Rais mpya Misri azua mvutano


Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 31 July 2012

Printer-friendly version

MVUTANO mpya wa madaraka umeibuka nchini Misri baada ya Rais Mohamed Mursi kubatilisha uamuzi wa maofisa wa jeshi wa kulivunja Bunge.

Jeshi lilitoa amri ya kulivunja Bunge kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu ya Kikatiba iliyotolewa mwezi uliopita. Uamuzi huo wa Rais Musri unaibua mvutano kati yake ya jeshi pamoja na mahakama.

Hata hivyo, siku moja baada ya Rais Mursi kutangaza hatua hiyo, Mahakama Kuu ya Katiba imetoa taarifa kwamba uamuzi wake wa kulivunja Bunge ni wa mwisho na unapaswa kutekelezwa bila kuhojiwa.

Hatua hiyo ya Mahakama Kuu ya Katiba inaonyesha kuibuka mvutano mkubwa na rais huyo mpya ambaye alitoa amri ya kubatilisha amri ya kuvunjwa Bunge.

“Maagizo na maamuzi yaliyotolewa ni ya mwisho wala hayawezi kukatiwa rufani kama ilivyoelezwa katika sheria. Maamuzi haya na maelezo yanapaswa kufuatwa na mamlaka za serikali,” ilieleza taarifa ya mahakama baada ya kikao cha dharura juzi.

Vilevile, Farouk Soltan, ambaye ni jaji mstaafu alisikika akisema kuwa uamuzi wa Musri hauna msingi wa kisheria. Soltan alikuwa akizungumza na mtandao wa magezeti ya taifa Al-Ahram.

Hatua hiyo ilifikiwa saa chache baada ya Spika wa Bunge, Saad al-Katatny, kuliita Bunge linalotawaliwa na wabunge wengi wa Kiislamu kuanza mikutano yake kuanzia jana Jumanne.

Akionyesha kuheshimu maamuzi ya mahakama, Katatny alisema kazi ya kwanza ya Bunge hilo ingekuwa kuangalia utekelezaji wa uamuzi wa mahakama uliotolewa na mahakama mwezi uliopita ambapo baadhi ya vifungu vinakiuka katiba.

Mbali ya mahakama kufanya kikao, taarifa za vyombo vya habari zinasema, viongozi wa jeshi waliojilimbikizia madaraka pia walifanya mkutano wa ghafla kujadili azma ya kulivunja bunge.

Aidha,  Mursi aliagiza Jumapili iliyopita Bunge likutane akilenga moja kwa moja kutoafikiana na maofisa wa jeshi ambao walimkabidhi rais huyo madaraka 30 Juni mwaka huu.

Jeshi lilichukua madaraka ya kuiongoza Misri tangu yalipofanyika mapinduzi ya wananchi yaliyomwondoa Hosni Mubarak. Lakini, siku chache kabla ya kukabidhi  madaraka kwa Musri, jeshi lilijipa mamlaka zaidi ya rais.

Uamuzi ya Musri ulikuwa ukilenga katika kurudisha mikononi mwake mamlaka yaliyoporwa na jeshi kwa kutaka bunge, linalotawaliwa na wafuasi wengi wa chama chake cha Muslim Brotherhood.

Taarifa za vyombo vya habari zinasema kuwa baada ya kipindi kifupi cha kuwa madarakani, Mursi ameamua kudhibiti mamlaka yake huku akitumia itikadi ya Kiislamu ili kuondoa maofisa hao ambao inaonekana kuwa na chembechembe za utawala wa Mubarak.

Msimamo wake huo pia unalenga katika kuimarisha mfumo wa kisheria ambao utamwezesha Mursi kuwa na mamlaka zaidi dhidi ya maamuzi ya mahakama ya sheria ya kuvunja bunge, na kujenga uchumi wa nchi hiyo ambao umezorota kutokana na mtikisiko wa kisiasa uliodumu kwa miezi 17.

"Rais Mohamed Mursi ameagiza bunge kukutana na kuanza vipindi vyake," alisema Yasser Ali mmoja wa wasaidizi wa  Mursi.

"Jeshi lilitaka kuvunja bunge wakati Brotherhood hawaikutaka iwe hivyo," alisema Shadi Hamid wa kituo cha Brookings Doha.

Saad Husseini, ambaye ni mfuasi wa chama cha Udugu wa Kiislamu – Muslim Brotherhood, alisema kuwa hakuamini kama jeshi linaweza kupingana na maamuzi ya Mursi.

"Tuna imani kuwa jeshi halitaiingiza nchi katika machafuko ya kisiasa," alisema.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa walisema kuwa hawakutegemea kuwepo na mahusiano ya kirahisi kati ya jeshi na rais, lakini wakiamini kuwa

0
No votes yet