Utuki wa matukio Malawi, Zambia


Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 16 May 2012

Printer-friendly version

DOKTA Kenneth Kaunda, rais wa kwanza wa Zambia kati ya mwaka 1964-1991 na Dk. Kamuzu Banda aliyekuwa rais wa Malawi kati ya mwaka 1961-1994 wote kwa pamoja walikuwa marais kwa muda mrefu katika nchi zao lakini asili yao kwa namna fulani si katika nchi hizo.

Kaunda na Kamuzu, wakati wa uongozi wao walikuwa wanatumia kaulimbiu ya "Wamuyaya" (yaani kutokuwa na kikomo), walikuwa na kitu walichobeba mikononi mwao kama alama ya kuwa na mamlaka.

Frederick Chiluba, aliyekuwa rais wa Zambia baada ya kumng’oa Kaunda alizaliwa mwaka 1943, wakati Bakili Muluzi aliyechukua nafasi ya urais kutoka kwa Kamuzu Banda nchini Malawi alizaliwa mwaka 1943.

Chiluba na Muluzi kwa pamoja walikuwa wakipigania kuendelea kuwa madarakani kwa awamu ya tatu lakini jitihada zao zilishindikana baada kupata upinzani toka pande mbalimbali.

Katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu Chiluba alimteua Levy Mwanawasa kuwa mrithi wake na alishiriki kumpigia kampeni wakati Muluzi alimteua Bingu wa Mutharika ambaye pia alimpigia kampeni. Mwanawasa na Mutharika wote kwa pamoja walishinda katika chaguzi hizo.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kuchaguliwa kuwa rais, Mwanawasa hakuonyesha shukrani wala upendeleo kwa Chiluba na kuamua kumpeleka mahakamani kwa tuhuma za kuhusika katika rushwa. Naye Mutharika aliamua kumpeleka Muluzi kortini kwa tuhuma za rushwa.

Kwa hiyo, Chiluba alishtakiwa katika uongozi wa  Mwanawasa na Muluzi alishtakiwa chini ya uongozi wa Mutharika.

Mwanawasa alishinda muhula wa pili na kuendelea kuwa rais wa Zambia; Mutharika naye alishinda muhula wa pili na akaendelea kuwa rais wa Malawi. Baada ya ushindi huo, Mwanawasa alimchagua Rupiah Banda kuwa makamu wa rais, wakati Mutharika alimchagua Joyce Banda kuwa makamu wake.

Mwanawasa alifariki katika kipindi cha pili cha uongozi wake kutokana na ugonjwa wa ghafla wa mapigo ya moyo, naye Mutharika alifariki katika kipindi cha pili cha uongozi wake kwa ugonjwa kama uliomuua Mutharika.

Vifo vyote viwili vilitabiriwa na nabii maarufu wa Nigeria, TB Joshua.

Baada ya vifo hivyo, Rupiah Banda alichukua madaraka kutoka kwa Levy Mwanawasa kumaliza muda wake wa uongozi, na Joyce Banda amechukua madaraka kutoka kwa Bingu wa Mutharika baada ya kifo chake.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba watu waliochukua madaraka ya marais hao waliofariki dunia, majina yao yanafanana yaani "Banda".

Kuna hili pia, baada ya miaka mitatu, rais Banda wa Zambia alipoteza nafasi yake iliyochukuliwa na aliyekuwa kiongozi mkongwe wa upinzani nchini humo Michael Sata. Joyce Banda ambaye amechukua madaraka ya urais atakabiliwa na uchaguzi wa rais mwaka 2014 ambapo atakuwa ameishatumikia miaka mitatu ya urais wa nchi hiyo.

Je atapoteza nafasi hiyo kwa kiongozi mkongwe wa upinzani nchini humo John Tembo?

0
No votes yet