Usalama wa Taifa wabinafsishwa


Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 01 July 2008

Printer-friendly version
Serikali yaingizwa mkenge
Siri sasa zaanza kufumuka
Rais Jakaya Kikwete

KAMA kampuni ya Meremeta Limited inahusika na ulinzi na usalama wa taifa, kama alivyoeleza Waziri Mkuu Mizengo Pinda, basi usalama wa nchi umebinafsishwa , MwanaHALISI limeelezwa.

Ijumaa wiki iliyopita, Pinda aliliambia Bunge kuwa hawezi kujibu hoja zozote juu ya kampuni ya Meremeta, hata akisulubiwa, kwa sababu kampuni hiyo inahusiana na jeshi na 'ulinzi na usalama wa taifa.'

Lakini nyaraka na taarifa mbalimbali ilizonazo MwanaHALISI, zinaonyesha kuwa asilimia 50 ya hisa za kampuni ya Meremeta, zinamilikiwa na wageni.

Kwa msingi huo, 'ulinzi na usalama wa taifa' umo mikononi mwa makampuni ya kigeni ambayo yana ubia katika Meremeta.

Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kukiri kuwa usalama wa taifa umo mikononi mwa raia wa kigeni. Hii pia ni mara ya kwanza wananchi wa Tanzania kuelezwa kuwa ulinzi na usalama wao unategemea makampuni ya kigeni.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizoko mikononi mwa gazeti hili, wabia wa Meremeta ni pamoja na kampuni ya Trienex (Pty) ya Afrika Kusini yenye hisa 50.

Wabia wengine ni PC-London Law Service na London Secretarial Service ambazo ni za Uingereza na Afrika Kusini, na kila moja ina hisa moja.

Taarifa za makampuni haya zinaonyesha kuwa watia saini kwenye akaunti ya Meremeta iliyoko NBC Bank Limited mjini Musoma, ni Anthony A. Jafferies, Jan H. Duvenage, Doglas N. Geyser na Roy Dias.

Watia saini wote waliotajwa ni raia wa kigeni ambao haikuthibitika wanaweza vipi kukabidhiwa jukumu la kuweka ulinzi na usalama wa Tanzania.

Hawa ndio Pinda alisema hawezi kujadili kampuni yao kwa kuwa inahusika na ulinzi na usalama wa taifa.

Meremeta imekuwa ikichimba dhahabu katika eneo la Buhemba, Musoma mkoani Mara kwa miaka saba sasa bila ya kutoa mchango wowote kwa maendeleo ya wilaya ya Musoma kama makampuni mengine yatoavyo huduma kwa wananchi wanaoishi maeneo ya machimbo.

Taarifa zinasema kampuni ilifungua akaunti yake ya benki Na. 030105000364 tarehe 1Januari 2002 na hadi 20 Juni 2008 ilikuwa na akiba ya dola za Marekani 9,622.8.

Hii ni baada ya akaunti hiyo kufanya maingizo ya karibu dola 80,000,000 sawa na zaidi ya Sh. 96 bilioni ambazo hazijawahi kuonyeshwa kwenye bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Miongoni mwa maelfu ya waliolipwa na Meremeta, kwa ushahidi tu, ni pamoja na Caltex Tanzania Limited (dola 260,283.28 = Sh. 312 milioni); GSI LUCH UNI (Euro 167,131.79), Major Drill STD (dola 125,671.60) na fedha nyingine dola 123,200.00 kupelekwa benki ya Chase Manhattan, Marekani.

Miongoni mwa walioingiza fedha katika Meremeta ni Jeffares and Green (dola 1,476,336.00) ya tarehe 24 Februari 2005. Jeffares and Green ndio wanaonekana kuwa wawekaji fedha nyingi na mara nyingi katika akaunti ya Meremeta.

Haikuwezekana kufahamu mara moja wanaoweka fedha nyingi kiasi hicho katika akaunti hii ni nani. Ni serikali pekee inayoweza kuthibitisha iwapo na hao ni wabia katika ulinzi na usalama wa taifa.

Wakati Pinda anasema Meremeta ni kampuni ya 'ushushushu' ya serikali, taarifa zinasema kuwa Kamati ya Rais Jakaya Kikwete ya kuchunguza mfumo wa mikataba ya madini chini ya Jaji Mark Bomani, iliona mkataba wa Meremeta na kubaini haikuwa kampuni inayohusu ulinzi na usalama.

Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Beno Ndullu amekaririwa akiiambia Kamati ya Bomani kuwa serikali ilikopa Sh. 14 bilioni kutoka benki yake kuipa Meremeta, chini ya mfumo wa dhamana ambao serikali inalipa riba ya asilimia 14 kwa mwaka.

Awali, taarifa zinasema, Meremeta ilikuwa chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na siyo Idara ya Usalama wa Taifa. Ilikuwa ikimilikiwa na kampuni ya jeshi ya Suma JKT.

Mwaka 2002 iliondolewa chini ya Suma na kupelekwa Hazina ambako baadaye ilikabidhiwa kwa Wizara ya Nishati na Madini.

Wakati kuna taarifa kuwa sasa Meremeta imefunga shughuli zake kwa kufilisiwa, na kwamba shughuli zake ziko chini ya kampuni ya Tangold Limited, bado akaunti za Meremeta zinafanya kazi chini ya jina hilohilo la Meremeta Limited.

Ni Meremeta inayodaiwa kufilisiwa na kurithiwa na Tangold, ambayo inadaiwa kuchotewa mabilioni ya shilingi na serikali katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005; tena kwa kazi ambayo haijawahi kuelezwa.

Kumekuwa na mzunguko wa fedha kati ya Tangold, serikali na Meremeta, kiasi kwamba kuna wakati Tangold, inayodaiwa kuwa ya serikali, lakini imekanwa na Msajili wa Hazina, imeipa Meremeta kwa wakati mmoja dola 13.3 milioni tarehe 8 Oktoba 2005.

Aidha, tarehe 8 Desemba 2005, Tangold iliilipa Meremeta Sh. 100.9 milioni. Fedha hizo na zile za awali hazijajulikani zilitumika kwa shughuli ipi.

Katika hali hii, yawezekana Waziri Mkuu ameingizwa kwenye 'mkenge;' kutetea ambacho hakijui,

0
No votes yet
Soma zaidi kuhusu: