Ujumbe wa walimu kwa CWT


Joster Mwangulumbi's picture

Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 27 April 2011

Printer-friendly version
Mtazamo

MAKALA ya wiki iliyopita iliyokuwa na kichwa “CWT wakomboeni walimu” imeamsha hasira za walimu dhidi ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Baadhi wamelaani makala kwamba inawabeba CWT, wengine wamemlaani mwaandishi kwa madai aliandika jambo asilolijua. Pwani wamesema wanafuata nyayo za Kigoma.

Kwa kifupi, walimu takriban wote walionipigia simu au waliotuma ujumbe kwa ‘sms’ wanauchukia uongozi wa CWT. Ujumbe wao ni huu:

 

 “Nimefurahishwa sana na walimu wa Kigoma kutaka kujitoa; madai yao ni ya kweli kabisa. Kwa mfano, viongozi wanajilipa posho zaidi ya Sh. 700,000 bila makato yoyote. Tuna vitegauchumi Dar es Salaam na Mwanza, vinafanya kazi, lakini makato ya asilimia mbili yapo palepale! Kwa nini walimu wasiandamane? Nakuomba ufuatilie vitegauchumi hivyo ubaini ukweli,” unasema ujumbe kutoka simu 0789084104.

“Hao CWT tunawachangia pesa nyingi sana, kwa nini hawatoi hata mikopo ya bei nafuu kwa wanachama? Pesa zote na vitegauchumi ni kwa faida ya nani? Wizi mtupu!” 0755911149.

“Joster Mwangulumbi, hujatuelewa vizuri walimu wa Kigoma, naomba unihoji,” anasema 0652145693.

“Kichwa cha habari kinavutia ila content  yako inajaribu kutetea CWT. Walimu tunachohitaji ni ukombozi wa kimaslahi na kihadhi. Chama kinawezaje kuongoza wafanyakazi ambao mshahara wao hautoshi mzunguko wa siku 18 ndani ya mwezi? Viongozi wanapogeukia uwekezaji usio na tija kwa wanachama na kuacha malengo ya kuwakomboa na kutetea maslahi yao ndipo tunaona bora kujiondoa na kubakia bila chama au kuanzisha uasi kama FIBUCA dhidi ya TUICO.

“Kuendelea kuitegemea CWT ambayo viongozi wake ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni upuuzi. Hata migomo yao ni stageboycotts. Rais anatangaza mgomo,  katibu mkuu na naibu wake watasema hakuna mgomo ili walimu wachanganyikiwe na wasigome.” “Nisikuchoshe sana ila chama chetu hakiko serious na matatizo ya walimu.

CWT wilayani makatibu wengi wamefunga ‘ndoa’ na halmashauri, hata ukipeleka matatizo wanakushauri tu na hawataki kujiingiza moja kwa moja kwenye utatuzi wa tatizo lenyewe, kwa sababu wanakula na kunywa na maafisa elimu na wakurugenzi wa halmashauri.” 0786243723.

“Baada ya miaka mitano, kama chama kitabaki kuwa cha kulilia madeni tu uasi utazidi ila hongera kwa kujitokeza kusema juu ya mgogoro wa walimu na CWT dhaifu,” 0786243723.

“Pamoja na mafanikio hayo ambayo umeandika kama mafanikio ya CWT, ukubali kwamba chama hicho kimeshindwa kusimama kidete kutetea maslahi ya wanachama wake hasa walimu wanaoanza kazi.

“Mwalimu anazalisha wasomi, viongozi, watawala na wataalamu wa fani mbalimbali, lakini anaishi maisha ambayo yanazidiwa hata na mpigadebe Uvumilivu wa walimu unakaribia kufika mwisho.” 0769116000.

“Hayo maoni uliyotoa naona kama umetumwa, kwani walimu wa Kigoma wako sahihi sana. CWT hakifanyi kazi yoyote ya kumtetea mwalimu,” 0684713374.

“Nimeacha ualimu baada ya miaka 10, nimeajiriwa na TCC. CWT ni wasaliti siwapendi.” 0718144025.

“Mimi ni mmoja wa walimu ambao hatuoni faida ya CWT. Viongozi wanajinufaisha wenyewe. Makatibu wa wilaya ndo kabisa, na hivi ni wa kuajiriwa heri wangekuwa wa kuchaguliwa. Mimi mwenyewe nadai malimbikizo ya mshahara kuanzia Novemba 2001 hadi Oktoba 2005 sijalipwa na nilishakata tama; sijapanda daraja tangu mwaka 2004 mpaka leo. Kuna haja gani kuwa na CWT?”

“CWT haina maana kabisa kwa walimu zaidi ya kuendelea kuwatafuna hata kwa kile kidogo tunachopata. Hakina utetezi wowote kwa walimu.” 0715171715.

“Si kweli kwamba walimu wamelipwa malimbikizo yao, bado wanadai. Pili tunataka hesabu za mapato na matumizi ziwekwe wazi,” 0762812983.

“Nakuombea kwa Mungu akufunulie na akujalie hekima kwa kutukumbuka walimu,” 0788982516.

Meseji ziko nyingi ila nafasi ndogo. Naibu Katibu mkuu wa CWT, Ezekiel Oluoch naye anasema, “Nimesoma mawazo yako kwenye MwanaHALISI ya leo, uk 4 tutayafanyia kazi.” 0764189904

0
No votes yet