Pat Robertson: Seneta wa Replican aliyefanya biashara na Mobutu, Taylor


Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 27 January 2010

Printer-friendly version
Pat Robertson

NI seneta mpya wa chama cha Repulican katika jimbo la Massachusetts. Amepita katika migogoro na shutuma nyingi kutokana na kauli zake.

Ni mtu anayejulikana sana katika dini yake na hata kwenye uwanja wa siasa.Vitendo vyake, mwenendo wake kwenye sekta ya biashara, aghalabu vimekuwa vikipamba taarifa katika vyombo vya habari.

Kauli na vitendo alivyowahi kuvitoa na kufanya, kiasi cha kuleta mkanganyiko na gumzo kubwa ni wakati akijitangaza kuwa mlokole. Kauli yake kwamba baadhi ya madhehebu ya kiprotestanti ni maficho ya wapinzani wa Yesu,ni baadhi tu ya kauli zilizozua kasheshe.

Si hivyo tu, seneta huyo pia amewahi kudai kuwa ana nguvu ya kufukuza vimbunga na tufani kwa kupitia sala zake.

Huyo ndiye Pat Robertson, seneta mpya wa Massachusetts kwa kofia ya Republican. Alichaguliwa wiki iliyopita baada ya kumshinda mgombea wa Democrats, Martha Coakley.Uchaguzi huo ulikuwa unafanyika kufuatia kifo cha seneta Edward Kennedy, mwaka jana.

Huyu amewahi kuwa na mahusiano ya kibiashara na fedha na rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor. Taylor alimruhusu kuchimba almasi za Liberia. Hivi sasa Taylor ameshitakiwa katika mahakama ya kimataifa ya The Hague, kutokana na uhalifu wa kivita.

Pia amewahi kuwa na uhusiano wa kibiashara na aliyekuwa rais wa Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo-DRC), Mobutu Sese Seko, ambaye ana rekodi mbaya ya kuiba mali za nchi yake na kuzificha nje, huku akiiacha nchi yake ikiwa haina maendeleo. Mobutu alipinduliwa na Laurent Kabila, wakati yeye akiwa kwenye matibabu nchini Morocco. Alifariki dunia na kuzikwa huko huko.

Robertson alishutumiwa duniani kote kutokana na wito wake kwamba Hugo Chaves, Rais wa Venezuela, auawe.

Lakini pia alilaumiwa sehemu mbali mbali duniani alipotoa kauli kuwa ugonjwa wa kiharusi uliompata aliyekuwa Waziri Mkuu wa Israel, Ariel Sharon, ilikuwa ni adhabu kutoka kwa Mungu kutokana na mabavu yake katika Ukanda wa Gaza.

Robertson amekuwa ni mtu wa vituko na kauli tata katika maisha yake. Amewahi kuiponda dini ya Kihindu kuwa ni ya mapepo, watu katili na mashetani, huku akiita dini ya Kiislamu kuwa ni ya ibilisi.

Robertson amewahi pia kutoa kauli nyingi za kulaani harakati za kuleta usawa wa kijinsia, ngono za jinsia mmoja na hata utoaji mimba.

Zaidi ya kauli zake za kisiasa na kijamii, zilizozua mijadala, Robertson na mhubiri mwenzake Jerry Falwell walizua mjadala mwingine kuhusu mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Marekani. Walizua mjadala huo walipotoa kauli tata 11 Septemba, 2001, kwamba mashambulizi hayo yaliwezeshwa sana na wapagani, watoa mimba, wanaharakati wa usawa wa kijinsia na mashoga.

Wahubiri hao wawili wa Neno la Mungu baadaye walilazimika kuomba radhi kutokana na kauli hizo zilizovuta hisia kali miongoni mwa Wamarekani na kwingineko duniani.

Takribani wiki mbili baada ya kimbunga cha Katrina, kilichotokea 29 Agosti, 2005, na kuua watu 1,836, Pat Robertson aliibuka na kauli kuwa hiyo ilikuwa ni adhabu kutoka kwa Mungu, kutokana na sera za utoaji mimba za Marekani.

Mnamo 9 Novemba, 2009, Pat Robertson alisema kwamba Uislamu ni mfumo wa kisiasa unaotumia nguvu, uliolenga kuziangusha serikali duniani. “Mnapambana siyo tu na dini, bali pia na mfumo wa kisiasa. Kwa hiyo tuwachukulie waumini wa Uislamu sawa na Wakomunisti na vikundi vya kifashisti.”

Kauli za Robertson kuhusu matetemeko ya nchini Haiti mwaka huu, pia zimezua mjadala. Anasema kuwa waasisi wa Haiti waliingia mkataba wa kishetani ili kujitawala kutokana na utumwa wa Kifaransa. Kwamba matetemeko hayo ni adhabu dhidi yao kuhusu mkataba huo.

Watu mbali mbali maarufu kutoka kwenye makanisa walipinga kauli hiyo ya Robertson, wakisema haikufuata wakati, isiyojali janga dhidi ya Haiti, na kwamba haiwakilishi msimamo wa Wakristo.

Mwishoni mwa mwaka 1976, Robertson alitabiri kwamba mwisho wa dunia ungefika Oktoba au Novemba 1982. Mei 1980 alisema, “nawahakikishieni kwamba ifikapo mwisho wa mwaka 1982 kutakuwa na hukumu dhidi ya ulimwengu.”

Jina lake kamili ni Marion Gordon "Pat" Robertson. Alizaliwa 22 Machi, 1930 eneo la Lexington,Virginia. Shughuli inayochukua muda wake mwingi ni uinjilisti. Ana mke aitwaye Adelia Elmer. Amejaliwa kupata watoto, Robertson, Anne Carter na Absalom Willis.

Ni muasisi wa taasisi kadhaa, kikiwamo kituo cha sheria na haki, mtandao wa matangazo ya Kikristo, Chuo Kikuu cha Regent na taasisi nyingine nyingi. Ni muumini wa madhehebu ya Kibatisti. Amekuwa kiongozi katika dhehebu hilo kwa miaka mingi.

Aliwahi kuwania nafasi ya mgombea urais wa Republican mwaka 1988, lakini hakufanikiwa.

Baba yake Absalom Willis Robertson alikuwa ni seneta wa chama cha Democratic. Mama yake anaitwa Gladys Churchill. Alimwoa Adelia "Dede" Elmer 26 Agosti, 1954.

Alipokuwa na umri wa miaka 11, aliingia shule ya awali. Kuanzia mwaka 1940 hadi 1946 aliingia shule iitwayo McCallie, iliyopo HYPERLINK "http://en.wikipedia.org/wiki/Chattanooga,_Tennessee" \o "Chattanooga, Tennessee" Chattanooga, Tennessee. Alifaulu vizuri masomo yake na kujiunga na Chuo Kikuu cha Lee kilichopo Washington. Somo lake kuu lilikuwa ni historia.

Mwaka 1948, Robertson alijiunga na jeshi la maji la Marekani. Alihudhuria mafunzo ya kijeshi na kutunukiwa kamisheni, akiwa na cheo cha Luteni Usu.

Kwa ujumla historia ya Robertson imejaa vituko na kauli tata ambazo amekuwa ama akilazimika kuzitetea au kuomba radhi. Kuingia kwake katika Baraza la Seneti kunaweza kuleta changamoto nyingi zaidi.

0
No votes yet