Mungu aitwa mahakamani


Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 02 December 2009

Printer-friendly version
MUNGU ameponea chupuchupu

Jaji Marlon Polk wa Marekani ametupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa dhidi yake.

Jaji amechukua hatua hiyo kwa maelezo kuwa anwani ya Mungu haipatikani na hivyo hawezi kupelekewa samansi ya kuitwa shaurini.

Kesi hiyo ya aina yake ilikuwa imefunguliwa na Seneta wa Nebraska, Ernie Chambers, ambaye sasa anasema anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa jaji.

Chambers alitaka itolewe amri ya sitisho la vifo, uharibifu na ugaidi “vinavyosababishwa na Mungu.”

Jaji Polk alisema katika uamuzi wake kwamba mlalamikaji alipaswa kuwa na uwezo wa kumfikia mshitakiwa ili kesi yake iweze kuendelea kusikilizwa.
 
"Kutokana na mahakama hii kugundua kuwa hakuna uwezekano wa samansi kumfikia mtajwa kwenye kesi husika, mahakama hii  inatupilia mbali shauri lililofunguliwa," alisema Jaji Polk katika uamuzi wake.

Chambers hawezi kufungua kesi upya bali anaweza kukata rufaa. Anasema bado anatafakari kwa makini uamuzi huo ili kujua kama atakata rufaa au la.

Alifungua kesi hiyo mwaka jana, na kwamba alisema, “Mungu alikuwa amesababisha vifo vingi na uharibifu na ugaidi kwa mamilioni ya wakazi wa dunia."

Chambers alisema, “Mahakama ilijua kuwepo wa Mungu na yote ayafanyayo kiasi cha kujua uwezo wake wa kujua yote. Kwa vile Mungu anajua kila kitu, basi ni wazi kuwa atakuwa anajua kwamba kuna shitaka hili dhidi yake."

Seneta hiyo wa Nebraska kwa miaka 38, alinukuliwa akisema alifungua shitaka hilo ili kutoa ujumbe kuwa mtu yeyote anaweza kumshitaki yeyote akiwamo Mungu.

Jaji Marlon Polk wa Marekani ametupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa dhidi yake. Jaji amechukua hatua hiyo kwa maelezo kuwa anwani ya Mungu haipatikani
0
No votes yet