Unataka uponyaji? Nenda Namibia


Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 06 June 2012

Printer-friendly version

WAUMINI wa dini ya Kikristo waliozoea kukimbilia miujiza ya uponyaji kutoka kwa wachungaji mbalimbali wamekumbana na mambo mazito.

Badala ya kupokea uponyaji raia wanne wa Namibia na wawili kutoka Angola hivi karibuni walipokea uponyaji wa kitumwa baada ya kujikuta walifungwa minyororo kwenye mawe na magogo.

“Uponyaji” huu wa kitumwa unapatikana katika kanisa la Mitume lililoko Sauyemwa katika mji wa Rundu, eti kwa sababu “ni hatari kwa jumuiya hiyo”.

Mchungaji Moses Matyayi wa kanisa hilo amekuwa akifanya hivyo, lakini amewaongeza raia hao wane wa Namibia na wawili wa Angola akiwemo mwanamke aliyefuata ‘tiba ya uponyaji’ kutokana na ugonjwa usiojulikana.

Mchungaji huyo anayesifiwa sana kutokana na ‘kipawa’ anasema baadhi ya wamuni wake waliofungwa kwenye mawe na magogo ni kwa lengo la kuzuia wasitoroke na anasema hatawaachia mpaka wawe wamepona kabisa.

Anasema jamii ya leo imejaa aina zote za magonjwa na matendo mabaya. Kiongozi huyo wa kanisa anayefanya kazi za kuhubiri na kliniki ya uponyaji anasema kwamba wagonjwa wake wanapata shida kwa vile kanisa lake halipati msaada kutoka kokote.

Matyayi amewaambia waandishi wa habari kwamba “amewaponya” watu wengi siku za nyuma kwa maombi tu.

"Wengi walikuwa wanakuja hapa wakitembelea fimbo na magongo, lakini ukiwatimua leo, hawarudi tena,” anaeleza mchungaji huyo.

Akionyesha rundo la fimbo na magongo, alisema watu wanachoshwa na tiba za hospitalini na za kienyeji na pale wanapokwenda kwake kwa maombi, maumivu yote na ulemavu unabaki kuwa historia.

Kwa mujibu wa mchungaji huyo, wagonjwa wengine wanaokwenda kwake kwa ajili ya maombi, wanatoka sehemu mbalimbali za Namibia na hata Angola.

"Vitu hivi vyote unavyoviona walikuja navyo wagonjwa kutoka kwa waganga wa kienyeji na wakishapona wanaviacha hapa hapa,” alisema.

Miongoni mwa waliofungwa kwenye magogo ni watu wanne wanaosadikiwa wamerukwa akili kwa lengo la kuzuia wasikimbie.

Serikali haina habari. Mratibu wa makosa ya jinai mkoa wa Kavango, Kamishna msaidizi, Willie Bampton, amesema kwamba polisi hawana habari na shughuli hizo katika kanisa hilo ambako watu wanaosumbuliwa na magonjwa ya akili wanafungwa kwa minyororo.

Ofisa ustawi wa jamii katika wizara ya jinsia na watoto, Fransiska Hamutenya, amesema huo ni “udhalilishaji”.

0
No votes yet