Wasomaji nao wanayao


Joster Mwangulumbi's picture

Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 21 September 2011

Printer-friendly version
Wazo Mbadala

HIVI ndivyo baadhi ya wasomaji walivyoona inafaa kutoa hisia zao kwa meseji baada ya kusoma makala iliyouliza “Serikali ina ndoa na wakristo?”

Makala ilichapishwa hapa katika toleo la wiki iliyopita.

Wewe ni mbwa tena unaf… na nguruwe, mmekalia kutuhujumu waislamu tu k…la…yako. Mnachokitafuta kwetu (waislamu) mtakipata. Nenda Tigo ukachukue ‘details’ zangu ili nikamatwe kwa kukutukana. Fanya haraka m… yako. 0658656753.

Wakristo bila serikali hawana chao. Yote hii imetokea mbali tokea mkutano wa Berlin 1884/1885. Sumu kubwa ni makubaliano maalumu baina ya serikali na makanisa (Memorandum of Understanding – MOU) ya mwaka 1992. 0714600816.

Sina hakika kama serikali iliyochaguliwa kidemokrasia na watu wa dini zote inaweza kufanya hivyo hata siku moja. Lakini sijui pia kama serikali inatoa ruzuku kwenye taasisi za dini zaidi ya msamaha wa kodi. 0788032481.

Bajeti ya serikali hutangazwa kila mwaka bungeni. Mimi sijawahi kusikia wizara ikitenga fedha kwa ajili ya taasisi za dini ya kikristo. Hao waongo. 0713263587.

Hebu waulize waislamu wenzangu wanaokulalamikia, kile kiwanja cha Chang’ombe Temeke walichopewa na serikali ili kijengwe chuo kikuu cha Kiislamu Afrika Mashariki na Kati, mbona wameuza tena kihuni? Wanataka serikali ifanye nini? Ama wanadhani hayo si makubaliano?

Ninavyowafahamu ninyi wakristo suala la MOU lingekuwa limefanywa na waislamu ingekuwa kelele magazetini kila siku hadi bungeni kwamba katiba imevunjwa ila kwa waislamu sawa. Kuna mahakama za biashara na za kazi zinatumia kodi zetu mbona wakulima hawalalamiki? Iweje mahakama ya kadhi iwe nongwa wakati zinahudumia asilimia 50 ya Watanzania wenzenu? Wakristo kubalini na mambo mazuri ya wenzenu. 0715565788.

Hawa waislamu waache chokochoko, kama mahakama ya kadhi ina maslahi kwao basi waanzishe na wasimamie wao wenyewe kama alivyosisitiza Rais Jakaya Kikwete, wasitegemee fedha za walipakodi wote zitumike kuendesha mahakama ya kadhi.  0687558505.

Jamani matatizo yaliyoko kati ya BAKWATA na serikali isiwe sababu ya kusema kuna udini. Kupandikiza mbegu hizo kwa watu ambao hawana mawazo kama haya, ongeleeni masuala haya bila kutaja haya mambo, oneni mfano wa Nigeria, kuweni na fikra za kujenga taifa siyo tu ili gazeti lisomwe. Tanzania itabaki daima kuwa moja. 0714585553.

Masuala ya dini ni magumu sana, ninaamini yatakuwepo hadi kiama. 0717178198.

Wakristo hawajajenga shule wao wenyewe, wamepewa fedha nyingi sana na serikali tangu enzi za Mwalimu Nyerere hadi sasa ili wajenge shule na makanisa. Waislamu hawajapewa hata senti tano. 0716466221.

Waislamu kazi yao kulalamika tu kwamba wanaonewa, wajenge shule. Si kweli kwamba wakristo wanapewa fedha na serikali ila wanachangishana fedha kwa ajili ya kujenga makanisa, vyuo, shule na hospitali. 0759399256.

Waislamu wanachekesha, wanasema hawaitaki Bakwata kwa sababu imeundwa na serikali sasa kwa nini wanataka mahakama ya kadhi iundwe na serikali? 0712853680.

Muhimu, waislamu katika nchi hii hawalalamiki bure. Kushabikia upande wa pili ni kupanda mbegu za vita. Unyonge wa waislamu una majibu ya kihistoria pamoja na kupuuzwa na serikali yao. 0757125596.

Ni kweli mfumo kristo ndio unaoendesha nchi hii. Pamoja na upendeleo maalum, anguko la CCM na Bakwata ni lazima. 0786555666.

Usiendeshwe na kulazimishwa na unafiki kaka, palipo na ukweli sema kwani ndiyo tiba mbadala. Wazoee tu kwani msema ukweli huchukiwa. Tuache udini. 0752316099.

Usiandike tena makala kama hizi za udini kwenye gazeti hili. 0753000018.

0658 383 979 jmwangul@yahoo.com
0
No votes yet