Rekodi ya kuzama kwa meli


Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 30 May 2012

Printer-friendly version
Ripoti Maalum

MIAKA mitatu iliyopita, injini za meli ya mv Butiama zilizimika ikiwa karibu na bandari ya Mwanza. Ikaelea kwa zaidi ya saa mbili huku abiria wakihaha bila msaada.

Ilifahamika baadaye kuwa meli hiyo haikuwa na mawasiliano ambayo yangetumika kupata msaada wa haraka.

Meli nyingine ya mizigo, mv Nyamageni ilizama ziwani Victoria ikiwa na abiria zaidi ya 20 waliosafirishwa pamoja na masanduku ya soda kwenda visiwani.

Februari mwaka huu, mv Pacific iliyokuwa ikisafiri kati ya Mwanza na kisiwa cha Ghana, ilizama. Ilikuwa na abiria 17. Mmoja alifariki. wengine 16 waliokolewa.

Kwa mujibu wa Sumatra, boti iliyokuwa na abiria 31 ilizama huko Musoma, mkoani Mara. Abiria wote waliokolewa kwa kutumia zana za uokozi.

Ofisa Mwandamizi wa Sumatra, Alfred Wariana  anasema, katika ajali tatu za “karibuni,” bila kutaka kutaja karibu kiasi gani; kati ya watu 81 waliokuwa katika boti, ni mmoja tu aliyefariki dunia. Anasema hii inaonesha sheria zimeanza kufuatwa.

Anasema maofisa wake wanakagua vyombo vya majini kabla ya kuanza safari ili kuthibitishwa usalama wake.

Wariana anajigamba kwamba usafiri katika Ziwa Victoria ni “salama zaidi kuliko barabarani.”

“Usafiri wa barabarani, hata wa ndege hapa Afrika, ndiyo ‘moving coffins’ (majeneza yanayotembea). Barabarani kuna magari na  pikipiki zinazochinja watu kila siku”, anasema Wariana.

0
No votes yet