Romney: Obama anafanya kampeni ‘chafu’


Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 18 July 2012

Printer-friendly version

KAMPENI za urais nchini Marekani zimeingia patamu baada ya mgombea kupitia chama cha Republican, Mitt Romney kumshutumu rais wa sasa, Barack Obama kuwa anafanya kampeni "za uongo na zisizo na uwazi."

Pia, Romney ametupilia mbali mapendekezo kadhaa, yakiwemo ya baadhi kutoka kwa wafuasi wa chama cha Republican kwamba Obama atoe muda zaidi wa marejesho ya kodi ya mapato.

Aidha, katika mahojiano yaliyofanyika juzi Jumatatu na kituo cha Fox & Friends, mgombea huyo amepinga tuhuma zilizotolewa na Meya wa jiji la Chicago, Rahm Emmanuel, ambaye alimtuhumu Romney kwa “kupinga” mashambulizi juu ya rekodi zake katika mji wa Bain.

"Nafikiri watu wakikushutumu kuwa umetenda uhalifu una sababu ya kwenda mbele yao kwa nguvu, na nitaendelea kusonga mbele yao," alisema Romney, akisisitiza kuwa mashambulizi ya Obama  “hayana mwelekeo na ukweli."

"Ni nini kinaweza kusemwa juu ya rais ambaye rekodi zake ni mbaya kiasi kwamba kitu anachoweza kufanya kwenye kampeni ni kunishambulia mimi?" alihoji.

Vilevile, Romney anasema kuwa kampeni “chafu” anazozifanya Obama hazitadumu kamwe. Hata alipoulizwa iwapo angefanya fujo katika kupinga mashambulizi ya chama cha Democrats juu ya rekodi zake, gavana huyo wa zamani alijibu “Kosa pekee ni kuangalia rekodi za rais."

"Isingeshangaza, kwa rais, kama unatumia sehemu ya muda wako katika kuangalia rekodi zako," alisema Romney.

Mashambulizi ya Obama "yanaweza kufanikiwa kwa Chicago lakini kamwe hayatafanikiwa kwa nchi nzima ya Marekani," aliongeza Romney.

Romney aliyapuuza pia mapendekezo yakiwemo kutoka kwa baadhi ya wanauchumi kwamba atatakiwa kutoa miaka miwili zaidi ya marejesho ya kodi yake ya mapato, akisema kuwa itakuwa kama kumpa Obama risasi nyingine katika kampeni zake.

"John McCain aliwania urais na alipendekeza mpango wa miaka miwili ya marejesho ya kodi ya mapato. John Kerry aliwania urais na mke wake aliyekuwa na mamia ya mamilioni ya dola, hakutoa miaka ya kurejesha kodi yake ya mapato. Kwa namna nyingine hilo halikuwa suala kwake," Romney aliiambia Fox News.

Aidha, Romney alisistiza kuwa Marekani ipo makini juu ya uchumi na kazi zaidi ya “mashambulizi” na kwamba watu wa Obama wanataka kupata vitu vingi zaidi na zaidi.

"Suala ambalo watu wako makini nalo ni kuona nani anayeweza kuinuia uchumi ili uwasaidie watu kuwa na maisha bora hapo baadaye," alisema Romney.

Matamko hayo ya Romney yamekuja wakati kampeni zake zikipigwa vita na kampeni za Obama wiki iliyopita. Siku ya jumatatu, kampeni za Romney zilikuwa zinaelekeza lawama kwa rais Obama kwamba amekuwa akifanya kampeni kwa chama chake badala ya kusimama katika nafasi ya kati bila kupendelea chama chochote.

"Tunapaswa kuwa na uchumi ambao wanasiasa ndani ya Marekani, wanafanya majadiliano kuhusu wapi uwekezaji unaenda na wapi…dola za walipa kodi zinatumika kulingana na kuunganishwa kwa watu na kiasi gani cha pesa kiliongezeka katika mzunguko wa kampeni zilizopita?" alihoji Ed Gillespie, mshauri wa Romney wakatia akizungumza na waandishi wa habari.

“Au unataka uchumi ambao unaendeshwa na maamuzi ya wawekezaji wa sekta binafsi katika kuruhusu watu kutumia zaidi ya wanavyoingiza na kufanya maamuzi yao binafsi?" alihoji zaidi Gillespie

0
No votes yet