na mengine duniani.

Kwa maana hiyo, Membe si mtu ambaye anatarajiwa kuwaza au kuropoka jambo kubwa kama hilo la kutuhumu ofisi za balozi nchini kusaidia chama cha siasa, kwa kujaribu kujenga hoja dhaifu juu ya harakati za CHADEMA na maandamano yake ya kuhamasisha uwajibikaji wa serikali kulingana na mahitaji ya kweli ya wananchi.

Kwa hiyo, wakati Sophia anaweza kusamehewa kwa kukopa msemo wa waumini wa Kikristo ‘hajui atendalo’ kwa Membe ni tofauti sana. Anajijua na anatazamwa kama miongoni mwa miamba ya siasa za Tanzania inayoibukia kwa sasa kuelekea mwaka 2015.

Membe anapaswa kukumbuka kuwa CHADEMA walianza operesheni zao tangu mwaka 2007, walipobuni Operesheni Sangara ikifuatia uamuzi wa Bunge wa kumsimamisha mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, kutokana na hoja ya Buzwagi.

Tangu wakati huo, CHADEMA wamekuwa na operesheni kadhaa za kujinadi kwa wananchi hata kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana, juu ya mambo kadhaa lakini kubwa ni kueleza jinsi rasilimali zao zinavyoibwa.

CHADEMA walipata kuanika orodha ya mafisadi 10 kwenye viwanja wa Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam, na Membe anafahamu orodha ile hadi leo ipo na haikupatikana kwa nguvu za mabalozi, ila ni wizi unaofanywa na wahusika katika ofisi za umma kuanzia sakata la EPA ambalo linajulikana wazi kwamba jumla ya Sh. 133 bilioni zilichotwa kifisadi.

Membe anajua pia kwamba suala la umeme ambalo CHADEMA safari hii wamelivalia njuga ni matokeo ya mikataba mibovu kama wa Richmond ambao uliileta nchini pia Dowans ambayo sasa inaidai TANESCO Sh. 94 bilioni baada ya kushinda kesi dhidi yao kuhusu kuvunjwa kwa mkataba wa kuzalisha umeme.

Kadhalika, Membe anajua vilivyo kuwa mkataba wa Richmond ndio ulisababisha Februari 8, 2008 kuvunjika kwa Baraza la Mawaziri kwa kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa. Pia mawaziri wengine wawili, Nazir Karamagi aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini na mtangulizi wake kwenye wizara hiyo, Dk. Ibrahim Msabaha, walijiuzulu sambamba na Lowassa.

Lakini zaidi, tukitazama mambo ambayo CHADEMA wanasimamia kwa sasa, yaani kuzidi kupanda kwa gharama za maisha; umeme wa ghali, na kukataa kulipwa Sh. 94 bilioni kwa Dowans, si mambo ya CHADEMA, ni mambo yanayogusa maisha ya kila siku ya wananchi, CHADEMA wanawakumbusha tu wananchi kwamba serikali iliyopo madarakani inapaswa kushughulika na matatizo hayo. Kwa maneno mengine CHADEMA wanaikumbusha serikali kwamba kuna kazi ya kufanya ambayo haijafanywa.

Kwa kuwa Membe ameamua kujirahisisha mwenywe, naomba kumuuliza maswali haya. Hivi mfumuko wa bei unakuwaje ni suala la kuchochewa na nchi za nje? Je, si kweli kwamba kwa sasa  wananchi wanalia kwa mfumuko wa bei? Membe hajui hili? Je, Membe haoni bei ya petroli inavyopaa kila uchao?

Mbili, nani anayeweza kusema kuwa anafurahishwa na Dowans kulipwa na TANESCO Sh. 94 bilioni? Je, Membe anaafiki malipo haya pamoja na mizengwe yote inayojulikana kuhusu Richmond ambayo iliurithisha mkataba wake kwa Dowans? Je, Membe hakuwa sehemu ya Bunge la Tisa lililoagiza mkataba wa Dowans uvunjwe?

Sasa CHADEMA wanaposhupalia Dowans kutokulipwa hata senti moja inakuwaje ionekane ni mpango wa mataifa ya nje?

Ukitafakari kwa kina hakuna hoja inayosukumwa na CHADEMA ambayo haina mashiko kwa wananchi; zote zinaonyesha dhahiri shahiri kwamba taifa lipo matangani; shida nyingi za wananchi. Kwa sasa elimu tabu, mahitaji ya wananchi kama chakula, usafiri katika kila nyanja ni tabu. Haya hakika si mapya machoni kwa Membe.

Mwisho, Membe anapaswa kuelewa kwamba serikali ambayo yeye ni Waziri, hayo mataifa anayosema yanafadhili CHADEMA, yakiamua kukata misaada yake ya kibajeti, serikali hiyo hakika itaanguka. Kwa hiyo wa kulaumiwa kwa kutumia fedha za wafadhili ni serikali, hakika si CHADEMA.

Membe anapaswa kuwa makini zaidi, kwa kuwa kama anataka sifa nyepesi awe tayari kudondoka kwa wepesi huo huo katika anga za kisiasa. Na Isaac Kimweri

MAWAZIRI wawili, Sophia Simba na Bernard Membe, wametoa tuhuma nzito kuhusu ustawi wa siasa nchini. Kwa nyakati tofauti, Membe na Simba wametuhumu mataifa ya nje kuwa yanajiingiza katika siasa za ndani ya nchi kwa kufadhili chama kimoja cha siasa ili kifanye vurugu na kuvunja amani ambayo imetamalaki nchini kwa miaka mingi

Membe anapaswa kuwa makini zaidi, kwa kuwa kama anataka sifa nyepesi awe tayari kudondoka kwa wepesi huo huo katika anga za kisiasa..

0
No votes yet
Soma zaidi kuhusu: